Mwanza: Tamasha la siku mbili la utamaduni wa Mtanzania limeanza leo katika viwanja vya msalaba mwekundu

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
320
412
Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) kwa kushirikiana na Kituo cha Makumbusho cha Bujora Mwanza wameandaa tamasha kubwa la utamaduni lenye lengo la kurithisha utamaduni wetu kwa vizazi vyetu vya sasa litakalofanyika katika viwanja vya Redcross Kisesa Jijini Mwanza kuanzia leo Jumanne Septemba 07, 2021 mpaka kesho Septemba 08, 2021.

Mgeni rasmi kwenye tamasha hili ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan. Wote mnakaribishwa.

#Turithishe utamaduni wetu.
#Tudumishe utamaduni wetu.
#Amani na Umoja ni tunu zetu.

====

Tamasha la utamaduni laanza leo Mwanza
1631006558271.png

Mwanza. Tamasha la siku mbili la utamaduni wa mtanzania limeanza leo katika viwanja vya msalaba mwekundu vilivyopo karibu na makumbusho ya Bujora wilayani Magu mkoani Mwanza.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan huku likihudhuriwa na viongozi wa kimila (Machifu) kutoka makabila 120 nchi nzima.

Akizungumza leo, Katibu wa tamasha hilo ambaye ni chifu wa wasukuma wa Mwanza, Aaron Mikomangwa amesema tamasha hilo linalenga kurithisha, kudumisha na kuendeleza mila na desturi za Mtanzania.

"Kuanzia leo watanzania watakaofika katika viwanja hivi watajifunza mila na tamaduni za makabila yao na mengine ikiwemo ngoma, mavazi, chakula na kushuhudia usimikaji wa viongozi mbalimbali wa kimila," amesema Mikomangwa.

Ameongeza kwamba katika tamasha hilo pia kutakuwa na mashindano ikiwemo mashindano ya kurusha mikuki, kusaga na kukoboa nafaka kwa kutumia vifaa vya asilia ikiwemo mawe, na ambapo watashuhudia jinsi ambavyo watu wa zamani walikuwa wakiwasha moto kwa kutumia miti na nyasi (Ulindi na ulimbombo).

Akizungumzia tamasha hilo Chifu kiongozi wa mkoa wa Mbeya Zulu Gama amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ili kujifunza mila na tamaduni za makabila mengine.
 
Matendo yetu ya kila siku ndiyo tunayowarithisha watoto wetu kuliko hayo matukio ya siku moja moja. Tunayowariylthisha wqlatu wetu kwa sasa:

1) udikteta wa viongozi - watoto wetu wanasikia jamii inavyolalamikia kila leo udikteta wa viongozi

2) udhulumati wa jeshi la polisi. Kila siku watoto wetu wanasikia kwa wanaowazunguka juu ya ubaya wa jeshi la polisi tulilo nalo

3) uwongo, uzandiki na hila. Watoto wetu wanasikia na kushuhudia kutoka kwa wanaowazunguka, jinsi viojlngozi walivyo waongo, wanaongea mengine, wanatenda mengine. Wanahuburi haki wanatenda udhalimu.

Huu ndiyo urithi tunaowapa watoto wetu kika siku. Na haya yanaingia kwa watoto wetu zaidi kuliko nyimbo za makabila yetu na hadithi za kusimuliwa kuwa jamii yetu ilikuwa ya upendo mkubwa huku wao wakishuhudia uovu, udhalimu na uonevu wa mamlaka za serikali kwa watu wake.
 
Hakuna cha maana zaidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma, Zoezi kama hili angeeda Afisa Utamaduni wa halmshauri.
Nyie watu mtakufa vinywa wazi, haki ya nani.......si kwa chuki na pinga pinga hizo!

Wakati mwingine jitahidini kukubaliana tu na maisha yalivyo ili mupate amani ya moyo angalau kwa masaa kadhaa kwasababu haijalishi mtu unamchukia kwa kiasi gani ni lazima aendelee kuishi kulingana na business yake. Na business ya kiongozi ni mambo km hayo.
 
Nyie watu mtakufa vinywa wazi, haki ya nani.......si kwa chuki na pinga pinga hizo!

Wakati mwingine jitahidini kukubaliana tu na maisha yalivyo ili mupate amani ya moyo angalau kwa masaa kadhaa kwasababu haijalishi mtu unamchukia kwa kiasi gani ni lazima aendelee kuishi kulingana na business yake. Na business ya kiongozi ni mambo km hayo.
Hujui gharama zinazotumika wewe pokea buku zako 5 za bando, nchi inaliwa haswa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom