Mwanza leo: Je, Tundu Lissu ana "Special Personal Inteligence" inayofanya monitoring ya usalama wake?

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,536
Leo nilikuwa Mwanza kwa shughuli binafsi. Bahati nzuri nikakutana na msafara wa Tundu Lissu maeneo ya Nyegezi ukitokea Shinyanga.

Kwa ambao hawaielewi Mwanza, ni kuwa Nyegezi ni eneo lililo nje kidogo takribani 20km kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza.

Hapa Nyegezi ndipo inapojengwa stendi kuu ya mabasi ya kwenda mikoa ya mashariki, katikati ya nchi, kusini, kaskazini na Pwani...

Sasa kilichowashangaza wengi ni hiki;

Mara msafara wa Tundu Lissu ulipofika usawa wa Kamanga Hospital iliyoko eneo hili la Nyegezi ukielekea katikati ya jiji, ghafla ulisimama kwa dakika chache pale. Haikueleweka wamezungumza nini maana hakuna aliyetoka nje ya gari.

Baada ya muda gari zote za msafara huo, ziligeuza zilikotoka hadi Usagara Njia panda ya kuelelekea Sengerema/ Geita na Shinyanga. Kutoka pale hadi Usagara ni takribani 25km.

Ukaingilia barabara ya Kisesa na kisha ukaja Igoma na kuzungumza na watu pale, na baadaye ukaendelea na safari kuelekea Musoma na Tarime.

Watu wengi walishangaa. Mimi nilishangaa pia. Nikajiuliza intelejensia ya wanausalama wa Tundu Lissu walipokea taarifa gani hata wakabadilisha uelekeo ghafla kwa namna ile?

Mimi sina jibu. Kama unalo, karibu.
 
Kuna "STAGE" fulani mtu akifika, hasa kwenye "USHAWISHI WA UMMA" inakua too late kumuua, kifo chake kinaweza kusababisha machafuko. Badala ya "KUMUUA" sasa inabidi "UMLINDE" kwa hali na mali machafuko yasitokee.

Lissu walivyojaribu mara ya kwanza, ingetimia nia yao basi isingeleta machafuko kwasababu hakufikia "STAGE HII YA USHAWISHI ALIYONAYO", hii hatua wakimuua basi wameipasua nchi na kuleta machafuko.

Ninaamini hao watu "WASIOJULIKANA", wana akili na sio wapumbavu kiasi ya kutokulijua hilo.
 
Kwanza wewe sio mwenyeji wa mwanza.kuanzia mjini kati mpaka hapo kamanga hospital hizo kilometa ulizozitaja sio sahihi.acha kupotosha.jipange upya.
 
Kuna "STAGE" fulani mtu akifika, hasa kwenye "USHAWISHI WA UMMA" inakua too late kumuua, kifo chake kinaweza kusababisha machafuko. Badala ya "KUMUUA" sasa inabidi "UMLINDE" kwa hali na mali machafuko yasitokee...
Na hakuna ajuaye jee machafuko yakitokea hao wanasiasa walio madarakani nao watakufa kwa risasi, mapanga au kuchomwa moto?
Hakuna apendaye machafuko hata kidogo, maana hakuna atakaye kuwa salama
 
Mwanza hakukuwa na watu kabisa ndio maana aliamua kugeuza ili kuepuka aibu
 
Back
Top Bottom