Mwanza: Mtoto ateketea kwa moto wakati wa operesheni ya Kiserikali

Hii habari hata haieleweki, mara kaliua mara mwanza, brother umekunywa pombe "gambe"
"Gambe" labda umekunywa wewe.

1. Habari inasikitisha sana.
2. Huwa mnalipwa kiasi gani kurukia treni kwa mbele?

IMG_20210619_153019_243.jpg
 
Narukia treni?

Wewe ndio umekurupuka, umepata taarifa ya kitu kaa chini uandike vizuri sio kukimbilia huku kupost, uonekane we ndio wa kwanza kupata taarifa?.

Unaendelea kukurupuka jombi. Originally kichwa kilikuwa hivi:

"Mtoto aungua Moto hadi kufa katika operesheni ya Dola."

Baada ya maelezo ya awali kwenye mada, link hii kama ilivyo hapa chini, niliiambatanisha:


Moderator wamekuja wakakarabati kwa makosa kichwa. Pia wakatoa link na kuya paste maelezo kutoka kwenye link ambayo yana pia huo ukakasi wa "Mwanza."

Kistaarabu - habari inasikitisha na hilo nimelisema. Makosa ya Moderator yanihusu miye vipi?

Bado tu huoni kukurupuka kwako?
 
Haya poa braza K
Unaendelea kukurupuka jombi. Originally kichwa kilikuwa hivi:

"Mtoto aungua Moto hadi kufa katika operesheni ya Dola."

Baada ya maelezo ya juu link hii kama ilivyo hapa niliambatanisha:


Moderator wamekuja wakakarabati kwa makosa kichwa. Pia wakatoa link na kuya paste maelezo ambayo yana pia huo ukakasi wa Mwanza.

Kistaarabu - habari inasikitisha na hilo nimelisema. Makosa ya Moderator yanihusu miye vipi?

Bado tu huoni kukurupuka kwako?
 
Haya poa braza K

Nilitaka nikupe ki emoji cha kucheka. Ila kama nilivyosema habari hii inasikitisha sana.

Nimeziona picha za tukio hili. Katika about 20 sikuweza kuangalia zaidi ya 2.

Nilipo siku yote imeharibika. Bila shaka itanichukua siku kadhaa kulitoa tukio baya hili mawazoni.
 
Habari hii ni kutoka Kaliua, Tabora ambako wale jamaa wasiokuwa na chembe ya utu walikuwa wametia timu kwenda kufanya yao.

Unachoma vipi nyumba ambayo wanaweza kuwemo ndani watoto wadogo, wazee au wasiojiweza?

Piga picha kumwona mtoto wa miaka 4 yuko je.

Eeh mola wetu umrehemu malaika wako huyu aliyetangulizwa kifedhuli kwako. Ukawakirimu majahili hawa ujira sawa sawa na matendo yao:

(Picha za tukio hili haziwekeki hapa katika hali yoyote).

=====

Mwanza. Mtoto Nyanzore Ng'wandu (4) amefariki dunia kwa kuteketea kwa moto wakati wa operesheni ya kuwaondoa wananchi waliovamia eneo tengefu ndani ya Hifadhi ya jamii Isawimo inayoundwa na vijiji 11 vya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana Ijumaa Juni 18, 2021 mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Abel Busalama amethibitisha kifo cha mtoto huyo kilichotokea wakati wa operesheni iliyofanyika Juni 16, 2021.

Mtoto aliyetekea kwa moto ni mjukuu wa mzee Ng'ombeikungire Ng'wandu, mkazi wa kijiji cha Kombe wilayani Kaliua.

"Serikali imesikitishwa na kifo cha mtoto huyo na vyombo vya dola vimeanza uchunguzi wa kuhusu tukio hilo. Mimi binafsi nimefika eneo hilo nikiongozana na kamati ya usalama ya wilaya."

"Kuna maswali na hoja nyingi kuhusu kifo cha mtoto yule, kwanza wana familia wanasema aliteketea baada ya kuanguka mlangoni katika jitihada za kujiokoa. Lakini eneo mwili upokutwa ni karibia hatua mbili kutoka mlangoni," amesema.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, kuna hisia kuwa kifo cha mtoto huyo ni tukio la kutengenezwa kwa nia ya kukwamisha operesheni ya kuwaondoa waliovamia eneo la hifadhi na kuendesha shughuli za kibinadamu ikiwemo makazi, kilimo, uvuvi na ufugaji.

"Siwezi kusema kwa uhakika ni nani ametengeneza tukio hilo lakini mazingira yanatia shaka na ndio maana vyombo vinafanya uchunguzi wa kina," amesema mkuu huyo wa wilaya

Akizungumzia tukio hilo, diwani wa Usinge, Titus Kavura amelaani kitendo cha askari Mamlaka ya Wanyamapori na Jeshi la Polisi walioshiriki operesheni hiyo kutumia nguvu na mabavu badala ya busara kiasi cha kuteketeza nyumba bila kutoa fursa kwa wananchi kujiokoa na kuokoa mali.

"Walichokuwa wanafanya askari wale ni kufika na kutia moto nyumba bila kujali ndani kuna watu wala mgonjwa, hii ndio maana wazazi walitimua mbio kujiokoa na kumsahau mtoto aliyekuwa amelala ndani," amesema diwani Kavura.

Mwanachi
Mtu mwenye akili timamu anaweza akafanya haya waliofanya hao mashetani?, mimi ningekuwa Rais, ningewalisha kitanzi hao mbwa wote endapo watathibitika pasi na shaka kufanya uzembe uliosababisha kifo cha mateso makali kiasi hicho kwa malaika mdogo kiasi hicho, lazima tuwe na utu at some point!!
 
Yaani wazazi waache mtoto aungue moto Ili kukwamisha operation??

Kuna wakati msukuma akianza kutuponda wenye vielimu vyetu hua namuelewa ni mambo kama haya yanafanya elimu ionekane sio kitu.
 
Sio tu kuchunguzwa... Afukuzwe kazi kwa kosa la uharibifu wa mali na kusababisha kifo Cha mtoto...

Utetezi wake una ukakasi mkubwa huyo hafai kuwa kiongoz...
Anyongwe mbwa huyo, ikithibitika kahusika na uzembe uliosababisha kifo cha mateso makali namna hiyo, tena kwa malaika wa miaka minne??!!😭😭😭😭😭
 
Back
Top Bottom