Mwanza ni kiini cha mabadiliko ya kiutawala Tanzania!!

Mwanza imerudi tena kwenye kuweka historia ya kubadili hali ya mambo Tanzania. Mwanza ndiko TANU waliiona nguvu ya vyama vya ushirika na kuamua kuviingilia ili kuua nguvu yake kwa wakulima wa Kanda hiyo.

Mwanza ndiko CCM waliona sherehe za "Nane nane" zitekwe nyara na chama hicho ili kibakie salama dhidi ya wakulima wa tanzania. Mwalimu alitembea kwa miguu kutoka kwao Butiama hadi Mwanza kuunga mkono "Azimio la Arusha".

Mwanza ndiko Rais Magufuli alitoa amri ya kutokubughudhiwa kwa wamachinga mpaka Halmashauri ziwe na mipango ya wapi pa kuwapeleka toka kule walikokuwa. Leo tena Rais amesimamisha ubomoaji wa nyumba jijini humo.

Watanzania wajue kwamba Mwanza ni kama mtoto ndani ya tumbo la mama yake kabla ya kuzaliwa. Mtoto huwa tumboni mwa mama yake lakini si sehemu ya mwili wa mama yake na ndiyo maana ikifika miezi 9 ni lazima atoke kwa hiyari ama atatolewa kwa lazima kama atachelewa kutoka.

Watanzania wanapaswa kujua kwamba Mwanza ni sehemu ya Tanzania lakini ni sehemu tofauti na sehemu zingine za Tanzania. Kama watu wa Mtwara wana kero zinazofanana na watu wa Mwanza wanachotakiwa kufanya ni kuwaambia watu wa Mwanza waipiganie ili na wao wa Mtwara wafaidike na kitakachoamuliwa Mwanza!

Mwimbaji Dk. Remmy Ongala alilijua hilo na ukiusikiliza wimbo wake wa "Safari ya Mwanza" utaelewa nguvu ya Mwanza katika Tanzania!

Hili jambo ni rahisi sana.sina maana ya kuliweka kikabila isipokua huku Mwanza ndipo kiini cha kabila kubwa hapa nchini,kwa sasa kabila hili tunamiliki mikoa mitano ktk kabila moja,kwa sababu ya uwingi huo hakika ukiwakumbuka hata kwa salamu na ukitaka wakupigie kura ya kupata madaraka utayapata maana wakiamua wote kwenda kwenye sanduku la kura kukupa mamlaka itawezekana.

na hii isiwe hasira kwa wengine ni jambo la kawaida na lisilete utengano wa kikanda,kitu ambacho wanasiasa wengine hawajajua ni kwamba USUKUMANI hakunaga mtu mkorofi wala mbaguzi, MSUKUMA yoyote humuona mTanzania mwingine ni ndugu moja,hivyo basi hata ktk siasa ukiweza kuja kanda ya usukuma utakua umetengeneza kura nyingi ktk uchaguzi maana utapewa na Mwanza,Shinyanga,Tabora,Simiyu na Geita.

ikiwa hivyo nani atakushinda ktk uchaguzi?lakini neno langu halijapanga kuleta ubaguzi wa kikabila wala kikanda

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Kama wasukuma wangekuwa wana ukabila usingeona makabila mengine yakishamili kibiashara katika maeneo ya wasukuma.

Leo hii ukienda kwenye mikoa yenye wasukuma wengi utakuta wafanyabiashara wa kichaga wamejaa na biashara zao zinapata mafanikio makubwa kwa sababu wanunuzi ni wasukuma.

Wakina dada wengi wa makabila mengine wameolewa na wasukuma.

Kwa ujumla, wewe unaodhani wasukuma wana ukabila inawezekana ukawa ni mkabila namba moja.

Huwezi kujua kama fulanio ni chawi kama huna elimu ya kichawi!

Acheni kuwalazimisha wasukuma wawe wakabila na siku wakiwa wakabila itakuwa ni jadi kwa serikali kuongozwa na watu kutoka katika kabila la wasukuma. Kwenye siasa, namba zinahesabika!
Kwa mfumo huu nchi itachafuka maana tuna Raisi anaeukumbatia ukabila
 
Hili jambo ni rahisi sana.sina maana ya kuliweka kikabila isipokua huku Mwanza ndipo kiini cha kabila kubwa hapa nchini,kwa sasa kabila hili tunamiliki mikoa mitano ktk kabila moja,kwa sababu ya uwingi huo hakika ukiwakumbuka hata kwa salamu na ukitaka wakupigie kura ya kupata madaraka utayapata maana wakiamua wote kwenda kwenye sanduku la kura kukupa mamlaka itawezekana.na hii isiwe hasira kwa wengine ni jambo la kawaida na lisilete utengano wa kikanda,kitu ambacho wanasiasa wengine hawajajua ni kwamba USUKUMANI hakunaga mtu mkorofi wala mbaguzi,MSUKUMA yoyote humuona mTanzania mwingine ni ndugu moja,hivyo basi hata ktk siasa ukiweza kuja kanda ya usukuma utakua umetengeneza kura nyingi ktk uchaguzi maana utapewa na Mwanza,Shinyanga,Tabora,Simiyu na Geita.ikiwa hivyo nani atakushinda ktk uchaguzi?lakini neno langu halijapanga kuleta ubaguzi wa kikabila wala kikanda

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
Binafsi mkuu hujui usemacho kama wewe ni msukuma huwezi ona huo ukabila naanza na facts hizi hapa kukudhihirishia wasukuma ni wakabila na wabinafsi nimesoma nao a level walikuwa wanakaa vikundi vikundi wao tu kama camps zao hawajichanganyi na watu wengine yani msukuma rafiki zake watakuwa ni wasukuma

Je unajua kigezo cha mabula kushinda ubunge kwasababu ni msukuma na opponent wake alikuwa mjaluo hicho kilikuwa kigezo cha kupigiwa kura na wasukuma maana hata kwenye kampeni alikuwa anajinasibu kwa kiluga
 
Wanasiasa wanaangalia nguvu ya wapiga kura iko wapi? Jiulize Mwanza walipoamua kwenda upinzani 2010 kanda ya ziwa kilitokea nini? Karibu mikoa yote ya kanda ya ziwa walifanya mabadiliko, Mwanza walipofuta upinzani 2015 mikoa mingine ya kanda ya ziwa kilitokea nn? kwa ufupi kanda ya ziwa ina nguvu sana ya kuamua nani awe rais wa JMT , politicians knows that na wanatumia mbinu zote kupata kuungwa mkono.
sikuelewi una maanisha nini, Katika nchi hii haijawahi kutokea UPINZANIA KUWA NA VITI VINGI VYA UBUNGE NA MADIWANI KAMA ILIVYO SASA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015 AMBAPO HIYO MWANZA YAKO ILIPIGA KURA ZA KIKABILA KUMCHAGUA MAGUFULI KAMA ALIVYOBAINISHA JANA
 
Ukiona mtu anang'ang'ania kwa ukabila ujue huyo mtu hana hoja ya kuinfluence watu, halafu watu wanasema jamaa sio msukuma ni mzinza sema anajua tu kisukuma hao wazinza sijui wanatokea sehemu gani hapa Tanzania
wanapatikana kwa wingi wilaya ya sengerema na hata geita
 
Binafsi mkuu hujui usemacho kama wewe ni msukuma huwezi ona huo ukabila naanza na facts hizi hapa kukudhihirishia wasukuma ni wakabila na wabinafsi nimesoma nao a level walikuwa wanakaa vikundi vikundi wao tu kama camps zao hawajichanganyi na watu wengine yani msukuma rafiki zake watakuwa ni wasukuma

Je unajua kigezo cha mabula kushinda ubunge kwasababu ni msukuma na opponent wake alikuwa mjaluo hicho kilikuwa kigezo cha kupigiwa kura na wasukuma maana hata kwenye kampeni alikuwa anajinasibu kwa kiluga
mie shule nlosoma a level kabila lililokua na ubaguzi walikua ni wahaya asee hawa jamaa walikua kivyao vyao na walitusaliti sana kila tulipopanga kufanya mgomo ili kishinikiza jambo fulani liwekwe sawa.
 
Binafsi mkuu hujui usemacho kama wewe ni msukuma huwezi ona huo ukabila naanza na facts hizi hapa kukudhihirishia wasukuma ni wakabila na wabinafsi nimesoma nao a level walikuwa wanakaa vikundi vikundi wao tu kama camps zao hawajichanganyi na watu wengine yani msukuma rafiki zake watakuwa ni wasukuma

Je unajua kigezo cha mabula kushinda ubunge kwasababu ni msukuma na opponent wake alikuwa mjaluo hicho kilikuwa kigezo cha kupigiwa kura na wasukuma maana hata kwenye kampeni alikuwa anajinasibu kwa kiluga

Akili yako siwez kuifanya ielewe chenye nimesema.ukimsema Mabula hukumbuki chama alichokua anapambana nacho kimejaa ukanda ndo sababu kubwa na si ubaguzi wa msukuma,

?yamkini umekutana na udhaifu wa mtu mmoja mmoja uliyo kwa watu.uliza vzr wasukuma wakoje toka enzi na enzi.ukiwa hupendi au unajisikia vibaya basi we pita hivi
 
Kama wasukuma wangekuwa wana ukabila usingeona makabila mengine yakishamili kibiashara katika maeneo ya wasukuma.

Leo hii ukienda kwenye mikoa yenye wasukuma wengi utakuta wafanyabiashara wa kichaga wamejaa na biashara zao zinapata mafanikio makubwa kwa sababu wanunuzi ni wasukuma.

Wakina dada wengi wa makabila mengine wameolewa na wasukuma.

Kwa ujumla, wewe unaodhani wasukuma wana ukabila inawezekana ukawa ni mkabila namba moja.

Huwezi kujua kama fulanio ni chawi kama huna elimu ya kichawi!

Acheni kuwalazimisha wasukuma wawe wakabila na siku wakiwa wakabila itakuwa ni jadi kwa serikali kuongozwa na watu kutoka katika kabila la wasukuma. Kwenye siasa, namba zinahesabika!
Hawa wakijua wewe ni msukuma mwenzao basi wataanza kuongea kisukuma hata kama walikua wanaongea kiswahili...
 
Hapana mikoani kote ukabila mtupu except mikoa ya mwambao wa bahari
Hupo sahihi. Unaikumbuka kauli ya Mwalimu? Mwalimu aliwahi kusema, 'ukimpa Mhaya uwaziri umewapa wahaya, ukimpa uwaziri mtu wa Iringa, umempa yeye'.

Kuna makabila ambayo yameegemea sana kwenye fikra za kikabila, yapo na yanafahamika. Hatuwezi kuwalaumu sana maana ni mambo yaliyojengeka kwenye jamii zao kwa miaka mingi. LAKINI KINACHOSHANGAZA NA KUTIA HOFU NI PALE MNAPOKUWA NA KIONGOZI ANAYEEGEMEA KWENYE UKABILA. Watanzania hili tulipinge kwa nguvu zetu zote. Huyu anatuingiza motoni.

Tulitarajia kiongozi wakati wote apalilie umoja na awe mstari wa mbele kuudhoofisha ukabila. Kiongozi anayeupa nguvu ukabila, siyo kiongozi bali ni shetani aliyejivika ubinadamu. Ukabila ni daraja la kuvukia kuelekea umautini. Mauti ya kutufikisha jehanamu.
 
Mkuu mm naona shida ni kuona watu wengi hawamkubali kaona pa kujikingia ni kabila lake ambapo kaona wapo wengi hivi wale walio bomolewa kimara anajua maumivu wanayo yapata wakisika ile kauli ya jana
 
Usukumani, ukabila uliopo ni katika kuongea Kisukuma lakini siyo ukabila wa kuwatenga watu, kuwaonea au kuwabagua.

Hata usipokuwa msukuma, ukifika vijijini kabisa, kama unakijua kisukuma, utaongea na kila mtu kama vile mlifahamiana toka utotoni. Utakaribishwa kila mahali, siyo kwa unafiki bali kutoka moyoni kabisa. Hata kama hujui kisukuma, ukiwapata wale wanaojua kiswahili, hata kama siyo kwa ufasaha, utadhihirisha ukarimu wao.

Mnachotakiwa kujua, Mwalimu kuna wakati alisema, viongozi madikteta hutafuta kwa nguvu kushikamana na makundi fulani iIi wale watu wahisi anawapenda, na wamtetee kunapokuwa na kelele dhidi yake. Atajishikamanisha na kabila fulani (mara nyingi kabila lenye watu wengi), Atajishikamanisha na dini fulani (mara nyingi dini yenye waaumini wengi), anaweza kujishikamanisha na kanda fulani (mara nyingi kanda yenye watu wengi).

Huu ni mtihani kwa wasukuma, ni mtihani kwa wakatoliki na ni mtihani kwa kanda ya ziwa.
 
Back
Top Bottom