Mwanza: Rais Magufuli aweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja la Kigogo - Busisi

Kwa taarifa yako mara nyingi kampuni hizi hununua nondo toka hafa std ya BS.
Wazalishaji wa Tz wengi hawafikii ubora unaotakikana.
VIWANDA VYA NONDO, KOKOTO, CEMENT WATAPATA HIVYO KUONGEZA MZUNGUKO KWENYE UCHUMI
 
Mkuu una macho yanayoona hatua moja au mbili tu kutoka uliposimama na akiri zako zimetosheka pale ukila na kulala.

Hiyo bilioni 600 inaenda kutengeneza tilioni 2,3 ndani ya mwaka na faida nyingine nyingine sana
'Hiyo bilioni 600 inaenda kutengeneza tilioni 2,3 ndani ya mwaka.'

Uongo mtupu,utaanza story za multiplier effects.
 
Ananiboa kuongea mara kwa mara kisukuma jukwaani tu.
Mkapa na mkwere hawakuwa na Frequency ya namna hii hata wikiwa kwao.
Ana address wananchi wa nchi nzima kiswahili ni muhimu.
Mimi hunifurahisha sana akiongea kilugha, mkuu hata wewe huwezi kufurahisha kila mtu kwa kila jambo hufanyalo
 
Daah hao jamaa Wana ferry ambayo kila saa moja wanaweza vuka just a waiting ya lisaa limoja! Hiyo hela ingetosha kutengeza barabara ya mbeya makongorosi mpaka ipole tabora km 420 pia rungwa km 70 kwenda kufika barabara ya singida highway, kweli kupanga ni kuchagua, imagine bado tuna mikoa mingine haiko connected na lami mpaka leo!
 
Rais Dk. John Magufuli leo Jumamosi Desemba 7, anaweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo - Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 katika Ziwa Vitoria litakalounganisha Mkoa wa Mwanza na Geita.

Hapa kazi tu.

Mwanza. Yawezekana watu wakisikia taarifa za Rais wa Tanzania, John Magufuli kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi unadhani ni daraja la kawaida kama madaraja mengine nchini.

Wanaodhani hivyo wanajidanganya kwa sababu utakapokamilika, daraja hilo linalounganisha Wilaya za Misungwi na Sengerema za Mkoa wa Mwanza nchini Tanzania pamoja na mikoa ya Mwanza na Geita litakuwa ndilo daraja refu kuliko lote katika Ukanda huu Afrika Mashariki na Kati.

Daraja hilo linaunganisha barabara zinazoenda nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Daraja hilo ambalo ujenzi wake utagharimu zaidi ya Sh700 bilioni kwa mujibu wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mwasiliano, Isaac Kamwele, litakuwa na urefu wa kilomita 3.2 likipita juu ya Ziwa Victoria.

Mradi huo pia utahusisha ujenzi wa barabara unganishi wenye urefu wa Kilomita 1.6 na fedha zote za utekelezaji zinatokana na mapato ya ndani.

Alipotangaza uamuzi wa kujenga daraja eneo hilo wakati wa ziara zake kadhaa mkoani Mwanza, Rais Magufuli alisema kukamilika kwa mradi huo siyo tu kutarahisisha usafiri na usafirishaji, bali pia utaondoa adha ya wagonjwa kupoteza maisha wakati wakisubiri vivuko vinavyotoa huduma eneo hilo.

Eneo la Kigongo – Busisi linahudumiwa na vivuko viwili vya Mv Mwanza ambacho ni kipya na Mv Misungwi ambazo hutumia wastani wa dakika 30 hadi 40 kuvuka kutoka upande mmoja hadi mwingine.

“Kila siku watu wamekuwa wakisubiri feri (kwa muda mrefu) haiwezekani kila siku tunategemea feri. Anafika pale mama mjamzito mpaka ukasubiri feri; uchungu utakusubiri wakati mtoto anataka atoke? Pale wameshakufa watu.” amewahi kukaririwa akisema Rais Magufuli

“Tumeomba fedha kutoka kwa wafadhili tumekosa. Tumeamua tunajenga kwa fedha zetu wenyewe,”

Tayari Rais Magufuli na viongozi wengine wa Kitaifa, kidini na wananchi wamewasili eneo la tukio.
Miradi ya kanda ya ziwa. Na bado.
Sehemu nyingine anatupia vimiradi vya billion mbili tatu kuwaziba midomo.
Ten percent yetu kama kawa, kama dawa.
Maendeleo hayana chama wala ukanda. Viva Jiwe!
 
Sisi Watanzania watu wa ajabu sana ,leo palitakiwa JF pafurike shagwe kwa furaha na matarajio makubwa. Mradi huu wa sita kwa urefu wa madaraja Barani Africa. Watu tupo busy na tamko siasa ubaguzi na utani wa mkuu kwa swahiba wake Kitwanga.
 
Mkuu una macho yanayoona hatua moja au mbili tu kutoka uliposimama na akiri zako zimetosheka pale ukila na kulala.

Hiyo bilioni 600 inaenda kutengeneza tilioni 2,3 ndani ya mwaka na faida nyingine nyingine sana
Sio kweli mkuu ndani ya mwaka mmoja trillion 2 had 3,ebu nidokeze kwa njia ipi
 
Hao nao wawe wanalipia kuvuka maana sisi wa kigamboni tuna makosa gani nchi nzima sisi tu ndiyo walipia daraja.
Tena hawa ndio kabisa inafaa walipie, maana ni wanyarwanda, warundi na wakongo ndio watakaofaidika zaidi na daraja hilo!

Hapa nachokoza nyuki, kana kwamba sijui kuwa kuna waTanzania watakaolitumia daraja. Lakini si hata hao wa Kigamboni ni waTanzania?.
Vivuko vitaendelea kufanya kazi, kama huna hela subiri vivuko (navyo vinalipiwa?, sawa, kwa nini daraja lisilipiwe ili pesa irudi na kujenga miradi mingine?)
 
Mkuu,hizo pesa zingejenga kiwanda na wananchi wangepata ajira za kudumu,unlike daraja ambapo ni ajira ya muda mfupi
Hilo daraja likikamilika Miji miidogo Kama Katoro,Buselesele, Usagara, itakuwa kiuchumi.
Vijana watasafiri kati ya geita na Mwanza kwa Dkk 45.
Kwa uchumi wa geita( madini,mananasi,samaki,) viwanda vitajengwa na ajira za kudumu
 
Hii miradi ni mizuri changamoto ni kwamba huwezi kuona impact yake kwenye mzunguko wa Pesa kwa sababu asilimia kubwa ya wakandarasi ni wageni hivyo fedha yote huchukuliwa kwao. Jambo la pili mitambo na material nyingi zinazotumika huingizwa kutoka nje. Kama miradi hii ingekuwa inatekelezwa na wakandarasi wazawa ungekuwa mbali. Hii ndiyo sababu fiscal policy siyo njia nzuri ya kudhibiti mzunguko wa fedha kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania. Watalaam wetu hamumshauri mheshimiwa Rais?
 
Kwa aina hii ya washauri wa uchumi wetu Tanzania ,acha tu uchumi uende zigzaga style
 
Hao nao wawe wanalipia kuvuka maana sisi wa kigamboni tuna makosa gani nchi nzima sisi tu ndiyo walipia daraja.
Yeah ....waweke electronic toll plaza on both sides ya daraja kwa kulipa kidogo...kusaidia quick investment returns....
 
Nakuvisha taji mkuu hebu tembea kifua mbele uko vyema upstairs
Mkuu una macho yanayoona hatua moja au mbili tu kutoka uliposimama na akiri zako zimetosheka pale ukila na kulala.

Hiyo bilioni 600 inaenda kutengeneza tilioni 2,3 ndani ya mwaka na faida nyingine nyingine sana
 
Back
Top Bottom