Mwanza: Moto wateketeza vibanda vya biashara zaidi ya 30

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1581498205846.png

Vibanda zaidi ya 30 vya wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga wapatao 200 vimeteketekea kwa moto ulioanza majira ya saa 10 usiku katika eneo la Makoroboi jirani na msikiti wa Wahindi jijini Mwanza.

Vyanzo vya habari vinaeleza kwamba moto huo umesababishwa na hitilafu ya umeme na uunganishaji holela wa nyaya za umeme,mali mbalimbali za machinga hao zimeteketea kabisa na hakuna mtu yeyote aliyepata madhara kutokana na moto huo.

1581498129230.png

Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Nyamagana Daktari Philis Nyimbi amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa zoezi la kubainisha vibanda vingine vilivyoteketea linaendelea.

Chanzo: ITV
 
Pole yao. huwa nakumbukaga miaka ile soko la mwanjelwa mbeyaaaa..... angalau miaka hii washamudu dhibiti mioto
 
Palipo ungua ni lile eneo lilipokana na matemple ya wahindi...Zile kuta zilikuwa zinapendeza ila kwa sasa zimekuwa na masizi... Vitu vilivyokuwa like eneo vimeteketea totally... Japo eneo kubwa la makoroboi bado linapiga kazi.
 
Yap!!!hilo eneo wahindi wamepambana kiwaondoa hao machinga na mafundi mchundo toka kitambo,nakumbuka wale mafundi mchundo waliwahi kulalamikia halmashauri iliyotaka kuwaondoa eneo hilo baada ya wahindi kutoa rushwa nene kwa viongozi wa halmashauri,hata hivyo zoezi hilo la kuwaondoa lilikwama,so yaweza kuwa hii ni plan B
Wale Wahindi wanapambana sana Machinga Watoke hilo Eneo.. Zinaweza kua Njama pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom