MWANZA: Jeshi la Polisi lamshikilia raia wa DRC kwa tuhuma za kuiba watoto 3

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Pia jeshi la Polisi wilayani Nyamagana linamshikilia Raia wa DRC Asia Ismail maarufu kwa jina la Hapendeki Katembo kwa tuhuma za kuteka watoto 3, tukio hilo lilitokea Oktoba 18 mwaka huu katika eneo la Shede kata ya Mkuyuni jijini Mwanza

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi, amesema raia huyu alikuwa akiondoka na watoto hao alionekana na mmoja wa wazazi wa watoto hao na kupiga kelele na ndipo wananchi walipokuja kuwaokoa.


Katika tukio jingine watu wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto , waliofariki ni Jackline Machimu (38) anayefanya kazi katika hospitali ya wilaya ya Ngudu na mtoto wake Juliana David (4)
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kubaini chanzo cha moto huo

Katika tukio jingine mtu mmoja amefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kwa radi katika kijiji cha Isenyi wilyani Sengerema


 
Hayo ni matukio machache yanayofahamika tu.ukienda mkoani mara vijana wengi wamechukuliwa kwenda nchi jirani tena kwa kudanganywa wanaenda kupewa kazi wamefika porini wakakabidhiwa kila mtu SMG hakuna kukimbia kuna mmoja alifanikiwa kutoroka akasimulia kila kitu ila hadi leo sioni vyombo vyetu vikifatilia.
 
Back
Top Bottom