Mwanza inapokea 10% tu ya mizigo kutoka Dar huku Kigoma ikipokea 41% ya mizigo. SGR ya Mwanza ni White Elephant project

Good analysis. Now lets dig deeper.
Katika hizo Tani 3.4m za Congo only Tani 136,573 zilihudumiwa na badari ya Kigoma ktk huo mwaka 2017/18 sawa na 4%. Means 96% ya mizigo ya Congo ilipita Isaka to Congo via kigali kwa kutumia njia ya barabara.
What does that tells you?
Kigoma or Isaka?
Wanafikiri bandari ya KG inapeleka mizigo DRC, Rwanda, Burundi hadi UG. Hawaelewi hata kwa nini Isaka inaitwa Bandari kavu. Huyo jamaa hajui logistic za kanda ya ziwa na magharibi. Anatakiwa ajue pia kuna mizigo kwenda DRC na Zambia inapita Katanga Bay, Sumbawanga na siyo Kigoma.
 
Sawa! Haitawezekana mradi wowote uungwe mkono kwa asilimia mia moja.Lazima watu kama wewe muwepo.Ila hilo halitazuia mradi husika kusimama.
Mkuu drone kwan huyo mshikaji umeshamsahau huwa yupo against Mwanza, sasa kigoma( Burundi) kuna uchumi gani kule kulinganisha na kanda ya ziwa? Au tunajenga reli kwaajili ya kusafirisha bidhaa tu nje ya nchi na sio kwa mahitaji yetu ya ndani?
 
Mleta mada,

Target kubwa mbili za SGR ni kiuchumi na huduma kwa wasafiri (wananchi)

Katika target ya kiuchumi SGR itapita pale Isaka ambapo ndio lango kuu la bandari kavu ktk kuhudumia maeneo hasa ya Kigoma, Kahama, Geita nk nchi jirani kama Rwanda, Burundi nazo zitanufaika pia

Katika kuboresha utoaji huduma ktk usafiri, endapo SGR itafika Mwanza basi wasafiri wa mikoa jirani na Mwanza kama Shinyanga, Mara, Geita, Kagera watakuwa wanufaika wakubwa ktk huduma ya treni hii.

Hvyo kwa namna hiyo utaona ufikaji wa treni mpaka Mwanza utahudumia wasafiri wa mikoa takribani MINNE inayozunguka/jirani na Mwanza

Pia, tusisahau hii SGR ni mpango mkakati wa nchi kuendelea kuwin soko lake la kuzilisha nchi jirani kwasababu mwenzetu Mkenya nae anakimbizana na SGR yake ili apore soko letu hasa nchi ya Rwanda na Burundi,, hvyo natoa raí kwa viongozi wetu waongeze kasi ktk ujenzi wa SGR yetu
BIG UP
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Mtoa post unazani sgr Mwanza to Isaka itawanufaisha tu wana kanda ya ziwa? Au unazan mizigo haitaenda kenya, uganda na Rwanda? Unazani kuwa Sumbawanga hawaitaji sgr na wakati huko ndio kuna boda nzuri ya kwenda Congo, Unataka sgr iende Kigoma ili isafirishe mawese kati ya kigoma na dar? Kila kitu kinachofanyika ni kwa manufaa ya taifa kwanza, na je unajua population ya kanda ya ziwa? Unajua uchumi wa kanda ya ziwa kitaifa? Nakushauri acha chuki za kijinga angalia vitu vyenye masilahi kwa taifa kama hutaki sgr iende Mwanza hama nchi au kavunje huo mradi.
 
Kutoka Tabora hadi kigoma Kipande pekee cha barabara ambacho hakina lami ni km 41 za kutoka Kazilambwa(Tabora) kwenda Chagu(Kigoma).....

While barabara ya Isaka to Rusumo kipande kibovu ni kile cha Rusahunga-Rusumo chenye 92km.

We unadhani kwann wana prefer kupitisha 96% ya mizigo ktk km 92 mbovu za barabara ya Isaka-Rusumo over 4% ya mizigo ktk 41km mbovu ya Tabora kigoma?

..inabidi pia kuangalia UFANISI wa bandari ya Kigoma pamoja na meli za mizigo.
 
Wakuu mnogage.

Kwa mujibu wa BBC ikimhoji mtaalam wa Uchumi imebainika kwamba mzigo unaoingia bandari ya Dar es Salaam kuelekea Nchi za jirani via Central corridor ni asilimia 10% tu ya mzigo huo unaelekea bandari ya Mwanza wakati asilimia 41% huelekea bandari ya Kigoma.

Cha kushangaza imekuaje reli ya SGR ijengwe kuelekea Mwanza? Wananchi wa nchi hii tunazidi kubebeshwa mizigo ya misumari Kisa maamuzi ya kisiasa.Mpaka hapo tunazika pesa na kuzalisha white elephant project,very sad.
Huo ni uvivu wa kufikiri na choyo kilichopindukia,population ya watu wa Kanda ya Ziwa ni kubwa mno,pili wana mifugo mingi,tatu kuna madini ya kutosha,nne kuna Ziwa Victoria ambalo ni ziwa kubwa Afrika yote,uzalishaji wa Kanda ya Ziwa huwezifananisha na Kigoma,vile usalama Kanda ya Ziwa kumetulia kuliko Kigoma,kuna mambo muhimu ya kujadili,hili lako mtoa hoja ni chuki binafsi kwa Mwanza na si vinginevyo.
 
Mtoa post unazani sgr Mwanza to Isaka itawanufaisha tu wana kanda ya ziwa? Au unazan mizigo haitaenda kenya, uganda na Rwanda? Unazani kuwa Sumbawanga hawaitaji sgr na wakati huko ndio kuna boda nzuri ya kwenda Congo, Unataka sgr iende Kigoma ili isafirishe mawese kati ya kigoma na dar? Kila kitu kinachofanyika ni kwa manufaa ya taifa kwanza, na je unajua population ya kanda ya ziwa? Unajua uchumi wa kanda ya ziwa kitaifa? Nakushauri acha chuki za kijinga angalia vitu vyenye masilahi kwa taifa kama hutaki sgr iende Mwanza hama nchi au kavunje huo mradi.
Umenena vyema mtu wa Mungu,si kila kitu tukosoe Tanzania ni yetu sote tuwe wazalendo wa kweli,tuache chuki na unafiki wa kikanda.
 
Wakuu mnogage.

Kwa mujibu wa BBC ikimhoji mtaalam wa Uchumi imebainika kwamba mzigo unaoingia bandari ya Dar es Salaam kuelekea Nchi za jirani via Central corridor ni asilimia 10% tu ya mzigo huo unaelekea bandari ya Mwanza wakati asilimia 41% huelekea bandari ya Kigoma.

Cha kushangaza imekuaje reli ya SGR ijengwe kuelekea Mwanza? Wananchi wa nchi hii tunazidi kubebeshwa mizigo ya misumari Kisa maamuzi ya kisiasa.Mpaka hapo tunazika pesa na kuzalisha white elephant project,very sad.
Kigoma ni km 158. Usiogope tutajenga. Mwanza na isaka kuna mzigo wa kutosha sana. Rwanda na DRC Kusini na Uganda pia
 
Hiyo pande haina wanasiasa au wataalamu wenye ukabila au wanaovutia mambo kwao ndio maana yamewakuta hayo.

Kwani huoni reli ya mkoloni iliwahi kufika Kigoma kabla ya Mwanza?

Hata nyie wasukuma wa huko bila yule jamaa kujipendelea kwao hilo daraja, airport, hospital,reli nk mungeishia kuviona Dar na Arusha tuu.

Tzn hii mambo yanaenda.kikabila,kama hamna watu wenye akili kwenye system mtasalia hivyo hivyo.Unaweza ona Magu alivyohawanya mahalmashauri ,mikoa nk huko Kanda ya Ziwa

Kwa hiyo maamuzi hayajali uhalisia bali yanajali nani wa kwetu yuko kwenye nafasi ya maamuzi aweze kupendelea.
Hahaha
Hapo ndo kwenywe aisee
Mwanza imeendelee hata kabla ww hujazaliwa 😃😃
 
Ndo maana ya kuweka miundombinu ya ziada inajengwa meli ya mizigo, daraja la JPM ili demand upande .mh Raisi ulimsikiliza ama ulienda kutafuta kuni. Alisema Mwanza ni mji wa kimkakati katika region
Bongo lala huyo haelewi kitu
Kakaaa kichuki chuki tu
 
Tuseme ulichosema ni kweli je hujiulizi kwanini mpaka leo miaka 60 Kigoma ni mkoa pekee michache iliyobaki haina barabara za uhakika? juzi umesikia Mwanza BOT wamefungua branch pale sababu mikoa ya kule inachangia 25%. kama nilivyosema itakuja kufika kote huko kwa sasa wenye malory ya mizigo au bidhaa za Congo badala ya kuchukulia Dar watakuja hapo Isaka tu na kupeleka Congo hizi ndio fursa zitaletwa na SGR kama dry port mambo mengi yatakuja kwa fursa. feasibility study imefanyika inaweza kuwa ni rahisi mizigo kuchukuliwa Isaka to Congo badala ya kupeleka reli Kigoma lazima tuwaamini waliofanya study na zaidi hata watoa mikopo wanapitia study hizi ili kupitisha mikopo yao kwa kujuwa unafungua fursa katika uchumi. Tuipeni nafasi SGR mimi naamini ni kitu bora kabisa na itapunguza gharama za kurekebisha barabara zetu. Kama tunahoji hili la SGR kwenda Mwanza tungehoji barabara pia kwenda Mwanza kwanza kabla ya Kigoma hapo ingeleta logic.
BOT ina branch Mwanza miaka mingi tu iliyopita na jengo liko Nyerere road. Jengo lililofunguliwa juzi ni kuongeza huduma kutokana na mahitaji kuwa makubwa
 
Tungeomba watu waje na data zinazoonyesha mizigo ya ndani toka Mwanza ni ipi hasa ukilinganisha na Kigoma. Pili je unafikiri kufikiria nchi za nje/majirani ni kosa? Ukiwa mchumi huwezi kuacha kufikiria nchi jirani ili uweze kuendesha reli yako ya umeme. Tulisitazame kikanda tulitazame kiuchumi zaidi.
Wewe mburula kanda ya ziwa si Mwanza tu kuna Kagera, Mara Geita Simiyu na Shinyanga.
 
Back
Top Bottom