Mwanza: OCD Bukoba, Babu Sanare afariki kwenye ajali ya gari

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Taarifa ya ajali

SSP Babu Sanare OCD Bukoba amepata ajali mbaya gari yake kupinduka maeneo ya Igaka Sengerema na kupelekea kifo chake.

Bwana ametwaa jina la bwana lihidimiwe.

OCD.jpg
 
Speed ya gari ilikuwa 180 KMS per hr. Na alikuwa hajafunga mkanda . R.I.P

Kwa mtaji huo kifo chake kama vingine kimeangaziwa vyema kwenye uzi huu hapa chini:


Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kwahiyo gar ikikaguliwa haiwez kupata ajali? Au waache kukagua mabus

Umesafiri na mabasi ukaona kuwa hao jamaa bora waachane na hiyo shughuli isiyokuwa na ufanisi wowote?

Ajali ipi imesababishwa na ubovu wa basi? Tuanzie hapo kwanza.
 
Apumzike kwa amani.

Habari hii iwakumbushe wale wakaguzi uchwara wa mabasi stendi. Hawakulikagua gari la huyu bosi wao?

Vipi sababu ya ajali, haikuwa mwendo kasi uliopitiliza?

Hiiiiii bagosha!
Akili nyingine mnaanza kuzitumia mkiwa na miaka 10 na kuendelea?
 
Nimecheka msibani na hilo neno la mwisho..dah.
Ila ww🙌

Ndiyo ulio ukweli mchungu wenyewe.

Songwe na ajali ya watoto wa shule, kule twaambiwa sababu mwendo kasi. Huku panga pangua ngoma itavutiwa kwao.

Hiiiiii bagosha - ni kibwagizo sahihi kuwa sasa nasi tunachoka kutuona sisi ni wajinga wa kudumu.

Hivi hawa jamaa huwa wanatuona je hasa?
 
Askari hawakamatwi hata waki over speed.
Askari hawafungi mikanda.

Magari binafsi ya Askari hayana bima.
Magari binafsi ya Askari hayakaguliwi lkn Yana sticker za kukaguliwa.
Askari wanaendesha mwendo Kasi kupitiliza.

Jirekebisheni
 
Askari hawakamatwi hata waki over speed.
Askari hawafungi mikanda.

Magari binafsi ya Askari hayana bima.
Magari binafsi ya Askari hayakaguliwi lkn Yana sticker za kukaguliwa.
Askari wanaendesha mwendo Kasi kupitiliza.

Jirekebisheni

Hao sheria haziwahusu
Ustaarabu wa kawaida hauwahusu
Kwa nini sheria sote zisituhusu?
Wao ni sikio la kufa
Au rasmi kusikia kwao kenge!
 
Back
Top Bottom