Jiji la Mwanza vs Jiji la Arusha: Lipi ni zaidi kwenye hili?

Anonymous

Senior Member
Feb 3, 2006
125
320
Licha ya Tanzania kuongoza Afrika Mashariki kwa wageni wanaotalii mbugani, bado Utalii wa Ndani, umeendelea kuwa chini kulinganisha na Nchi nyingine kama Kenya na hivyo kuendelea kudumaaa kwa Sekta ya Usafirishaji na ya Huduma hasa Mahoteli katika maeneo yaliyo mbali na Kanda Kuu za Kiutalii nchini za Northern Tourism Circuit - Arusha, Moshi, Mto wa Mbu na Karatu, pamoja na Visiwa vya Zanzibar. Tanzania ina utajiri mkubwa wa maliasili na vivutio vingi vya kitalii wa ndani, vinavyoweza kutangazwa kwa njia ya kushindanisha ubora wa Kanda mbalimbali nchini.

Jiji la Mwanza ni epicenter ya Kanda ya Ziwa inayoundwa na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera, Simiyu na Geita. Lina influence pia kwa Mikoa ya Kigoma na Tabora.

Jiji la Arusha ni epicenter ya Kanda ya Kaskazini inayoundwa na Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga. Lina influence pia kwa Singida (na Dodoma kipindi cha nyuma).

Tafadhari weka bandiko lako lenye picha ama data ili kuweza kujenga vyema hoja iliyopo mezani. Hivyo, utakuwa vyema ikiweka suala lolote, lazima lijibiwe na Kanda nyingine ili kuleta ulinganishi.

Vigezo vya kushindanisha Majiji haya vipo hapo chini.
IMG_4820.jpg
 
Arusha ilikuwa zamani haina mpinzani mpaka sasa hapa nchini hakuna jiji zuri kama Mwanza.

Bahati nzuri mie si wa Arusha au Mwanza.
A-city nimeenda enda sana na mara ya mwisho ni Feb mwaka huu pia mwanza naifaham sana na jins inavyo change after every two months.

No place like Rocky City in Tanzania.

Mtoa mada kama una cash katumie Mwanza si Arushag

Najua watu wa Arusha watanipinga lakini kama umekuwa mwendaji wa Mwanza hasa toka 2008-sasa. Mwanza is best and still goes on.

Hata kwa usafi ni Mwanza au Moshi.
Naachia keypad za simu.
 
Rock Ciry si ndiyo Biriani Babaa!
Sasa usiniulize nini Makande !
Wenyewe wana midomo hao!
Hazipiti dkk 10 watauzingira Uzi kama mpira wa ko....

ngoja nimalizie hii supu ya mkia....nakurudia.....
 
Nataka nikaanze maisha mapya moja kati ya sehemu hzo mbili.Uzuri niusemao mazingira,kuendelea kiuchumi,afya nk

Karibu Mwanza...Mkuu...Bado kuna opportunity kubwa sana ya kutoka kimaisha...karibu mwanza karibu mwanza kwenye samaki wa maji baridi...

Bado hata viwanja vya kujenga bei rahisi...unaweza kuwa connected kirahisi.....ukiwa creative yaani mwanza utaipenda...karibu mwanza tena na tena...
 
Back
Top Bottom