Mwanza - Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015 kama yanavyotujia

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
4,993
Wakuu,

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi Mkuu 2015 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Mwanza. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Mkoa wa Mwanza una jumla ya majimbo ya uchaguzi 9 ambayo ni:-


Ilemela: Ndg. Angelina Mabula ametangazwa mshindi (CCM)

Nyamagana: Stanslaus Mabula (CCM)

Kwimba: Mansoor Hirani wa CCM

Sumve: Richard Mganga Ndasa (CCM)

Misungwi: Charles Kitwanga wa CCM

Magu: Kiswaga Boniventura (CCM)

Sengerema: William Ngeleja (CCM)

Buchosa: John Tizeba (CCM)

Ukerewe: Nicodemus Maganga (Chadema)

ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.


 
Last edited by a moderator:
Nipo hapa jimbo la misungwi tayari nishapanga foleni na watu wanazidi kumiminika na wengine wanahakiki majina na kupanga mstari pia wasimamizi wameshafika tayari kwa zoezi.
more updates to come stay tuned
 
ImageUploadedByJamiiForums1445747155.365797.jpg
Nishachinja tayari, damu inachuruzika tu
 
igoma jimbo la nyamagana hali ni shwari kabisa muda huu na hakuna foleni ndefu vituoni
 
Nani kama Ben Saa8 hapa Tanzania kumwamuru mkuu wa majeda kujitokeza ndani ya cku 7 la cvyo....na akagwaya na kutii na kujitokeza kwa mkwala tu mzito wa maandishi.

Ben Saa8 2025 Bliv me
Tunaomba upeleke mapenzi yako kwenye jukwa la mapenzi, humu ni kazi tu.
 
Niko magu mjini kata ya itumbili, kituo s/msingi itumbili watu niwengi balaa, utulivu upo kazi ni kuchinja tu
 
Nmesikia tetesi za hapo nyamagana mmmh ngoja tuone itavokua inaezaishia kuwa tetesi
 
Back
Top Bottom