Mwanza: Freeman Mbowe afungua Kikao cha kamati kuu, amzungumzia Lowassa

Mboww nawe tumekuchoka. Hii kauli ya tunataka tumeichoka. Tupe go ahead tuingie barabarani tu.
 
KILICHOTOKEA GEITA HAKIJAWAHI KUTOKEA KOKOTE DUNIANI POLISI KUANDIKISHA MAELEZO YA MTU WANAOMLINDA,NI UNAFKI MKUBWA" MBOWE

UPDATES - MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA , MHE. FREEMAN MBOWE AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA.

Wakati Mhe. Lowassa akielekea katika Kata yw Mkone jimbo la Geita vijijini ambako kuna Kampeni GB zinazoendelea za udiwani katika uchaguzi mdogo wa marudio, alizongwa na wananchi waliokuwa na shauku ya kumuona kama Kiongozi wao, tabia za Watanzania kupenda viongozi wawasalimie hazikuanzia kwa Lowassa.

No utamaduni wetu uliojengeka kwa miaka mingi,Wabunge wanasalimia,Madiwani wanasalimia sembuse Mgombea Urais ambae kwetu alishinda kura katika Uchaguzi wa mwaka juzi, wakati Mhe. Lowassa anawasalimia wananchi wale,polisi walikuja wakazunguka gari yake na kumchukua kumpeleka kwenye kituo kwa maelekezo ya OCD wa Geita.

Kitendo hiki tunaona ni kitendo cha kuendeleza muendelezo wa muda mrefu wa jeshi la polisi kuingilia shughuli zetu halali za kisiasa ni muendelezo wa jeshi la polisi kuendelea kuwa wakala wa chama cha mapinduzi na ni muendelezo wa jeshi la polisi kukihujumu chama hiki pindi zinapotokea chaguzi mbalimbali kuanzia za Rais, Wabunge, Madiwani na hats serikali za mitaa na vijiji.

Tumesikitishwa zaidi na kauli ya kinafki iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita eti kwamba walifanya kitendo kile kumlinda Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, hayo ni maneno ni maneno ya kudhihaki umma,kwani haiwezekani ukamlinda mtu kwa kumkamata kumzuia kuifanya shughuli yake aliyokuwa amekusudia kuifanya tena shughuli ambayo ina muda maalum wa kuitekeleza ukamshindisha kwenye kituo cha polisi ukamuamisha kutoka ofisi moja kwenda nyingine ukawapiga mabomu wananchi waliokuwa wanampokea bila kuwa na hatia yoyote ukawapiga waandishi wa habari bila kuwa na hatia yoyote na kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kuchukua habari, kisha huyo unae dai unamlinda ukamtaka aandike maelezo haijawahi kokote duniani imetokea Geita peke yake . Kuwa MTU anayelindwa anatakiwa atoe na maelezo polisi, sijui anatoa maelezo ya nini.

Kwa hiyo tunalaani kitendo hiki cha jeshi la polisi wamuache Mhe. Lowassa afanye siasa kama vile Kiongozi mwingine yeyote katika nchi yetu, waache viongozi wetu wanapokuwa wanaheshimika na kukubalika miongoni mwa umma waache umma uonyeshe hisia zake kwa viongozi wetu na jeshi lisiingilie viongozi wengine wa chadema katika ngazi mbalimbali wanapokuwa wakitekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na haki za kibinadamu.

Jeshi la Polisi kwa muda mrefu limekuwa linafungulia mashtaka mengine ya kubuma viongozi wetu mbalimbali katika maeneo mbalimbali na tunaamini jeshi la polisi ni serikali ni mkono wa serikali ni mkono wa chama cha mapinduzi na tuna imani kabisa kwa upole huu ambao sisi tunaonyesha kwa kuwa wapole na wanyenyekevu kwa vyombo vya umma itafika siku tutashindwa kuendelea na uvumilivu huu.

Wote mnazo taarifa bado Mbunge wetu ameendelea kusota maabusu mwezi wa tatu huu,Rais anazo taarifa, Waziri Mkuu anazo taarifa, Kamanda Mkuu wa Polisi anazo taarifa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali anazo taarifa, Jaji Mkuu anazo taarifa sasa kama viongozi wote hawa waandamizi ambao wanastahili kuisimamia haki katika nchi yetu wanaona watu wetu wakifanyiwa vitendo vya kishenzi vya kjnyama vya kihuni na wao viongozi wakaendelea kusherehekea na kuona nchi yetu ni ya amani sana ni jambo la kusikitisha sana sisi kama chama tunawalaumu sana kwa unafiki huko na tunawaambia Leo wataitesa chadema kesho watajikuta wanawatesa wenzao ndani ya chama chao au ndani ya serikali yao.

Tunataka nchi hii iongozwe kwa sheria na sio kwa visasi sio kwa chuki sio kwa giliba kila Mtanzania anaetaka kufanya siasa afanya siasa kwa mujibu wa sheria za nchi na sio kwa mapenzi ya Rais John Pombe Magufuli.

Bado sisi kama chama tunalalamika na tunadai haki yetu ya kufanya mikutano na kufanya kazi zetu za siasa kwa uwazi bila kificho kwa sababu ni haki yetu ya kisheria na Kikatiba, hatuendi kufanya mikutano ya hadhara sio kwa sababu tunaogopa tunaamini wapo watu wengine wenye nafasi mbalimbali kwenye akili timamu amabo hatimaye wataweza kuwashauri watawala wetu kwamba huko sio uongozi.

Kwa hiyo bado tunaendelea kudai haki yetu ya kufanya mikutano ya hadhara na tunadai Uhuru wa viongozi wetu kuwasalimia wananchi wakati wowote kama vile Rais Magufuli, mara kwa Mara amekuwa akisimama njiani na kuwasalimia wananchi.
 
Tanzania tujitoe AU... Gambia wametoa tamko ila Zanzibar giza totoroo
 
Watu wanataka chakula mlicho ahidi kanisani kukigawa kwa wenye njaa ili dunia isikie na sio kuleta usani sani hapa wakati mnajua watu wana njaa. Au ndo kama kawa kwa ulaghai.
 
Rais anasalimia wananchi kama kiongozi wa nchi sasa lowassa anataka akusanye wananchi na kuwasalimia kama nani
 
Back
Top Bottom