Mwanza Special Thread: Uzi wa kueleza masuala mbalimbali yanayohusu mkoa wa Mwanza

KASULI

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
599
669
Watu wa Mwanza huu uwe Uzi wetu wa kuelezea, Mazuri ya Mwanza, mazuri na mabaya ya hili Jiji, mfano biashara mbalimbali, maulizo na majibu.

Changamoto za mkoa, madalali wa Viwanja, nyumba, vyumba.

Mpigilio wa mji na makazi katika maeneo ya kando kando ya mji.

"Machinga influx" hii kitu imepoteza mandhari ya jiji hili.

Karibuni.
 
Mwanza ni mji mzur sana, Chakula, hali ya hewa na watu wakarim... wanawake wa Mwanza pia ni watu loyal sana.. they dont sell love kama sehem nyingine za nchi hii...
Umaskini upo kila sehem ya nchi hii
Watu wa Mwanza wameibukia na ulevi wa watu wa Dar siku iz..
Mwanza tatizo ni moja tu.. .public places zina vyoo vibaya ukilinganisha na maeneo mengine niliowah kutembelea, ila panabadilika na watu wanajifunza ...

Mwanza ukiwa huna mambo mengi unaish vizur sana
 
Mwanza poa tu ila pembezoni mwa ziwa pachafu sana kuanzia hapo wanaita uswahilini,Kabanga hadi Kirumba fish market...kama kungejengwa vizuri ilikuwa bonge la sehem ya kutulia.

Vipanya vimejaa sana mjini.
 
Hebu endeleeni kutupa dondoo kidogo, hv karibuni nitakuwa huko kwa kazi maalum not less than six month, nimezoea dar sioni kama kuna sehemu nitaweza kuwa comfortable kama dar...nahitaji kuijua mwanza vizuri....sijawahi fika kabisa huo mkoa...hii itakuwa mara yangu ya kwanza
 
Back
Top Bottom