Mwanza: Viongozi wa dini waguswa na mauaji yanayotokea nchini

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,786
4,421
1643627197921.png

Kamati ya viongozi wa dini mkoa wa Mwanza imefanya mkutano wa kukemea hali ya mauaji yanayoendelea hapa nchini ambao wamekutana kwa ajili ya kujadili hali ya mauaji yanayoendelea.

Mbali na kamati ya viongozi wa dini mkoa pia wameshirikishwa viongozi wote wa dini wa mkoa wa Mwanza. Katika mkutano huo viongozi hao wamesema mauaji yanayoendelea yanasababishwa na kukosa maadili, malezi ya wazazi na hofu ya Mungu.

Kutokana na hali hiyo viongozi wa dini kwa nafasi zao wameahidi kuongeza jitihada za kuendelea kufindisha maadili ili Mungu aweze kubadili mioyo ya wanadamu ambao wamegeuka kuwa wanyama.

Aidha wameiomba serikali kutumia sheria kutoa arhanu kwa wanaobainika kufanya vitendo vya mauaji ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Credit: Star TV
 
Back
Top Bottom