MWANZA: Majambazi yavamia dukani na kuua mteja mmoja

Chimo

JF-Expert Member
Aug 31, 2008
714
360
Majambazi yanayosadikika kuwa na silaha za moto (nyingi) wamevamia duka moja mtaa wa Nkurumah na kupora kiasi cha pesa hakijajulikana bado.

Duka hilo linauza bidhaa mchanyanyiko min market pia hutoa huduma za miamala ya njia ya simu M- PESA, Tigo Pesa na Airtel Money.

Wakati wakiwa kwenye harakati hizo aliingia mama mmoja mwenye asili ya kiasia kwa ajili ya kwenda kununua dawa za kutuliza maumivu, panadol ndio majambazi hayo yalipomfyatulia risasi tatu papo hapo na kufariki dunia kisha yenyewe kutoweka kusipofahamika.

Tukio hili limetokea kwenye duka na matukio ya kuporwa kwa watoa huduma za miamala ya pesa kwa njia ya simu imekuwa sugu kwenye jiji hili na mara nyingi hutumika silaha za moto kwenye matukio hayo.

JamiiForums: Picha ya marehemu imeondolewa, haifai kuwekwa mtandaoni.
 
Jamani mama wa watu. ..Alikuwa anatafuta dawa za maumivu, wakaamua wampumzishe kabisa
RIP Mama. ..
 
Duh inasikitisha sana aisee R.I.P mama, si ajabu aliaga watoto kuwa narudi sasa ivi nikanunue dawa lakini hatorudi tena akiwa mzima. Inauma aisee
 
Back
Top Bottom