Mwanza walia na mgao wa umeme. Dodoma, Kagera wachekelea!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanza walia na mgao wa umeme. Dodoma, Kagera wachekelea!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Aug 18, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkoa wa mwanza umekumbwa na adha kubwa ya mgao wa umeme hali ambayo imepelekea mbunge wa nyamagana kuliomba bunge liahirishe mjadala wa bajeti ya wizara ya maliasili na utalii ili kujadili hoja ya dharura ya mgao uliokithiri wa umeme ulioukumba mkoa wa mwanza pamoja na maeneo ya Arusha, Mbeya, Kigoma na Dar es Salaam.

  Nimeongea na mdau mmoja kutoka mwanza anasema tangu jumapili hawajaona mwanga wa umeme si mchana wala usiku. Watu wenye majenereta wamegeuza adha hiyo kuwa mtaji na baadhi yao hasa kwenye vibanda vya biashara wanachajisha simu kwa shilingi elfu moja (1000).

  Wakati watu wa mwanza wakisota gizani hali ni tofauti katika mkoa wa dodoma ambako hakuna hata chembe ya mgao wa umeme licha ya mkoa huo kutumia umeme wa gridi ya taifa. Hali kama hiyo imeripotiwa pia katika mkoa wa Kagera.
   
Loading...