Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,283
- 33,889
Mwanza imerudi tena kwenye kuweka historia ya kubadili hali ya mambo Tanzania. Mwanza ndiko TANU waliiona nguvu ya vyama vya ushirika na kuamua kuviingilia ili kuua nguvu yake kwa wakulima wa Kanda hiyo.
Mwanza ndiko CCM waliona sherehe za "Nane nane" zitekwe nyara na chama hicho ili kibakie salama dhidi ya wakulima wa tanzania. Mwalimu alitembea kwa miguu kutoka kwao Butiama hadi Mwanza kuunga mkono "Azimio la Arusha".
Mwanza ndiko Rais Magufuli alitoa amri ya kutokubughudhiwa kwa wamachinga mpaka Halmashauri ziwe na mipango ya wapi pa kuwapeleka toka kule walikokuwa. Leo tena Rais amesimamisha ubomoaji wa nyumba jijini humo.
Watanzania wajue kwamba Mwanza ni kama mtoto ndani ya tumbo la mama yake kabla ya kuzaliwa. Mtoto huwa tumboni mwa mama yake lakini si sehemu ya mwili wa mama yake na ndiyo maana ikifika miezi 9 ni lazima atoke kwa hiyari ama atatolewa kwa lazima kama atachelewa kutoka.
Watanzania wanapaswa kujua kwamba Mwanza ni sehemu ya Tanzania lakini ni sehemu tofauti na sehemu zingine za Tanzania. Kama watu wa Mtwara wana kero zinazofanana na watu wa Mwanza wanachotakiwa kufanya ni kuwaambia watu wa Mwanza waipiganie ili na wao wa Mtwara wafaidike na kitakachoamuliwa Mwanza!
Mwimbaji Dk. Remmy Ongala alilijua hilo na ukiusikiliza wimbo wake wa "Safari ya Mwanza" utaelewa nguvu ya Mwanza katika Tanzania!