Mwanza: Vivuko viwili vyasimamishwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Serikali imesitisha utoaji huduma za usafiri kwa vivuko viwili vya MV Athor na MV Orion vinavyofanya kazi kutoka Mwanza mjini kuelekea wilayani Sengerema mkoa Mwanza, baada ya kubainika kuwa na mapungufu, ambapo Waziri amesisitiza kuwa Wakuu wa mikoa na wilaya wasiingilie maamuzi hayo.

MV%20LINK.jpg

MV Orion, moja ya kivuko kati ya viwili vilivyosimamishwa kufanya kazi
Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amesema kuwa zoezi hilo linaanza leo Juni 12, 2021, na kueleza kuwa awali vivuko vilipewa barua na Wakala wa Usafiri wa Majini (TASAC) ya kusitisha huduma za usafiri tangu Mei 25 mwaka huu kufuatia vivuko hivyo kubainika kutokuwa na cheti cha ubora, cheti cha usajili na cheti cha viwango na sifa za mabaharia.
Mbali na vyeti vyombo hivyo pia vilibainika kuwa na utata wa umiliki wa vyombo kwani wamiliki wa sasa walivinunua kutoka kwa mtu mwingine, pamoja na kupelekea kutopandishwa kwenye cherezo kwa muda mrefu kwa ajili ya kuchunguzwa kama vinakidhi haja ya kuendelea kutoa huduma.
 
Hapa kuna la zaidi. Kamanga ferry ishawahi kufungiwa lakini baadae wakakifungua kivuko tena. Sababu ya mwanzo ilikuwa kelele hapo mahakama kuu. But kwa sasa mbadala wa kivuko ni mwaloni kwa mv samali
 
Maendeleo kwa nchi za dunia ya tatu ni dhana ya ndotoni. Kwa fikra hizi zinazoamua kuhusu mstakabari wa maisha ya wananchi kwa namna hii ni hakika pasi na shaka kwamba kuna ki-aina fulani cha laana.

Unafungia vivuko viwili ambavyo vimekuwa ni msaada kwa serikali, wananchi na nchi kwa miongo mingi tu just kirahisi tu hivyo simply una mamlaka ya kufanya hivyo.

Laiti nchi hii tungelikuwa na watoa Huduma ambao ni serious na reliable kama mwenye vyombo hivi japo wawili kila Wilaya ni hakika tungekuwa ni taifa la kutolea mfano kwa ubora na uhakika wa Huduma zetu.

Mungu atusaidie ili tuweze kuzitumia mbongo na akili alizotujalia, tuachane na matumizi ya akili za matope.
"NOT YET UHURU"
 
Tumeona lakini Sababu ya kuvifungia ?

Au baada ya kupoteza ndugu zetu ndio tutaanza kulaumu kwanini vilikuwa havifanyiwi check-up mpaka kuleta majanga kama hayo ?

Nilidhani kwa majanga yaliyoshatukumba tungekuwa tumeshajifunza... Hakuna chenye umuhimu kuliko Uhai wa Mwananchi (Safety First)
 
Sarikali ingesaidiana na mmiliki kufuta suruhu ili watu wahudumiwe. Mbona sababu zenyewe ni za kawaida. We hujaona vyombo vinavyomilikiwa na serikali vinaua. Mv Bukoba!
 
Serikali imesitisha utoaji huduma za usafiri kwa vivuko viwili vya MV Athor na MV Orion vinavyofanya kazi kutoka Mwanza mjini kuelekea wilayani Sengerema mkoa Mwanza, baada ya kubainika kuwa na mapungufu, ambapo Waziri amesisitiza kuwa Wakuu wa mikoa na wilaya wasiingilie maamuzi hayo.

MV%20LINK.jpg

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amesema kuwa zoezi hilo linaanza leo Juni 12, 2021, na kueleza kuwa awali vivuko vilipewa barua na Wakala wa Usafiri wa Majini (TASAC) ya kusitisha huduma za usafiri tangu Mei 25 mwaka huu kufuatia vivuko hivyo kubainika kutokuwa na cheti cha ubora, cheti cha usajili na cheti cha viwango na sifa za mabaharia.
Mbali na vyeti vyombo hivyo pia vilibainika kuwa na utata wa umiliki wa vyombo kwani wamiliki wa sasa walivinunua kutoka kwa mtu mwingine, pamoja na kupelekea kutopandishwa kwenye cherezo kwa muda mrefu kwa ajili ya kuchunguzwa kama vinakidhi haja ya kuendelea kutoa huduma.
Mwenye nchi anakuja mwanza,atatengua hii kauli.
 
Sarikali ingesaidiana na mmiliki kufuta suruhu ili watu wahudumiwe. Mbona sababu zenyewe ni za kawaida. We hujaona vyombo vinavyomilikiwa na serikali vinaua. Mv Bukoba!
Kwahio na vingine viuwe sababu vya Serikali vinaua ?

Ofcourse kwangu mimi mambo ya Transportation ni Service kwa wananchi kwahio Kodi zingetumika kuhakikisha haya mashirika ya usafirishaji (treni, meli na vivuko) vinafanya kazi kwa kutoa huduma ya uhakika na sio kwamba sababu serikali haijawekeza hapo basi iache chochote kipite bila kufuata utaratibu (taratibu nyingine zinaweza kufumbiwa macho ila sio la kuhakikisha ubora wa chombo)
 
Kama vinahatarisha usalama wa raia na mali zao bora visimamishwe kusubiri marekebisho. Kufumbia uozo wa vivuko ni kuweka maisha ya watu rehani.

Ila naibu waziri asitoe tu zile kauli alizowahi kutoa kiongozi mmoja pale Dar ferry kwenda kigamboni. Anayeona nauli ya kivuko ni kubwa apige mbizi.
 
Tumeona lakini Sababu ya kuvifungia ?

Au baada ya kupoteza ndugu zetu ndio tutaanza kulaumu kwanini vilikuwa havifanyiwi check-up mpaka kuleta majanga kama hayo ?

Nilidhani kwa majanga yaliyoshatukumba tungekuwa tumeshajifunza... Hakuna chenye umuhimu kuliko Uhai wa Mwananchi (Safety First)
"awali vivuko vilipewa barua na Wakala wa Usafiri wa Majini (TASAC) ya

1. kusitisha huduma za usafiri tangu Mei 25 mwaka huu kufuatia vivuko hivyo kubainika kutokuwa na cheti cha ubora, cheti cha usajili na cheti cha viwango na sifa za mabaharia.

2.Mbali na vyeti vyombo hivyo pia vilibainika kuwa na utata wa umiliki wa vyombo kwani wamiliki wa sasa walivinunua kutoka kwa mtu mwingine,

3.pamoja na kupelekea kutopandishwa kwenye cherezo kwa muda mrefu kwa ajili ya kuchunguzwa kama vinakidhi haja ya kuendelea kutoa huduma"

Mosi, Hizo ndo sababu za kusimamiahwa kama zilivyotajwa na mamlaka husika, naomba unisaidie kunionesha ubovu wa vyombo uko wapi huenda sijasoma vizuri.

Pili, umejiuliza hivi vyombo huwa vinahudumia watu wangapi, mizigo kiasi gani na magari mangapi kwa siku ili tujiulize mandala wake ni upi?

Kama ni kwa kutegemea chombo kimoja ama vingine vilivyopo siku zote unasemeaje capacity ya vyombo hivyo, je, vina uwezo wa kuhudumia abiria wake wa kila siku pamoja na jao walokuwa wanahudumiwa na vyombo hivi?

Huoni hii ndiyo inaweza kuwahatarisha wananchi zaidi kwa vile watalazimika kujazana kuliko uwezo wa vivuko hivyo husika.

Je? Unajua ni kiasi gani wananchi watahangaika wakati Sisi tupo kwenye viyoyozi na ma V8 mtaani huku tukiwa hatuna mpango nao?

Ndugu, najua unawajali Watanzania, ila jaribu kufungua macho zaidi uone kuna kitu hakipo sawa pahala.
 
Serikali imesitisha utoaji huduma za usafiri kwa vivuko viwili vya MV Athor na MV Orion vinavyofanya kazi kutoka Mwanza mjini kuelekea wilayani Sengerema mkoa Mwanza, baada ya kubainika kuwa na mapungufu, ambapo Waziri amesisitiza kuwa Wakuu wa mikoa na wilaya wasiingilie maamuzi hayo.

MV%20LINK.jpg

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amesema kuwa zoezi hilo linaanza leo Juni 12, 2021, na kueleza kuwa awali vivuko vilipewa barua na Wakala wa Usafiri wa Majini (TASAC) ya kusitisha huduma za usafiri tangu Mei 25 mwaka huu kufuatia vivuko hivyo kubainika kutokuwa na cheti cha ubora, cheti cha usajili na cheti cha viwango na sifa za mabaharia.
Mbali na vyeti vyombo hivyo pia vilibainika kuwa na utata wa umiliki wa vyombo kwani wamiliki wa sasa walivinunua kutoka kwa mtu mwingine, pamoja na kupelekea kutopandishwa kwenye cherezo kwa muda mrefu kwa ajili ya kuchunguzwa kama vinakidhi haja ya kuendelea kutoa huduma.
Sasa hivi vivuko vya Kitano vinatamba tu hapo Kamanga.
 
Hapa kuna la zaidi. Kamanga ferry ishawahi kufungiwa lakini baadae wakakifungua kivuko tena. Sababu ya mwanzo ilikuwa kelele hapo mahakama kuu. But kwa sasa mbadala wa kivuko ni mwaloni kwa mv samali
Pale kuna vivuko vya Kitano wala hakuna shida yoyote
 
Back
Top Bottom