Mwanza imezizima wananchi wakesha kuusubiri mwili wa mpendwa wao hayati Magufuli utakaowasili saa 1:00 asubuhi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,725
141,586
Sijapata kuona heka heka za kiwango hiki katika jiji la Mwanza ambapo watu wamekesha kumsubiri mpendwa wao hayati Magufuli waweze kutoa heshima za mwisho.

Kwa kweli hayati Magufuli anakubalika kanda ya ziwa maana nimeshuhudia wageni kutoka pembe zote za kanda hii wakiwa tayari kumpokea, kumuaga na hatimaye kumsindikiza hadi Chato kipenzi chao.

Vituo vya mafuta viko busy kuuza maana kila mmoja ameshakaa mkao wa mapokezi, kuaga kisha msafara kuelekea Chato baada ya zoezi la kumuaga hayati Magufuli kukamilika katika uwanja wa CCM Kirumba.

Updates;
Uwanja wa CCM Kirumba umefurika, watu ni wengi kweli kweli na wote wakiwa na sura za huzuni na simanzi.

Kule kwenye mzunguko ambako wamekaa wananchi wa kawaida kulijaa tangu alfajili kabisa kadhalika jukwaa la viongozi limeshasheheni wahusika.

Mwili wa hayati Magufuli umeshawasili uwanja wa ndege wa Mwanza na sasa msafara umeanza kupita katika mitaa mbalimbali ya jiji la Mwanza na baadae kuelekea uwanja wa CCM Kirumba.
 
Back
Top Bottom