MWANZA: Mtuhumiwa wa Mauaji ya Msikitini awatoroka Polisi


chakii

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Messages
17,013
Likes
14,864
Points
280
chakii

chakii

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2013
17,013 14,864 280
Taarifa ya jeshi la Polisi mkoani mwanza inaeleza kuwa mnamo tarehe 03.07.2016 majira ya 08:00 usiku katika maeneo ya mlima wa Kiloleli Nyasaka wilaya ya Ilemela mkoa wa mwanza, mtuhumiwa wa ujambazi katika maduka ya kutuma pesa kwa njia ya simu, pamoja na mauaji ya msikitini aliyejulikana kwa jina Hamisi Juma miaka [38] makazi wa Nyegezi aliyekuwa anashikiliwa na askari, alitoroka ulinzi wa askari, wakati akiwapeleka askari wa upelelezi kuwaonyesha eneo lingine wanapojificha majambazi wenzake.

Aidha baada ya askari kufika kwenye eneo la tukio ghafla majambazi waliokuwa wamejificha katika mlima tajwa hapo juu walianza kurusha risasi kwa askari ndipo askari walipo taharuki na kuanza kujibu mashambulizi ya risasi kwa majambazi hao.

Pindi majibizano ya risasi yakiendelea kati ya watuhumiwa wa ujambazi ambao walikuwa wamejificha kwenye mlima, hali hiyo ilipelekea mtuhumiwa bwana Hamisi Juma aliyekuwa chini ya ulinzi wa askari polisi kupata mwanya na kuwatoroka askari na kutokomea kusiko julikana.

Aidha a katika mapigano hayo askari walifanikiwa kukamata bunduki aina ya short gun ilyokatwa mtutu na kitako iliyokuwa na risasi moja chemba iliyotupwa na majambazi hao.

Hata hivyo taarifa hiyo imesema kuwa juhudi za kutafuta mtuhumiwa huyo zinaendelea na kuhakikisha anatiwa nguvuni na jeshi la polisi.

Katika tukio lingine la tarehe tajwa hapo juu majira ya saa 08:45 usiku katika eneo laKiloleli kata ya Nyasaka wilaya ya Ilemela mkoa wa mwanza, mtuhumiwa wa ujambazi katika maduka ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu, pamoja na mauaji ya msikiti wa Rahmani uliopo kata ya Mkolani aitwaye Mohamedi Bishof miaka [31] shombe wa kiarabu mkazi wa Nyasaka aliruka kutoka ndani ya gari la polisi kwa nia ya kutaka kutoroka, lakini hata hivyo alianguka barabarani na kuumiakichwani na sehemu mbalimbali za mwili wake.Aidha mtuhumiwa huyo wa ujambazi alifariki dunia njiani wakati akipelekwa hospitali kupatiwa matibabu.

Taarifa ya jeshi hilo inasema kuwa wakati wa uhai wake marehemu alikiri kuwa ni kweli alihusika katika matukio ya mauaji naunyang’anyi wa kutumia silaha katika vibanda vya m-pesa, tigo pesa na airtel money.

Pindi marehemu anakamatwa alikutwa akiwa na electronic devices aliyokuwa akitumia kufanyia matukio ya uhalifu jijini Mwanza na nje ya Mwanza pamoja na kompyuta mpakato moja aina ya dell ambayo walikuwa wamepora katika tukio moja la unyang’anyi wa kutumia silaha katika tukio la tarehe 05.05.2016 katika eneo la Kishiri Center ambapo mwenye duka aliyejulikana kwa jina la Phares Gabriel alijeruhiwa na risasi kwenye mguu wa kulia na mkono wa kulia na kupora fedha ambazo hazijafahamika zilikuwa ni kiasi gani.

Majeruhi aliyepigwa risasi katika tukio hilo alipelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando kupatiwa matibabu lakini baadaye alifariki dunia kutokana na majeraha ya risasi alizopigwa.Mwili wa marehemu mtuhumiwa upo hospitali ya rufaa ya Bugando kwa uchunguzi na utambuzi.

Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza bado lipo katika jitihada kali za kuhakikisha watuhumiwa wote wanaodaiwa kuhusika katika uhalifu wanakamatwa na kufikishwakatika vyombo vya sheria.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi anawataka wananchi wa jijina mkoa wa Mwanza kutulia huku wakiendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi, ili kuweza kufanya kazi vizuri na kufanikiwa kuwakamata wahalifu na silaha wanazotumia mapema na haraka iwezekanavyo.


Chanzo: EATV
 
M

mliberali

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2012
Messages
4,406
Likes
3,138
Points
280
Age
46
M

mliberali

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2012
4,406 3,138 280
kwa taarifa hii hakuna kitu hapo hao majambazi inaonekana kama vile no washirika wa mapolisi, au inaonekana kama vile polisi waliwatumia kwenye mission zao sasa hawawahitaji tena wameamua kuwapotezea, kuwazinga wananchi
 
chakii

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Messages
17,013
Likes
14,864
Points
280
chakii

chakii

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2013
17,013 14,864 280
kwa taarifa hii hakuna kitu hapo hao majambazi inaonekana kama vile no washirika wa mapolisi, au inaonekana kama vile polisi waliwatumia kwenye mission zao sasa hawawahitaji tena wameamua kuwapotezea, kuwazinga wananchi
Hawa askari bure kabisa mkuu, wanapokea mshahara wa bure asee
 
Mapensho star

Mapensho star

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Messages
1,700
Likes
1,318
Points
280
Age
25
Mapensho star

Mapensho star

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2016
1,700 1,318 280
kuna mchezo hapa inakuw vp mtuhumiwa anakimbia na pingu af askari wetu walivyowashenz wanapenda sana kukamata bunduki baada ya muhusika
 
mzushi

mzushi

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
2,628
Likes
2,535
Points
280
mzushi

mzushi

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2012
2,628 2,535 280
hakuna aliyetoroka hapo huyo tayari ameshanyang´anywa roho yake haraka haraka hatutamsikia tena
 
uporo wa wali ndondo

uporo wa wali ndondo

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Messages
2,490
Likes
1,370
Points
280
uporo wa wali ndondo

uporo wa wali ndondo

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2013
2,490 1,370 280
Kwanini picha zake zisisambazwe kila mtaa kama walivyokuwa wakina T bag na michael scorfild (yule shoga) wa PB.
 
mzushi

mzushi

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Messages
2,628
Likes
2,535
Points
280
mzushi

mzushi

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2012
2,628 2,535 280
kuna mchezo hapa inakuw vp mtuhumiwa anakimbia na pingu af askari wetu walivyowashenz wanapenda sana kukamata bunduki baada ya muhusika
mkuu hivi wewe unamjua Msangi au unamsikia ,huyo marehemu itabaki story tu
 
M

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Messages
8,138
Likes
5,185
Points
280
M

Molembe

JF-Expert Member
Joined Dec 25, 2012
8,138 5,185 280
Ukiwajua polisi wa nchi hii hawakupi shida.
 
Majestic wolf

Majestic wolf

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2015
Messages
1,204
Likes
1,657
Points
280
Majestic wolf

Majestic wolf

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2015
1,204 1,657 280
Wangepiga risasi tu mama kijo aje kutetea
 
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
18,488
Likes
24,782
Points
280
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2012
18,488 24,782 280
Ukiwajua polisi wa nchi hii hawakupi shida.
Eti jambazi aliwatoroka police wakati walipo shambuliwa na majambazi kutokea juu ya mlima, na kisha police hao wakaanza kujibizana kwa risasi na majambazi wale. Eti hapo ilikua saa 8 usiku..
Katika hali ya kawaida, ni binadam gani mwenye uwezo wa kulenga shabaha gizani..!?
Je ilikuaje jambazi afanikiwe kutoroka huku akiwa na pingu na wakati huo taarifa inajieleza kwamba jambazi huyo alikua amekwenda kuwaonyesha police mlima wanapo jificha majambazi wengine?
Je jambazi huyo hakua na pingu?
Kwanini police walienda na jambazi hadi eneo la himaya ya majambazi?
Kwanini waliamua kutomuacha jambazi alie toroka kwenye gari la police na kisha kutoroka wakati alie baki kwenye gari la police eti alikufa baada ya kuvuja damu nyingi alipo anguka akiwa anajaribu kutoroka?
Agghhhh.....
This is crazy aiseeee...
Hizi intelijesia naona hazina weledi kabisa aiseee...... maana huu ni uongo ulio kosa weledi proper
Tumeshachoka kusikia habari za kizembe kama hizi Jambazi anawatoroka polisi chini ulinzi mkali?
 
Prince Kunta

Prince Kunta

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2014
Messages
11,533
Likes
9,903
Points
280
Prince Kunta

Prince Kunta

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2014
11,533 9,903 280
Watuhumiwa wa kisiasa wakikamatwa huo ulinzi wake sasa utasema ni gaidi ila ulinzi wa jambazi wala
 

Forum statistics

Threads 1,237,306
Members 475,501
Posts 29,283,973