Mwanza: TAKUKURU yawanyang'anya majengo manne Watumishi wa TANESA

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,442
3,353
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, imewapokonya waliokuwa watumishi wa shirika lililokuwa linajishughulisha na kupambana, kuzuia, kutibu na kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi nchini (TANESA) majengo manne yenye gharama ya kiasi cha shilingi milioni 420.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga amesema kuwa majengo hayo yalijengwa na Serikali ya Uholanzi katika kiwanja namba 32 kitalu ‘W’ eneo la Kapripoint jijini Mwanza na kuanza mchakato wa kuyakabidhi serikalini.

Stenga amesema mradi huo ulikuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na Uholanzi ambapo baada ya mkataba kuisha mwaka 2012, Serikali ya Uholanzi ilitoa maelekezo ya mgawanyo wa mali zilizokuwa zikitumika katika mradi huo zikiwamo magari na nyumba.

“Serikali ya Uholanzi iliekeza magari yachukuliwe na wafanyakazi lakini majengo manne yalipaswa kukabidhiwa serikali ya Tanzania, sasa baada ya wenye mradi kuondoka baadhi ya wafanyakazi wa Tanesa walifanya mchakato wa kinyemela na kujimilikisha na kuanza kupangisha watu na fedha zote zilikwenda mfukoni mwao," amesema.

Kamanda huyo amesema nyumba hizo zilikuwa zikimilikiwa kinyemela na mapato yake yalikuwa yakiwanufaisha watu wachache, hivyo tayari hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.

Aidha amesema kuwa TAKUKURU wanafuatilia taratibu za kubadilisha umiliki kutoka kwa waliokuwa watumishi wa Tanesa na kuwa mali ya Serikali ya Tanzania, ikiwemo kurudisha fedha walizopata kupitia nyumba hizo.
 
Mayu wane, hili Jimbo chadema waliliharibu Sana kila Kona Kuna wizi
Chatooo
tapatalk_1577999380187.jpeg

dodge
 
Si awamu hii hakuna upigaji hela, Hii ni awamu ipi tena? CCM ( Hama cha majambazi hoyee!!
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, imewapokonya waliokuwa watumishi wa shirika lililokuwa linajishughulisha na kupambana, kuzuia, kutibu na kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi nchini (TANESA) majengo manne yenye gharama ya kiasi cha shilingi milioni 420.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga amesema kuwa majengo hayo yalijengwa na Serikali ya Uholanzi katika kiwanja namba 32 kitalu ‘W’ eneo la Kapripoint jijini Mwanza na kuanza mchakato wa kuyakabidhi serikalini.

Stenga amesema mradi huo ulikuwa ukitekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na Uholanzi ambapo baada ya mkataba kuisha mwaka 2012, Serikali ya Uholanzi ilitoa maelekezo ya mgawanyo wa mali zilizokuwa zikitumika katika mradi huo zikiwamo magari na nyumba.

“Serikali ya Uholanzi iliekeza magari yachukuliwe na wafanyakazi lakini majengo manne yalipaswa kukabidhiwa serikali ya Tanzania, sasa baada ya wenye mradi kuondoka baadhi ya wafanyakazi wa Tanesa walifanya mchakato wa kinyemela na kujimilikisha na kuanza kupangisha watu na fedha zote zilikwenda mfukoni mwao," amesema.

Kamanda huyo amesema nyumba hizo zilikuwa zikimilikiwa kinyemela na mapato yake yalikuwa yakiwanufaisha watu wachache, hivyo tayari hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.

Aidha amesema kuwa TAKUKURU wanafuatilia taratibu za kubadilisha umiliki kutoka kwa waliokuwa watumishi wa Tanesa na kuwa mali ya Serikali ya Tanzania, ikiwemo kurudisha fedha walizopata kupitia nyumba hizo.
Isiishie kwa Wafanyakazi wa Tanesa hata Watumishi wa Ardhi waliofanikisha Mchakato wa kuwamilikisha huku wakijua ni mali ya Serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom