Mwanza - Meya na Naibu wake wachaguliwa toka CHADEMA

Mshindi Meya wa Mwanza ni Julius Manyerere (Chadema) amepata kura 17 Wakati wa CCM amepata Kura 15 Naibu Meya wa Mwanza Mshindi Ni Charles Chibela ( Chadema) Amepata kura 18 wakati wa CCM amepata Kura 14

Masikini CCM wamekosa hata Unaibu Meya? Kweli yamewafika shingoni. Pole zao. Na kama ni kazi ndo kwanza imeanza twendako watajaza wao.
 
Safi sana,idumu CHADEMA,chama cha kweli cha upinzani.Huu ndiyo upinzani wa kweli tuliokuwa tunausubili!!
 
Hayo ndio tunayoyasema kila siku, Nguvu ya Umma kila siku ndio mshindi! Sijui kwanini watu hawataki kuielewa hii.
 
Ahsanteni watu wa Mwanza you alwayz make me happy.......
Amani kwenu Kirumba,Nyegezi,Nyakato,Nyamanoro,Bwiru,,Ghana,Kamanga Buswelu,Kiseke,Buhongwa,Igoma,Mecco,Igogo,Bugarika,Bugando,Mkuyuni,Kahyenze,Capri Point, Isamilo,Pasiansi,Rufiji,Mabatini,Busisi,Natta,.Miti Mirefu, Langolango nk....MUNGU AWABARIKI NYIE NA VIZAZI VYENU VIWE NA HAMASA HII YA MAGEUZI MILELE NA MILELE HATA HAPO UKOMBOZI WA UKWELI NA MAENDELEO YA KWELI KTK NCHI HII YATAKAPOONEKANA
 
TARATIBU cmm inaanza kupotea. madhara ya arusha jana yameigharimu sana.

Mkuu I said it, hizi akili za 'kimakambamakamba' za kuwapiga mabomu na silaha za moto, watu wasio na silaha kwa kisingizio chochote kile ni ujuha! Amini usiamini kwa tukio la jana Arusha watanzania walio wengi wamejawa na chuki ya ajabu dhidi ya uongozi wa kidhalimu huu wa fisadi CCM, and soon hii hasira italipuka kwa kasi isiyo weza kuzimika!

HONGERENI SANA WANA MWANZA KWA KUFANYA UAMUZI ULIO SAHIHI, NAAM KULINGOA JIJI LETU MIKONONI MWA MAFISADI
 
Moto wa mapambano ndiyo umeanza, ccm na vyombo vyako vya dola kaa tayari kupokea mlichopanda kwa miaaka yote, muda wa mabadiliko ni sasa.
 
Halmashauri ya jiji la Mwanza imepata Meya Josephat Manyeere na Naibu wake Charles Chibela..ambao wote wanatoka CHADEMA.
 
Safi sana, Madiwani Mwanza wamegawanyika namna gani? Chadema wangapi, CCM wangapi, etc

Kama sijakosea Chadema ina madiwani 15+wabunge 2 na ccm ina madiwani 13 na cuf 2.
Cuf na ccm walikubaliana kusupportina kwenye umeya cuf waunge mkono ccm na ccm waunge mkono cuf kwny naibu. Kwenye kura za umeya hesabu ni 17 kwa 15. Kwenye unaibu chadema wamepata support ya diwani wa cuf au ccm maana kura ni 18 kwa 14
 
Mshindi Meya wa Mwanza ni Julius Manyerere (Chadema) amepata kura 17 Wakati wa CCM amepata Kura 15 Naibu Meya wa Mwanza Mshindi Ni Charles Chibela ( Chadema) Amepata kura 18 wakati wa CCM amepata Kura 14

Usahihi wa majina ya wagombea na kura zao kwa Kiti cha Umeya Jiji la Mwanza ni: Chadema-Josephat Kanyonyi Manyerere amepata kura 17 na mgombea wa CCM Stanisilaus Mabula kura 15. Kwa upande wa Unaibu Meya wagombea walikuwa ni Daud Suleiman Mkama wa CUF aliyepata kura 15 na mshindi wa Chadema aliyeshinda kuwa naibu ni Charles Marwa Chinchibera aliyepata kura 17 na siyo 18 kama alivyoandika Ogwalu Mapesa.

Uchaguzi huo umeshuhudiwa na Naibu Katibu mkuu Zitto Kabwe ambaye aliingia leo asubuhi na kusema sasa baada ya kushika Halmashauri sita wanataka kuonyesha mfano wa uongozi kwa CCM katika Halmashauri hiyo, kwanza amesema hazitapata hati chafu tena, na kwa vile zinayo mapato ya kutosha watahakikisha wananchi wanashuhudia mageuzi makubwa
 
Back
Top Bottom