Mwanza, Shinyanga, Maji na Thamani ya Fedha zetu

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
713
1,241
Mradi wa Maji Kahama Shinyanga na Thamani ya Fedha zetu

Ama kwa hakika maji ni hitaji la lazima la binadamu. Na kweli kero ya maji imekuwa ni moja ya kero kuu za wananchi wa Tanzania. Jitihada zozote za utatuzi wa kero hii ni za kupongezwa. Na aghalabu, jitihada kama hizo zikafanyika popote pale, husahaulisha wananchi kujiuliza maswali ya msingi. Leo, niibue mjadala kuhusu sekta ya maji mintaarafu mradi wa maji Kahama Shinyanga. Mjadala huu ni muhimu kwa kuwa sehemu kubwa ya nchi yetu sekta hii imekuwa ikitekelezwa kwa kupitia miradi mbalimbali. Kuna haja ya kutafakari, katika miradi hiyo; je, tunapata thamani halisi ya fedha zetu?(Value for money). Itakumbukwa kwamba hata katika mwaka uliopita wa fedha serikali ilitenga fedha lukuki katika sekta ya maji. Ni vyema tukajadili, zaidi ya fedha kupangwa katika bajeti; je, matumizi yalifanyikaje? Je, kiasi cha maji yanayotiririka kutokana na miradi ya maji sanjari na miundo mbinu iliyowekwa, inawaina na kiasi cha fedha tulichotumia ambacho kwa kiasi kikubwa kinatokana na kodi zetu mimi na wewe?

Tuanze na mradi wa Maji Kahama Shinyanga. Nimechagua mradi huu kwa kuwa mradi huu ulipangwa kutumia takribani bilioni 225(soma zaidi ya milioni laki mbili); kwa kiasi kikubwa fedha hizo zikiwa ni vyanzo vya ndani. Nimechagua mradi huu kwa kuwa pia, kuna malalamiko ya chini chini juu ya matumizi ya mradi huu na hasa mchakato wa utoaji wa zabuni mbalimbali za mradi husika. Ndani ya malalamiko hayo, yanatajwa majina ya watu ambao baadhi yao wako pia kwenye ile orodha ya mafisadi(List of shame) iliyotajwa na Dr Slaa na upinzani kwa ujumla pale Temeke Mwembe Yanga Septemba 15 mwaka 2007.

Kujitokeza kwa majina hayo, katika kushinikiza kutolewa kwa tenda na katika kuchukua tenda zenyewe kunafanya suala hili kuhitaji mjadala; ili hatimaye pumba na mchele ziweze kutenganishwa. Uwepo wa wingu hilo, unataka umma uyazungumze haya masuala ili serikali ijitokeze kuweka wazi taarifa za michakato ya mradi huu na kufafanua bayana kama matumizi yote yalifanyika na yanaendelea kufanyika kwa kuzingatia thamani ya fedha zetu.

Tuujadili Mradi wa Maji Kahama Shinyinga! Lengo kuu la mradi huu lilikuwa ni kusukuma maji kutoka ziwa Victoria kwenda miji ya Kahama na Shinyinga kupitia bomba refu, linalojengwa katika fukwe za ziwa kuelekea kwenye miji husika. Kwa ujumla mradi huu ulitarajia kuwa ufumbuzi wa kudumu wa tatizo kubwa la kihistoria la ukosefu wa maji miongoni mwa wananchi wa eneo hilo ambalo linatazamana kabisa na maji mengi katika ziwa Victoria.

Wazo la kuchukua maji toka Ziwa Victoria na kuyasambaza katika maeneo makavu ya kati ya nchi yetu, si geni sana kwani lilianza toka wakati wa mkoloni. Itakumbukwa kwamba mwaka 1910 Serikali ya Kikoloni ya Mjerumani ilipanga kuyatumia maji ya Ziwa Victoria kwa ajili ya umwagiliaji, usafirishaji na uzalishaji wa umeme katika maeneo ya kati ya mahali ambapo sasa tunapaita Mwanza, Shinyanga, Tabora na Singida. Hata hivyo, baaada ya Waingereza kuwashinda Wajerumani na Tanzania(wakati huo Tanganyika) kuwekwa chini ya mamlaka ya udhamini wao, waliamua kuweka mkazo kwenye matumizi ya maji ya Ziwa Victoria kwa ajili ya umwagiliaji na usafirishaji pekee.

Hatimaye mwaka 1956 Serikali ya Kikoloni ya Mwingereza ilifanya tathmini ya uchukuaji wa maji kutoka Ziwa Victoria katika Ghuba ya Smith kwa ajili ya Umwagiliaji mashambani katika mabonde ya Wambele na Manonga. Kumbukumbu za thamini hiyo zilibaini kwamba ardhi hiyo ilikuwa na tindikali kwa hiyo haikufaa kwa kilimo cha umwagiliaji. Lakini kama mradi huo ungetekelezwa wakati huo basi ungegharimu kiasi cha paundi za uingereza kati ya milioni 20 na 30 tu za wakati huo.

Baada ya uhuru kati ya mwaka 1971 na 1973 Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Uhandisi la(NODECO) toka nchini Uholanzi ilifanya tathmini nyingine ya uchukuaji wa maji toka katika ziwa kutoka katika Ghuba hiyo hiyo ya Smith kuelekea Shinyanga na baaadhi ya Vijiji vya Mwanza kwa ajili ya matumizi ya majumbani. Kazi hiyo ilitarajiwa kwa wakati huo kugharimu shilingi milioni 80 tu na ushee kama ingetekelezwa na ingeweza kutatua tatizo la maji kwa kiasi kikubwa. Kama ilivyo kawaida ya serikali yetu ya tathmini juu ya tathmini; kati ya mwaka 1999 na 2000 Serikali ilifanya tathmini nyingine kwa kushirikiana na NEDECO, Aquanet, DHV na HWG zote za uholanzi na M-Consult ya Tanzania kuhusiana mradi huo huo. Tathmini hiyo ilionyesha kwamba mradi unaweza kufanyika kwa kusukuma maji toka Ziwani mpaka Vilima Vya Ilalambogo na baadaye maji yanaweza kutiririka yenyewe kwa nguvu ya uvutano kwenda Kahama na Shinyanga.

Kutokana na matokeo ya utafiti huo, serikali ilijaribu kuwasiliana na washirika wa kimaendeleo toka Hispania na Uholanzi kwa ajili ya kufanya tathimi ya kina zaidi juu ya utekelezaji. Ndipo ilipothibitishwa kwamba mradi huo unaweza kabisa kutekelezeka. Matokeo ya mwisho yalipendekeza kwamba maji yachukuliwe toka Ziwani kwenye Ghuba ya Smith Sound katika vijiji vya Ihelele katika Wilaya ya Missungwa Mkoani Mwanza. Ndipo Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo(ya wakati huo) ilipoanza kuangalia jinsi ya kutekeleza mradi huo.

Wakati Wizara husika ikiwa inaangalia jinsi ya kutafuta fedha za wahisani kutekeleza mradi huo; Rais wa Jamhuri wa Muungano wa wakati huo, Bwana Benjamini Mkapa akailekeza Wizara kuangalia njia za kupata fedha za kutekeleza mradi huu toka vyanzo vya ndani. Hii ilikuwa ni mwaka 2001 wakati Mkapa alipokuwa akizindua mradi wa Maji pale Chalinze.

Katika mwaka wa fedha 2004/05 Wizara husika ikaomba fedha za mradi huu katika bajeti na kutengewa mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi. Kazi ikaanza mara moja!

Kutokana na mapendekezo ya ripoti husika, maji yakaanza kuwekewa miundo mbinu ya kusukumwa kutoka katika chanzo kwenda kwenye Kilima cha Mabale ambapo Tanki kubwa lingejengwa kabla ya maji kuruhusiwa kutiririka kwa nguvu ya mvutano kwenda Kahama na Shinyanga. Bomba hili lilipangwa kupitia vijiji 54 na kuelekea mpaka tarafa ya Mwamashimba na watu wote katika vijiji hivyo walipaswa kupata maji.

Sasa ni wakati wa kuwauliza watanzania wenzetu wa maeneo ambayo mradi umeshaanza kupita; kama kuna mwekekeo wa kupata thamani ya kodi zao ukilinganisha na fedha ambazo zimekwisha kutumika mpaka sasa.

Hawa ni wakazi wa wilaya za Kwimba, Missungwi, Shinyanga Vijiji na Kahama. Na kwa upekee wananchi wa eneo la mwanzo kabisa wa mradi wale wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kata za Ilujamate, Lubili na Mwawile. Hususani ndugu zangu wa vijiji vya Nyanghomango, Ilalambogo, Isenengeja na Ibinza.

Mradi huu una kandarasi zenye mikataba minne! Yote kwa ujumla wake ikigawanya katika kazi mbalimbali za kusafisha na kujenga katika chanzo cha maji; kuweka miundo mbinu ya msingi; kuweka pampu za maji; kutandaza mabomba; kujenga matanki ya kuhifadhia maji na kuweka kiwanda wa cha kusafisha maji. Na mikataba hii minne imepewa kwa kampuni mbili; kila moja katika umbali Fulani kutoka kwenye chanzo mpaka kuelekea sehemu ya mwisho. Lakini kinachoibua maswali, ni gharama za mradi wenyewe; mathalani mzabuni mmoja alipewa kazi ya kupeleka mabomba toka Dar es salaam kuyapeleka Missungwi, gharama ya kupelekea bomba moja tu- sio kulitandaza, kulibeba na kulipeleka, ilikadiriwa kuwa zaidi ya milioni tatu. Hili ni eneo moja. Hali inayoibua mjadala; zabuni hizi zilipitia mchakato gani? Ukianzia wazabuni wakuu wawili na hata wale wazabuni wa ndani wanaopewa zabuni ndogondogo na wazubuni wakuu! Je, tunapata thamani halisi ya fedha zetu? Zogho, Tujage. Wila!
 
Uchochezi mwingine unaanza taratibu, tena wa kikabila!

PM
 
!

Jamani, ni wakina nani hao? Si watajwe kabisa? unajua wanawake tunapata kero sana ya kutafuta maji umbali mrefu

Asha
 
Wakina nani wametajwa humu ambao wako pia kwenye orodha ya mafisadi? Ushahidi wa kimazingira. Aliyekuwa Waziri wa Maji wakati huo ni Lowassa aliyeko kwenye orodha ya aibu, swahiba wake mkubwa mwenye kupenda Tenda ni yule bwana wa Caspian wenye kumiliki kwa ukaribu pia Vodacom Tanzania. Je, inawezekana Lowassa alimpasia mwenzie tenda kifisadi hapa pia? Kama ni hivyo, basi hawa jamaa walianza kujikusanyia mihela ya kuendeleza mtandao wa kumuingiza Kikwete madarakani siku nyingi sana

Asha
 
Mnyika...Hongera kwa ujasiri wa kuleta hii habari mtandaoni....Maoni yangu ni kuwa hio habari uloweka naona ipo nusu...ni vema ungetupa status ya Mradi kwa sasa umefikia wapi. Hapo umeonesha maeneo mradi ulipotakiwa kupita....

Tukiwa na status ya mradi ulipofikia..either umefeli au umefaulu mradi, basi hapo tunaweza kuja ktk maswali yako ya mwisho juu ya Thamani ya Pesa.

Kuhusu Ugawaji wa Tender, i do believe tender nyingi hapa Nyumbani TZ, zinatolewa kwa upendeleo. hakuna watu wanaoingia ktk tender meeting, bila ya kuwa na clues ya ushakaji wa tender husika nani wampe...unless otherwise kuwa kunna vitu vya kitaalam vingi ambavyo kampuni za kibongo zitashindwa...if that is the case....hujatuwekea mradi mzima umetengenewa kiasi gani, na hoja ya kuhoji kusafirisha Bomba Moja, imecost miliion 3..naiona ina upungufu...alau ungetueleza bomba hilo lina ukubwa kiasi gani...inawezekana ni right figure...3m...Unajua cost ya kukodi Behewa Moja full..kutoka DSM kwenda mwanza kiasi gani?
 
Serikali imepunguza overall budget ya sekta ya maji kwa maelezo kwamba mradi huu umekamilika ambao kimsingi ndio ulichukua sehemu kubwa ya bajeti zilizopita. Hii ni kwa mujibu wa Mkullo

PM
 
Ila Mnyika ni kichwa sana sema ndio hivyo tena ameshakuwa compromised na ujio wa huyu babu wa mkongojo
 
Waziri wa maji wakati ule si ndiye aliyeko Chadema kwa sasa. CDM mkuje huku kumsafisha Mr. Polepole.
 
Ukifukua makabuli ya mda mrefu utakuta fuvu tu.
Tuhangaike na marehemu wa sasa.
 
Wakina nani wametajwa humu ambao wako pia kwenye orodha ya mafisadi? Ushahidi wa kimazingira. Aliyekuwa Waziri wa Maji wakati huo ni Lowassa aliyeko kwenye orodha ya aibu, swahiba wake mkubwa mwenye kupenda Tenda ni yule bwana wa Caspian wenye kumiliki kwa ukaribu pia Vodacom Tanzania. Je, inawezekana Lowassa alimpasia mwenzie tenda kifisadi hapa pia? Kama ni hivyo, basi hawa jamaa walianza kujikusanyia mihela ya kuendeleza mtandao wa kumuingiza Kikwete madarakani siku nyingi sana

Asha
muda
 
Back
Top Bottom