Mwanza: Wabunge wawili wa CHADEMA wapigwa mapanga na mmoja yupo hoi!

Nilipopigiwa simu alfajiri na Wapo Radio kwa upande mmoja niliwaza ni taarifa za siku ya wajinga lakini kwa upande mwingine nilipokumbuka matukio kama hili ya chaguzi za ndogo niliamini kwamba jambo hili linaweza kuwa la kweli. Niliwapa namba ya Wenje kufanya naye mahojiano toka Mwanza.

Ambacho ninaweza kusema kwa sasa ni hiki: JOHN MNYIKA: CCM inategemea matusi, mafisadi na wamwagaji damu; 'kudumisha amani na utulivu' ni maneno ya kuficha matendo yao maovu

Damu ya binadamu haiwezi kumwagika bure!.
 
Siasa zetu zinaelekea kubaya

Mkuu mimi kila siku huwa napost kuwa CCM wanatakiwa kuwaandaa vijana wao kukubali kushindwa, Slogan ya 'Ushindi kwa vyovyote' is the path to death for the country. Lets pray for the lives of these victims, anything worse will not serve well our country. Hawa vijana wanafanya hivi kwa kuwa vyombo vya dola vimeshindwa kuwa impartial.

Political leaders have to train themselves accepting election loses. Hiyo ndiyo democracy, ukishindwa leo unarudi na kujipanga ili kesho ushinde.
 
kama kuna uwezekano watu wanase mawasiliano ya wabunge wa zamani wa majimbo hayo lazima watakuwa wamewatuma vijana hao hili wakiwaua ufanyike uchaguzi mdogo wapate kurejea bungeni
 
kama kuna uwezekano watu wanase mawasiliano ya wabunge wa zamani wa majimbo hayo lazima watakuwa wamewatuma vijana hao hili wakiwaua ufanyike uchaguzi mdogo wapate kurejea bungeni
Mawazo yako tu but upeo wako wa kufikiri umeishia hapo
 
Hii imekuwa too much tena, inaonekana ccm hawataki kungwatuka na kupicha Chadema kushika Usukani, ccm wanahisi bila vitendo vyaujasusi basi hawana Ubavu kwa Chadema.

Chadema nilazima wawe ngangari ili kuchukuwa uchindi wa 2015na kipimo kizuri ni uchaguzi wa Arusha,
 
Nilipopigiwa simu alfajiri na Wapo Radio kwa upande mmoja niliwaza ni taarifa za siku ya wajinga lakini kwa upande mwingine nilipokumbuka matukio kama hili ya chaguzi za ndogo niliamini kwamba jambo hili linaweza kuwa la kweli. Niliwapa namba ya Wenje kufanya naye mahojiano toka Mwanza.

Ambacho ninaweza kusema kwa sasa ni hiki: JOHN MNYIKA: CCM inategemea matusi, mafisadi na wamwagaji damu; 'kudumisha amani na utulivu' ni maneno ya kuficha matendo yao maovu

Damu ya binadamu haiwezi kumwagika bure!.

Mnyika kuandika humu Jamii forum haitoshi. We need a proper mass media kutangaza huu uovu kwa ulimwengu

Kuna siku dunia itasikiliza na itaitikia wito wa sauti hii ya wanyonge..
 
Wabunge wawili mmoja wa Jimbo la Ilemela na mmoja wa jimbo la Ukerewe wamepigwa mapanga na mawe usiku wa leo kuamkia asubuhi na hii inatokana viongozi hao walikuwa huko Mwanza wakati wakipita nyumba kwa nyumba wakihamasisha watu wakapige kura kumchagua diwani wao huko CCM Kirumba.....
Source.....kipindi cha patapata Wapo Redio
Poleni sana majeruhi na wote mliofikwa na mkasa huo. Tunawaomba polisi waache kuitumikia CCM na iwafikishe wahalafu mbele ya sheria.

Nahisi iko haja ya kubadilisha sheria ya uchaguzi kuhusu muda wa kuanza na kumaliza kampeni za uchaguzi. Kwa utaratibu wa sasa watu wanaweza kukesha wanafanya kampeni mpaka asubuhi ya siku ya kupiga kura. Nashangaa kuwa sheria inasema wazi kuwa saa za mwisho za kufanya kampeni ni saa 12 au 12:30 jioni, lakini bado watu mmoja mmoja wanaruhusiwa/wanaachiwa kuendelea na kampeni usiku kucha. Utaratibu huu kwanza unaruhusu rushwa kutumika, pili uhalifu kama huu, tukitilia maanani kuwa matukio mengi ya uhalifu hutendeka usiku. Kwa faida ya amani na usalama, tuachane na utaratibu huu.
 
Mh Mnyika nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria kuihukumu ama kuishutumu CCM kuwa inahusika na kitendo hicho sio sahihi hata kidogo kwasasa hebu tusubiri vyombo huru vya usalama vifanye uchunguzi wa tukio hilo ili tuweze kutoa matamko yetu. Sisi wanachama wa CCM kama walivyo wanachama wa Chadema tunalaani kitendo hicho cha uhalifu kilichotokea
Nilipopigiwa simu alfajiri na Wapo Radio kwa upande mmoja niliwaza ni taarifa za siku ya wajinga lakini kwa upande mwingine nilipokumbuka matukio kama hili ya chaguzi za ndogo niliamini kwamba jambo hili linaweza kuwa la kweli. Niliwapa namba ya Wenje kufanya naye mahojiano toka Mwanza.

Ambacho ninaweza kusema kwa sasa ni hiki: JOHN MNYIKA: CCM inategemea matusi, mafisadi na wamwagaji damu; 'kudumisha amani na utulivu' ni maneno ya kuficha matendo yao maovu

Damu ya binadamu haiwezi kumwagika bure!.
 
Kama kweli hayo yametokea basi nchi yetu inaelekea pabaya, tunaomba mtuwekee picha kuthibitisha ukweli maana leo ni siku ya wajinga
 
Nilipopigiwa simu alfajiri na Wapo Radio kwa upande mmoja niliwaza ni taarifa za siku ya wajinga lakini kwa upande mwingine nilipokumbuka matukio kama hili ya chaguzi za ndogo niliamini kwamba jambo hili linaweza kuwa la kweli. Niliwapa namba ya Wenje kufanya naye mahojiano toka Mwanza.

Ambacho ninaweza kusema kwa sasa ni hiki: JOHN MNYIKA: CCM inategemea matusi, mafisadi na wamwagaji damu; 'kudumisha amani na utulivu' ni maneno ya kuficha matendo yao maovu

Damu ya binadamu haiwezi kumwagika bure!.

Mnyika unataka kutuaminisha kuwa CCM wote ndiyo wanahusika kuwapiga wabunge wa CDM?
 
Tupo Hospitali ya Bugando hapa. Ndg. Kiwia, mb anatoa maelezo kwa maafisa wa polisi.

Kuna mmoja wa majeruhi ambaye yupo hapa mwanzoni alisema yeye ni mtu wetu na ameumizwa pia. Imegundulika ni mtu wa UVCCM, Ahmed Mkilindi ambaye ndiye alikuwa anaongoza kikosi kilichowavamia kina Kiwia. Amepata jeraha mkononi (friendly fire?). Mwenyekiti wa CCM mkoa yupo hapa kaja kumwona. Nimewaambia Polisi mtu huyu asitolewe hospitali kinyemela bali atoe maelezo polisi kwanza. Huyu ni mtuhumiwa wa kwanza kabisa...

Siasa za Tanzania zinazidi kujidhihirisha kuwa hazina tofauti na nchi nyingine za Kiafrika. Chama cha siasa kuwa na makundi ya wahuni na kupiga watu ni hatari na chama hicho kinakosa 'moral' authority ya kutawala.

Tusubiri uchunguzi zaidi wa Polisi. I am so depressed

Tafadhali wape pole majeruhi. Ujumbe kutoka kwa mimi mtanzania mwenzenu mmoja ni huu. Kwamba kuanzia leo nimefuta dhana kuwa tanzania ni nchi ya amani. na kwa kufuta dhana hii. ndani ya moyo wangu nimekwishaingia katika vita. Na ninawaomba watanzania wote tukubali kuwa Tanzania si nchi ya amani tena kama tulivyoaminishwa miaka ya nyuma. Nimeharibu pesa nyingi sana mwaka juzi na mwaka jana kwa sababu ya upumbavu wa serikali ya CCM wa kuajili vilaza katika sehemu nyeti. Na ndiyo hiyohiyo inalazimisha kubaki madarakani? Shime Watanzania wenzangu. Tunaombea amani, lakini inaelekea Mungu tunayemuomba kaziba masikio. Twendeni vitani!
 
poleni sana kiwia na machemuli>kama waliohusika na uvamizi huu ni wana CCM hatua kali zichukuliwe ili vitendo vya vurugu katika chaguzi za Mwanza visirudiwe tena,ila vilevile wahalifu wanaweza kutumia opportunity ya uchaguzi kuvamia wanasiasa maana wengi wa wapiga kampeni hutembea na kiasi kikubwa cha fedha na vifaa mbalimbali vya thamani.
 
Hiki kitendo ni cha kulaaniwa na watanzania wote bila kujali itikadi zetu za vyama.

Hizo ni dalili kuonyesha kuwa mwisho wa ccm umefika, wao wanatambua mwisho wao na ndo maana wanacheza rough ili kuogopesha wananchi! Pole sana mh. Kiwia
 
Nilipopigiwa simu alfajiri na Wapo Radio kwa upande mmoja niliwaza ni taarifa za siku ya wajinga lakini kwa upande mwingine nilipokumbuka matukio kama hili ya chaguzi za ndogo niliamini kwamba jambo hili linaweza kuwa la kweli. Niliwapa namba ya Wenje kufanya naye mahojiano toka Mwanza.

Ambacho ninaweza kusema kwa sasa ni hiki: JOHN MNYIKA: CCM inategemea matusi, mafisadi na wamwagaji damu; 'kudumisha amani na utulivu' ni maneno ya kuficha matendo yao maovu

Damu ya binadamu haiwezi kumwagika bure!.

Damu ya binadamu wasiofata taratibu na kwenda kupiga kampeni usiku itaendelea kumwagika na ndio itajenga heshima kwa nchi yenye ustawi na kufata sheria bila shuruti.kampeni usiku wa manane nyumba za watu
 
Back
Top Bottom