Mwanza: Mafuriko ya mvua oliyonyesha jana Oktoba 18, yamefukua zaidi ya makaburi 20 eneo la Mswahili

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa moja jana jijini Mwanza nchini Tanzania yaamefukua zaidi ya makaburi 20 katika makaburi ya Waislam eneo la Mswahili, Kata ya Mkuyuni jijini humo Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkuyuni, Ibrahim Joseph amethibitisha.

Akizungumza leo Oktoba 19, 2019, wakati akiongoza kazi ya kutafuta na kukusanya mabaki ya miili ya binadamu ikiwemo mafuvu na mifupa, Mtendaji huyo amesema taratibu za kusitiri mabaki hayo zitafanyika baadaye kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislam.
 
Back
Top Bottom