Mwanza: Mwalimu adaiwa kuwa na mahusiano na Wanafunzi 3 huku akilala na wawili kwa wakati mmoja kitandani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,858
2,000
Mkuu wa wilaya ya Magu mkoani Mwanza, Salum Kalii, ameagiza Mwalimu Martin Mambosasa, wa shule ya msingi Ilungu anayetuhumiwa kuwadhalilisha kingono na kuwafanyia michezo michafu wanafunzi hata wawili kwenye kitanda kimoja kwa muda wa miaka saba kuondolewa wilayani humo.

Agizo hilo amelitoa kwenye kongamano la kuweka mikakati ya kukabiliana na ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mimba na ndoa za umri mdogo, utoro kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu na ndipo alipotoa maelekezo hayo.

"Kesi ambazo tulizibaini ikiwepo Mwalimu mmoja anayeitwa Mambosasa tulimkamata akiwa na mahusiano na wanafunzi zaidi ya watatu, na wakati mwingine alikuwa anawalaza kwenye kitanda kimoja wote wawili na kuwafanyia mambo ya ajabu sana, nimesema mimi simtaki kwenye wilaya yangu" amesema DC Kalii.


Muungwana
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,692
2,000
Agizo hilo amelitoa kwenye kongamano la kuweka mikakati ya kukabiliana na ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, mimba na ndoa za umri mdogo, utoro kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu na ndipo alipotoa maelekezo hayo.
Kwahiyo bila kongamano kuwepo asingeshughulikia jambo hilo?
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,692
2,000
"Kesi ambazo tulizibaini ikiwepo Mwalimu mmoja anayeitwa Mambosasa tulimkamata akiwa na mahusiano na wanafunzi zaidi ya watatu, na wakati mwingine alikuwa anawalaza kwenye kitanda kimoja wote wawili na kuwafanyia mambo ya ajabu sana, nimesema mimi simtaki kwenye wilaya yangu"
Huyu DC anashida kichwani si bure, kumbe alimkamata akiwa na hao wanafunzi, bado hakumpeleka kwenye vyombo husika, Samia una DC kweli hapo?
 

The Sun-of-a Beach

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,139
2,000
Hivi hili jambo lilikuwa halijachukuliwa hatua tu?maana limejulikana humu JF tangu mwaka jana.

Halafu mtu aliyepaswa awe jela muda huu anaambiwa tu "sikutaki kwenye wilaya yangu"? Hii nchi haijawahi kuwa na usawa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom