Mwanza: Wanafunzi watoro Shule za Msingi (19,133), Sekondari (7,594)

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Serikali Jijini Mwanza inatarajia kuanza zoezi la kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani ambao wamekithiri hususani katikati ya Jiji kuhakikisha wanarejea katika familia zao na kupata haki yao ya msingi ya kurejea shule.

Zaidi ya asilimia 90 ya watoto walio mitaani Jijini Mwanza wana umri wa kwenda shule lakini wanakosa haki hiyo ya kupata elimu kutokana na sababu mbalimbali ambazo zinazuilika.

Kaimu Afisa Elimu Mkoa Mwanza, Mwl. Maenda Chambuko amesema kuanzia Januari - Aprili, 2022 kuna wanafunzi watoro 19,133 katika Shule za Msingi, waliopo Shule ni 913,335 huku kwa Shule za Sekondari wanafunzi watoro wakiwa ni 7,594 na walio Shule wakiwa ni 222,132.

Hayo yamebainika katika katika kikao cha Kamati ya Kamati ya Kupambana na Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), Aprili 8, 2022. Naye, Afisa Maendeleo Mkoa Mwanza, Isack Ndassa ameshauri MTAKUWWA kushiriki zoezi la kuwabaini watoto walioacha shule na kukimbilia mitaani kwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu.

Baadhi ya viongozi wa kamati hiyo wamo Polisi Kata, Watendaji wa Kata, Maafisa Elimu Kata, Maafisa Maendeleo Kata, Maafisa Ustawi wa Jamii Kata na viongozi wa dini.

Kikao hicho kililenga kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuwaondoa watoto mitaani na kutokomeza utoro katika Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Mwanza.

Akifungua kikao hicho, Katibu Tawala Mkoa Mwanza Ngusa Samike ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ametaka uwepo mkakati wa kuwaelimisha wazazi na walezi ili wasiwe chanzo cha watoto wao kukimbilia mitaani.

Ameonya kuwa baada ya wazazi na walezi kupata elimu, watakaoshindwa kutoa ushirikiano ili kuhakikisha watoto wao hawakimbilii mitaani hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao hatua itakayosaidia kudhibiti wimbi la watoto kukimbia mitaani kiholela.

Samike amebainisha kuwa Serikali ya Rais Samia Sauluhu Hassan imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya sekta ya elimu ambapo katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, Mkoa Mwanza umepokea shilingi bilioni 20.5, hivyo si vyema watoto kukosa haki ya kupata elimu na kukimbilia mitaani.
4.jpg

Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Ngusa Samike (kushoto) akifungua kikao kazi cha Kamati ya MTAKUWWA Mkoa Mwanza kilicholenga kuweka mikakati ya kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani pamoja na kutokomeza utoto kwa wanafunzi mashuleni Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Katibu Tawala Mkoa Mwanza. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally na kulia ni Afisa Programu Mwandamizi wa Shirika hilo, Grace Mussa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally ameshauri mbinu rafiki kutumika wakati wa kutekeleza zoezi la kuwaondoa watoto mitaani pamoja na kutokomeza utoro mashuleni akishauri mbinu kama za utoaji uji ama chakula mashuleni kutumika ili kuhamisha watoto kupenda Shule.

Yassin ameshauri pia waalimu kuwa na mbinu rafiki kwa wanafunzi na kuacha tabia ya kuwashughulikia kwa adhabu kali kutokana na kukosa mahitaji ya shule ikiwemo sare ama viatu hatua itakayosaidia kupunguza utoro mashuleni. Pia ameshauri utaratibu wa kuwaondoa shuleni wanafunzi watoro ndani ya siku 90 kwani linakinzana na azma ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha wanafunzi kurejea shule.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza la Watoto Mkoa Mwanza, Glory Theonest amesema changamoto kubwa ambayo imekuwa ikisababisha utoro kwa wanafunzi hususani wa kike ni tabia ya baadhi ya waalimu kuwataka kingono na wanapokataa wanakuwa wanaadhibiwa vikali hata kwa makosa madogo na kuomba waalimu ambao pia ni walezi na wazazi kuwa marafiki wa wanafunzi na kuwasaidia kimasomo ili kufikia ndoto zao.

Kikao kazi hicho cha MTAKUWWA Mkoa Mwanza ni kikao cha kwanza katika kuweka mikakati ya kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani na kutokomeza utoro mashuleni ambapo vikao zaidi vitafanyika ili kuja na mbinu zitakazosaidia zoezi hilo linalotarajiwa kuanza kati ya mwezi Mei ama Juzi mwaka huu 2022 kufanikiwa.


Chanzo: Malunde
 
Watoto wanaacha shule baada ya kuona kaka zao waliosoma hawana ajira wala muelekeo wa maisha, wanaona bora wawe mtaani kuliko kupoteza muda, na sio Mwanza tu kuna tatizo la watoto kuacha shule Tanzania nzima.
 
Hii kitu niliiona mahali jana nikawa najiuliza maana wahudumu wa mgahawa flani ni vibinti tu ambavyo ukiwaangalia ni wa umri wa kwenda shule na wamependeza haswa.

Nikawa najiuliza.

1. Ni mimba za utotoni??

2. Ukosefu wa ada?? Ila mbona wanamiliki smartphone za bei ghali sana?? Kama anamiliki smartphone ya laki tano hawezi kosa ada ya mwaka mzima.

3. Makuzi mabaya. Kwamba mzazi hakuzingatia umuhimu wa elimu ya mtoto wake.
 
Watoto pekee wanaojielewa ni wa kimasai hawaendi shule wana utajiri wa mifugo wanachunga mifugo yao

Nafikiri ifike mahali tuachie tu kuwa kusoma iwe kitu cha hiari sio lazima
 
Hao madogo wamejiongeza mapema..wameona jinsi kaka na dada zao waliomaliza vyuo wanarudi home kugombea chai hawana nyuma wala mbele..sasa ya nini kupotenza miaka zaidi ya ishirini shuleni halafu unarudi kuanza zero.

Kijani wameua mfumo wa elimu na maendeleo kwa nchi hii shame on them.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ni kwel kabxa....jana napanda daladala Nata hapo....madogo wamezagaa pale kibao..mara waning'inie madirishan kuomba msaaada..kwa kwel ni kero
 
Back
Top Bottom