Mwanza: Kuhusu Kesi ya CHADEMA ya kufanya Mikutano nchi dhidi ya Polisi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,486
Shauri la madai na. 79 la mwaka 2016 lililofunguliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kwa niaba ya CHADEMA kuiomba Mahakama itengue amri ya Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa nchi nzima kwa muda usiojulikana na kuitangaza amri hiyo kuwa ni batili, bado linasubiri kupangiwa Jaji na tarehe ya kusikilizwa.

Pamoja na shauri hilo kuwa na maslahi makubwa kwa umma kwa sababu linagusa hatima ya Haki ya Kukusanyika na Haki ya Kujieleza ambazo ni mojawapo ya haki muhimu sana za binadamu, wananchi wanaoendelea kuguswa na udhalimu dhidi ya demokrasia wakiwa na matumaini makubwa katika shauri hilo, wanaombwa kuipatia uhuru Mahakama ili itekeleze wajibu wake katika misingi ya kisheria.

Tuendelee kuwa wavumilivu wakati tukisubiri haki ionekane ikitendeka kupitia uamuzi kwenye shauri hilo lililofunguliwa kwa Hati ya Dharura tukiamini kuwa wakati wowote litapangiwa Jaji na tarehe ya kusikilizwa kwa kadri ya hati ya maombi ilivyo.

Tujiepushe na mikakati au hila za maadui wetu wanaotaka kuonesha kuwa wananchi wenye maslahi na shauri hilo, tunailazimisha au kuisukuma Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kufanya uamuzi.

Taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa tumeshinda ni za uongo na zinasambazwa na watu we nye nia ovu dhidi ya shauri hilo lililoko Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

Makene
 
Lumumba walichanganyikiwa.......wangehamisha majaji kama walivyomuhisha yule wa dar kwa kujifanya kumpa cheo
 
sasa wale waliosema ukawa wameshinda hii kesi,walitolea taarifa wapi??mhh tanzania hii kwa taarifa za kuungaunga hatujambo
 
Asante kwa ufafanuzi.
 
Lumumba walichanganyikiwa.......wangehamisha majaji kama walivyomuhisha yule wa dar kwa kujifanya kumpa cheo

Utajuaje kuwa ni watu wa 'Lumumba'...Pamoja na hayo yule aliyeeneza habari zile amefanya jambo baya mno, wengi wetu tulijua ni uongo...nawapa pole (kwa dhati) kwa wale waliodanganywa (na kuanza kuchangia) na mtu yule aliyeleta uzi humu na ambaye nadhani haitakii mema JF...
 
Back
Top Bottom