Mwanza: Familia yazika mtoto wa kike akiwa hai ili wapate utajiri

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,779
18,746
Watu watatu akiwemo mkazi wa Kijiji cha Mahaha wilayani Magu mkoani Mwanza, Zawadi Msagaja (20), (Wa kwanza kulia), wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kike mwenye umri wa miezi sita kwa kumzika shambani akiwa hai ili wapate mali.


mauajii.jpg

Wa kwanza kulia ni Zawadi Msagaja (20), ambaye ni mama wa mtoto na anayefuatia ni dada wa Zawadi
Ni kesi ya mauaji namba saba ya mwaka 2022 ambayo imesomwa na Mwendesha Mashtaka wa serikali Mwanahawa Changale, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Fortunatus Kubaja, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza ambapo amesema washtakiwa hao watatu akiwemo Zawadi Masaga ambae ni mama wa mtoto huyo, Elizabeth Kaswa ambae ni dada wa Zawadi pamoja na Mume wa Elizabeth ambae pia ni mganga wa kienyeji aitwaye Mussa Mazuri kwa pamoja walitenda kosa hilo Novemba 13 mwaka huu kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu marejeo namba 16 ya mwaka 2022.

Baada ya washtakiwa hao kusomewa shtaka hilo la mauaji linalowakabili, Hakimu Mkazi Mwandamizi Kubaja akaiahirisha kesi hiyo hadi kesho Desemba 28 itakapotajwa tena na washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kisheria ya kusikiliza shauri hilo.

=======

Watu watatu wanaotuhumiwa kumzika mtoto akiwa hai, wamepandishwa kizimbani kwa tuhuma za kumuua mtoto huyo mwenye umri wa miezi sita kwa imani za kishirikiana ili wapate mali.

Watuhumiwa hao ni mkazi wa kijiji cha Mahaha wilayani Magu mkoani Mwanza, Zawadi Msagaja (20), dada yake Zawadi, Elizabeth Kaswa pamoja na mumewe, Mussa Mazuri ambaye ni mganga wa kienyeji.

Watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza na kusomewa shitaka ya mauaji ya mtoto huyo.

Akiwasomea shitaka hilo, leo Desemba 27, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Fortunatus Kubaja, mwendesha mashtaka wa Serikali, Mwanahawa Changale amesema washtakiwa walitenda kosa hilo Novemba 13, 2022 kinyume na kifungu namba 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu marejeo namba 16 ya mwaka 2022.

Amesema washtakiwa katika kesi hiyo ya mauaji namba 7/2022 walitenda kosa hilo katika mtaa wa Kisundi, kata ya Bugogwa, wilayani Ilemela mkoani humo kwa kumzika mtoto huyo akiwa hai ili wapate mali.

“Washtakiwa wote mchana wa siku hiyo mlishirikiana kumpatia mtoto wa Zawadi dawa ya kienyeji akalewa kisha mkamfukia akiwa hai na kumsababishia kifo kwa malengo ya kujipatia mali kinyume na sheria,” ameeleza Changale.

Baada ya washtakiwa kusomewa shitaka linalowakabili, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kubaja ameahirisha kesi hiyo hadi kesho Jumatano Disemba 28, 2022 itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa huku washtakiwa wakitakiwa kutozungumza chochote kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kisheria ya kusikiliza shauri hilo.

Mwananchi
 
Kanda ya ziwa mjitathmini.
Matukio yenu yanawafanya muonekane Watu wa ajabu.
Mnawaharibia wenzenu ambao tunawajua wanatabia nzuri
Yaani unavyaoandikaga makala nzuri humu jukwaani Ila one person una publicize the whole area, you're devaluing yourself socially.

You seem like you've zones even smt tribalism trauma. Isitoshe kusema kwako kusema nyie wa...... Mko hivi ni very easy kwako. Sorry ni just mind
 
Back
Top Bottom