Mwanza: Kijana akabiliwa na kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka bibi wa miaka 60

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
MAHAKAMA ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, imemuhukumu mkazi wa Kijiji cha Nange, Shabo Marando (47) kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka bibi wa miaka 60.

Mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mfawidhi Esther Malick, ilitoa hukumu hiyo baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka uliokuwa na mashahidi wanne.

Malick akisoma hukumu ya kesi hiyo ya jinai namba 87 ya mwaka 2019, akichambua ushahidi wa shahidi wa tatu, Dk Judith Kiwango wa hospital ya wilaya, ambaye alimfanyia uchunguzi bibi huyo, alisema alimkuta na michubuko sehemu za siri pamoja na manii.

Shahidi wa pili ambaye ni Sama Luheka (34), mkazi wa Kitongoji cha Igokelo, Kijiji cha Nange, alisema Julai 9 mwaka huu huko Igokelo baada ya kusikia kelele katika vichaka alikwenda eneo hilo na kumkuta mtuhumiwa akimbaka bibi huyo.

Naye bibi huyo aliyebakwa, kwenye ushahidi wake alidai kuwa anamfahamu mtuhumiwa kuwa ni mkazi wa kijijini kwake.

Alidai siku ya tukio alikuwa shambani akikusanya kuni na mtuhumiwa alifika na kusalimiana na mara akamkamata kwa nguvu na kumvutia kichakani na kumbaka.

Katika utetezi wake, mtuhumiwa huyo alidai kuwa mlalamikaji ni shemeji yake, alimpa eneo la kulima na siku ya tukio alikamatwa na wananchi baada ya kuwa amechota maji ya kumwagilia nyanya zake kwa madai kwamba dimbwi alilochota maji lilishazuiwa na kwamba si kweli kwamba alimbaka shemeji yake.

Awali mwendesha mashtaka wa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Juma Kiparo, akimsomea shtaka lake, alidai Julai 9 mwaka huu katika Kitongoji cha Igokelo, mtuhumiwa huku akifahamu kuwa ni kosa alimbaka bibi huyo na kumsababishia maumivu makali.


Chanzo: Mtanzania
 
Sawa amekutwa na manii, na mbona hatuoni sehemu inayosema kua manii ni za mtuhumiwa?

Hatuonyeshwi kama kipimo cha DNA kilifanywa. Mtu mmoja kudai alimuona mtuhumiwa akibaka kisha anayedaiwa kua mhanga akakutwa na manii - ambayo hayako proved ni ya mtuhumiwa - haihalalishi hii hukumu.
 
1575526457300.png

MKAZI wa Kijiji cha Nange mkoani Mwanza, Shabo Marando (47), amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka bibi wa miaka 60.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Esther Malick, baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka uliokuwa na mashahidi wanne.

Ilidaiwa na shahidi wa tatu, Dk. Judith Kiwango wa hospitali ya wilaya hiyo, aliyemfanyia uchunguzi bibi huyo kwamba, alikutwa na michubuko sehemu za siri.

Shahidi wa pili, Sama Luheka alidai alisikia kelele kichakani aliposogea alimkuta mtuhumiwa akimbaka bibi huyo.

Bibi huyo alidai mahakamani kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa alimkuta shambani akikusanya kuni, akamkamata kwa nguvu na kumvutia kichakani kisha kumbaka.

Kwa mujibu wa taarifa ya uhalifu wa kibinadamu iliyotolewa na Jeshi la Polisi, kwa mwaka 2018, kati ya matukio 11,759, ya ubakaji yalikuwa 7,617, sawa na asilimia 64.7.


Chanzo: Nipashe
 
1575622627696.png

Mahakama ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza imemhukumu mkazi wa kijiji cha Nange, Shabo Marando (47) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka bibi.

Hakimu Esther Malick alitoa adhabu hiyo baada ya kuridhika pasi na shaka na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa mashataka akiwamo Dk Judith Kiwango wa hospitali ya wilaya hiyo aliyemfanyia uchunguzi na kumkuta na michubuko na manii sehemu za siri.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Esther alisema ameridhika na ushahidi huo, hivyo anamhukumu mshtakiwa kutumikia kifungo hicho ili liwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kutenda makosa kama hayo.

Alipotakiwa kujitetea kabla ya kupewa adhabu, mshtakiwa alidai mlalamikaji ni shemeji yake na kukana kumbaka bali alimpa eneo la kulima na siku ya tukio alikamatwa na wananchi baada ya kuchota maji ya kumwagia nyanya zake katika dimbwi lililokuwa limekatazwa kutumiwa.

Awali, mwendesha mashtaka wa polisi, Juma Kiparo alidai Julai 9 kitongoji cha Igokelo, mshtakiwa akifahamu ni kosa alimbaka mwanamke huyo.

Source: Mwananchi
 
Dooh, pole sana kijana wa miaka 47,
Lakini pole zaidi ziende kwa bibi wa miaka 60 kubakwa!!? Hakika ni maumivu makubwa sana anayoyapitia kila akikumbuka hilo tukio, anahitaji kuonana na Therapist ASAP.
 
Back
Top Bottom