Mwanza kukosa int. Airport ni sawa???

spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,594
3,215
GrEaT ThinkERS!!!
Nijuavyo mimi kuna mambo mengi sana ya kutathmini kabla ya kufanya uamuzi kujenga kitu mahali fulani, Pamoja na yote tumesikia ahadi nyingi za viwanja vya ndege vya kimataifa lakini ni sehemu tofauti sana na Mwanza; Misenyi, Kigoma Bagamoyo nk. Kuna nini huko, kuna kigezo gani huko??
Upeo na Fikra zangu;
  • Mwanza kwanza ni jiji lililo na watu wengi wafanyabiashara, mahoteli na wageni wengi hivyo safari za kimataifa zinaweza kuanzia Mwanza.
  • Mwanza inazunguka na Buzwagi,Kakola mine, Geita Gold mine, North Mara mine, Hata tulawaka Mine, Williamson Diamond(Mwadui) Migodi yote inarusha wafanyakazi kila siku kuwapeleka Nairobi au Dar kwa ajili ya kuwa Concected na Int. airlines ktl viwanja vya huko.
  • Mwanza kuna Sangara wa Kumwa na viwanda vya minofu, Midege mikubwa inahitaji kutua kubeba mizigo kunda sokoni ulaya.
  • Mwanza iko pembezoni mwa mbuga ya Serengeti, watalii wote wanaotokea Ngorongoro na badae Serengeti wanalazimika tena kurudi Kenyata Int. airport Nairobi au kwenda Dar;
  • Mwanza ndiyo Jiji linalobeba Kanda ya ziwa kwa nini isipewe kipau mbele kama kanda zingine au kwa sababu SLEEPING GIANTS wenyewe kila kitu NDONHU SHIDA-Maanake Hamna Shida???
Mimi yangu ni hayo karibuni wana JF tusemezane!:target:
 

Anko Sam

JF-Expert Member
Jun 30, 2010
3,202
813
GrEaT ThinkERS!!!

[*]Mwanza ndiyo Jiji linalobeba Kanda ya ziwa kwa nini isipewe kipau mbele kama kanda zingine au kwa sababu SLEEPING GIANTS wenyewe kila kitu NDONHU SHIDA-Maanake Hamna Shida???
[/LIST]
Mimi yangu ni hayo karibuni wana JF tusemezane!:target:

Sleeping Giant ameanza kufubua jicho moja, ameakaribia kuamka. Si mmeona wenyewe kwenye uchaguzi!
 

smilingpanda

Member
Sep 10, 2009
42
5
sijui sasa hivi ila mwanza bado haijachangamka sana, kinachohitajika ni airport nzuri tu halafu baadae international airport inaweza kuja.na huko bagamoyo airport gani tena? hii terminal 3 haitosho au? au ndo kupoteza pesa tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom