Mwanza: Madereva wa Mabasi yaendayo mikoani wagoma

yoga

JF-Expert Member
Jan 6, 2013
1,808
8,313
Katika hali ya kushangaza madereva wa mabasi yaendayo mkoani kutokea mwanza wamegoma kuondoa magari stendi kwa madai ya kupunguzwa muda kutoka mwanza kwenda Darkufikia saa tatu za usiku tofauti na ule wa sumatra wa saa tano za usiku ,

Hii ni baada ya magari manne jana kutekwa yakitokea Dar es salaam kuja Mwanza maeneo ya Misungwi! mpaka dakika hii hakuna basi lolote linaelekea mikoa ya Dar, Dodoma, Tabora na sehemu nyinginezo lililo ondok stendi hapa!!!

Wahusika tunaomba mfike Nyegezi mwanza kushughulikia hili maana madhara yake kwa abiria ni makubwa kwani magari yatabidi yaende kwa spidi kufidia muda ulopotea wakati wa mgomo!!!! na hii inaweza pelekea hali ya sinto fahamu!!!!!
 
Wanamgomea nani? Wanamgomea Abiria? Hawajui kuwa anaeathirika zaidi hapa ni Abiria? Tiketi yako imeandikwa muda wa kuondoka? Nadhani kuna haja ya Abiria kuanza kusimamia haki zao!
 
katika hali ya kushangaza madereva wa mabasi yaendayo mkoani kutokea mwanza wamegoma kuondoa magari stendi kwa madai ya kupunguzwa muda kutoka mwanza kwenda dar - salaam kufikia saa tatu za usiku tofauti na ule wa sumatra wa saa tano za usiku , hii ni baada ya magari manne jana kutekwa yakitokea Dar es salaam kuja Mwanza maeneo ya Misungwi! mpaka dakika hii hakuna basi lolote linaelekea mikoa ya Dar, Dodoma, Tabora na sehemu nyinginezo lililo ondok stendi hapa!!!

wahusika tunaomba mfike Nyegezi mwanza kushughulikia hili maana madhara yake kwa abiria ni makubwa kwani magari yatabidi yaende kwa spidi kufidia muda ulopotea wakati wa mgomo!!!! na hii inaweza pelekea hali ya sinto fahamu!!!!!

SUMATRA wako sahihi, hata mchana mabasi hutekwa. Vituo vya ukaguzi viongezwe na trafiki na vyombo vya dola viongezwe.
 
vp mkuu yameshaondoka???

yameanza kuondoka! saahizi afu ni saambili mkuu sipati picha huko njiani maana lazima yakimbizane na mada hasa yale ya DAR ni hatari! na mizani ilivyo mingi nchi hii!!
 
Leo asubuhi katika stendi ya mabasi yaendayo mikoani(Nyegezi), madereva wa mabasi hayo walitishia kugoma kutokana na madereva wenzao kutekwa jana usiku.

Timbwili hilo lilianza mnamo saa kumi na mbili asubuhi mda ambao mabasi mengi yaendayo mikoani ndiyo huanza safari zake.

Aidha katika hoja za madereva hao ni kuwalalamikia SUMATRA kwa kuwalazimisha madereva wanaotokea Dar - Mwanza kufika saa saba usiku ilihali hakuna usalama wa kutosha, pia ni kuwepo na check point nyingi ambazo huwapotezea muda.

Pia wanashangazwa na utaratibu wa kituo cha Ubongo ambao wamekuwa na tabia ya kuruhusu mabasi yaendayo karibu na kuyaacha yanayokwenda mbali.

Mfano mabasi ya Dodoma,Morogoro na Tanga yanaruhusiwa kutoka saa kumi na mbili na yale ya Mwanza,Musoma,Songea yakiruhusiwa kutoka kuanzia saa moja. Baadhi ya mabasi yaliyotekwa jana ni Najumnisa,Lucky Star n.k

Inavyosemekana jumla ya zaidi ya mabasi 3 yalitekwa mkoani Shinyanga,wilaya ya Kishapu kijiji cha Nyasamba ambacho kipo mpakani na mkoa wa Mwanza.
 
hawa watekaji watakuwa ukawa haiwezekani wateke gari peupe hivo na wasikamatwe.
 
Kwa hiyo wanataka magari yaende kwa kasi zaidi ili kuuwai huo muda alafu tufe kwa ajali badala ya kufa na majambazi?!
 
Jana nilisafiri na Lucky Star nilifika mwz saa sita usiku mbona sikuona huo utekaji? Tulipita misungwi saa tano tukakuta Princess Muro imepaki katikati ya barabara peke yake bila abiria. Sasa sijui ndo walitekwaa
 
Back
Top Bottom