Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 121,947
- 95,237
Walimu wahamishwa kwa nguvu Mwanza
-
Halmshauri ya Jiji la Mwanza imewahamisha kwa nguvu kwenye nyumba walizokuwa wanakaa walimu wanne wa shule za sekondari Mlimani, Mapango na Pamba za Jiji hilo ili kupisha ukarabati unaotekelezwa na Serikali.
Zoezi la kuwaondoa walimu hao kwenye nyumba hizo limefanyika baada ya kukataa kuhama kwa hiari na kudai hawajalipwa fedha za kufunga mizigo.
Zoezi hilo limefanyika kwa kusimamiwa na askari mgambo.
Akisimamia zoezi hilo jana kwa niaba Mkurugenzi wa Jiji, Kiomoni Kibamba, Ofisa Mtendaji wa kata ya pamba, Jonas Mugisha amesema walimu hao wameondolewa kwa nguvu baada ya kukaidi amri ya kuhama kwa hiari kupisha ukarabati wa nyumba hizo.
Amesema walimu hao walipewa barua iliyokuwa ikiwataka kuhama kwenye nyumba hizo ili ziweze kukarabatiwa pamoja na shule hiyo kwani serikali imetowa Sh milioni 540.
Mmoja wa walimu hao, Abel Dendwa akizungumza kwa niaba ya walimu hao amesema inasikitisha kuona mfanyakazi wa umma anafanyiwa vitendo vya unyanyasaji nakwamba ni vema serikali ikaingilia kati suala hilo ili haki iweze kutendeka ikiwamo ya kulipwa fedha zao za kufunga mizigo.
Mtanzania