Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,642
- 6,071
Wakuu
Leo CHADEMA imefanya kufuru nyingine katika Jiji la Mwanza. Umefanyika mkutano mkubwa katika Uwanja wa Sahara ambao uko maeneo ya katikati kabisa ya Jiji hili lililozungukwa na madhari ya milima yenye utajiri wa madini na Ziwa Viktoria lenye utajiri wa samaki, uliofuatiwa na maandamano makubwa ya amani yaliyodumu kwa saa nzima na zaidi.
Siku ya leo wananchi wa Mwanza wamepeleka ujumbe mkubwa sana kwa watawala. Kwanza kwa namna isiyokuwa ya moja kwa moja, wame-challenge umuhimu wa ile sheria inayohitaji wananchi 'kuomba' (au kutoa ripoti?) kibali cha kuomba kuandamana.
Pili wametuma ujumbe tena kwa mara nyingine kuwa maandamano ya CHADEMA yasipoingiliwa na polisi, hayawezi kuwa na vurugu hata kidogo. Watu mbalimbali, wanaume kwa wanawake, watoto kwa wakubwa, vijana kwa wazee, wameandamana na msafara wa Katibu Mkuu, Dkt. Slaa kutoka eneo la mkutano mpaka Hotel aliyokwenda kupumzika.
Hakuna namna nyingine ya kuweza kuita hali hiyo isipokuwa kusema wazi kuwa yalikuwa maandamano ya amani kwa takriban saa 1 na kitu. Jiji la Mwanza kwa muda wote huo hasa maeneo ya katikati hadi maeneo ya Bwiru shughuli zilisimama kwa muda. Jiji lili-paralyze kwa muda.
Vijana wanaimba "mafisadi wajiuzulu, mafisadi wajiuzulu". Ilikuwa ni baada ya nondo za uhakika kupigwa pale uwanjani, kuhamasisha masuala mbalimbali ikiwemo vita takatifu dhidi ya UFISADI na MAFISADI.
Mkutano wa leo Mwanza umehitimisha ziara ya siku 10 ya Dkt. Slaa kukagua uhai wa chama katika mikoa 5 ya Tabora, Shinyanga, Simiyu, Geita na Mwanza ambayo ilikuwa ni mwendo wa vikao vya ndani asubuhi, mchana, jioni mikutano ya hadhara kisha vikao vya ndani tena usiku.
Maandamano yalikuwa makubwa kwa kweli. Watu wamehamasika. Rebellion dhidi ya CCM na utawala mbovu unaoandamwa na kashafa moja baada ya nyingine uko wazi sana wakuu.Umati wa watu wamelazimika kukimbia umbali wa takriban kilometa 5, kutoka Sahara pale mpaka maeneo ya Bwiru,
Kama ilivyo ada, maelefu ya watu wa Mwanza waliitikia wito kisha wakakubaliana na nondo zilizokuwa zikipigwa na makamanda tangu majira ya saa 9 mpaka saa 12, bila ulinzi wa polisi. CHADEMA wanajilinda wenyewe katika mikutano na maandamano. Wakiachiwa, wanaweza.
Makamanda, wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Slaa, Godbless Lema, Mwita Mwikabe Waitara na wengine kibao, waliwakoga wananchi kwa hoja zinazozungumzia namna ya kutafakari mstakabali wa taifa.
Nondo za leo zilikuwa ni;