Anonymous
Senior Member
- Feb 3, 2006
- 125
- 320
Licha ya Tanzania kuongoza Afrika Mashariki kwa wageni wanaotalii mbugani, bado Utalii wa Ndani, umeendelea kuwa chini kulinganisha na Nchi nyingine kama Kenya na hivyo kuendelea kudumaaa kwa Sekta ya Usafirishaji na ya Huduma hasa Mahoteli katika maeneo yaliyo mbali na Kanda Kuu za Kiutalii nchini za Northern Tourism Circuit - Arusha, Moshi, Mto wa Mbu na Karatu, pamoja na Visiwa vya Zanzibar. Tanzania ina utajiri mkubwa wa maliasili na vivutio vingi vya kitalii wa ndani, vinavyoweza kutangazwa kwa njia ya kushindanisha ubora wa Kanda mbalimbali nchini.
Jiji la Mwanza ni epicenter ya Kanda ya Ziwa inayoundwa na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Simiyu na Geita. Lina influence pia kwa Mikoa ya Kigoma na Tabora.
Jiji la Arusha ni epicenter ya Kanda ya Kaskazini inayoundwa na Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga. Lina influence pia kwa Singida (na Dodoma kipindi cha nyuma).
Tafadhari weka bandiko lako lenye picha ama data ili kuweza kujenga vyema hoja iliyopo mezani. Hivyo, utakuwa vyema ikiweka suala lolote, lazima lijibiwe na Kanda nyingine ili kuleta ulinganishi.
Vigezo vya kushindanisha Majiji haya vipo hapo chini.