KUGAWANYIKA kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kuundwa kwa Halmashauri mpya ya Wilaya ya Ilemela kumekirejeshea Chama Cha Mapinduzi (CCM) matumaini ya kuongoza tena jiji hilo, huku Chama cha Wananchi (CUF) ndicho kikiwa na kura ya kuamua nani anakuwa Meya.
Taarifa kutoka ndani ya CCM hapa Mwanza zinaeleza kuwa tayari vikao vya mikakati vimeanza ili kufanikisha mipango ya kuongoza Jiji hili kwa kuwashirikisha madiwani wawili wa CUF ili waweze kuungana na chama hicho dhidi ya CHADEMA katika uchaguzi wa meya.Taarifa kutoka ndani ya vikao hivyo zinaeleza kuwa mlengwa katika mikakati hiyo ni Diwani wa CUF wa Kata ya Mirongo, Daud Mkama, ambaye ataungwa mkono na CCM katika umeya ili nacho kiungwe mkono na CUF kwenye unaibu meya.
Hata hivyo, inasemekana ahadi hiyo inaweza ikawa inatumika kumvuta diwani huyo na chama chake kuwaunga mkono tu kwa kuwa CCM wana hofu kuwa CHADEMA wana uwezekano mkubwa wa kumfanya awe naibu meya hivyo CCM imemuahidi umeya ili kukichanganya CHADEMA.
Mheshimiwa (Mkama) anashawishiwa kwa kuwa kuna taarifa kuwa CHADEMA wameahidi kumuunga mkono kama naibu meya. Wanachofanya CCM ni kumvuta aamini kuwa anaweza kuwa meya, lakini kwa uhakika uko mkakati mwingine ambao haujui utaibuliwa dakika za mwisho ili malengo ya CCM kunyakua umeya yatimie na yeye ataambulia unaibu meya, kinaeleza chanzo chetu toka ndani ya vikao hivyo.
Tayari ziko dalili kuwa CUF wanaweza kuwa wamekubaliana kuwaunga mkono CCM na kuwaacha wapinzani wenzao CHADEMA kwa kuwa juhudi za CHADEMA kumshawishi diwani huyo zinaeelekea kukwama.
Habari hizi zimekasirisha wananchi wengi wa Jiji la Mwanza na kuhoji endapo kama kweli chama cha CUF ni wapinzani wa kweli au ni vibaraka wa CCM.
Source:Raia mwema.