Mwanza: BAWACHA wapata safu mpya ya uongozi wa Kitaifa: Sharifa Suleiman, Catherine Ruge, Bahati Chumu, Nuru Ndossi, Aisha Machano

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,521
217,786
Amechaguliwa leo kwenye Mkutano Maalum ulioitishwa Mwanza ili kuziba pengo la wale Corona 19 waliovuliwa uanachama.
=====
1621419278361.png

Sharifa akabidhiwa mikoba ya Mdee Bawacha

Chama cha Chadema kimemteua Sharifa Suleiman kuwa kaimu mwenyekiti wa Baraza la wanawake la chama hicho (Bawacha) ambapo kabla ya uteuzi huo, Sharifa alikuwa makamu mwenyekiti wa baraza hilo.

Mwanza. Chama cha Chadema kimemteua Sharifa Suleiman kuwa kaimu mwenyekiti wa Baraza la wanawake la chama hicho (Bawacha) ambapo kabla ya uteuzi huo, Sharifa alikuwa makamu mwenyekiti wa baraza hilo.

Akizungumza leo Jumanne Mei 18, 2021 katika kikao maalumu cha kuchagua viongozi wa chama hicho kujaza nafasi zilizoachwa wazi, katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema kutokana na Sharifa kutosaliti wala kuhasi chama, kamati tendaji ya Chadema wamempitisha kukaimu nafasi hiyo mpaka watakapoitisha uchaguzi.

“Kuna jambo jingine ambalo ofisi ya katibu mkuu na Bawacha tulifikiria lifanywe na Bawacha, mchakato wake wa kukaimisha kwa muda zile nafasi nyingine zilizo wazi ambazo hamna mamlaka ya kikatiba ya kumchagua kuziba moja kwa moja.”

“Kwa uamuzi huo hatutokaimisha nafasi hizo kwenye kikao hiki badala yake Chadema ina utajiri mkubwa wa taratibu za uendeshaji wa chama. kwa uamuzi wa kamati kuu tunapenda kutumia kifungu cha 12(0) cha itifaki ya chama ambayo kifungu cha 12.12 (2) kinasema yafuatayo na naomba ninukuu.

“Makamu wenyeviti watakuwa wasaidizi wakuu wa wenyeviti na kazi zao na kukaimu wakati ambapo wenyeviti hawapo, kwakuwa hakuna mwenyekiti, makamu mwenyekiti alibaki ambaye hakushiriki usaliti, uhasi na ubinafsi sasa yeye atakaimu uenyekiti mpaka pale tutakapoitisha mchakato wa uchaguzi wa kuziba nafasi,” amesema Mnyika.

Bawacha wapata safu mpya ya uongozi wa juu

By Saada Amir
  • Uchaguzi umefanyika ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi baada ya baadhi ya viongozi wake kuteuliwa kuwa wabunge wa viti maalumu bila ridhaa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mwanza. Baada ya kumwondoa Halima Mdee na wezake 18, Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) limemchagua Catherine Ruge kuwa katibu mkuu kwa ushindi wa kura 34 dhidi kura 23 alizopata mshindani wake wa karibu, Ester Daffi.

Mgombea mwingine wa nafasi hiyo, Asia Msangi ameyepata kura nane ambazo hazikutosha kumpa uongozi alioumba kwa makada wenzake.

Wakati Catherine akiibuka mshindi wa nafasi hiyo ya juu, Bahati Chumu Haji amechaguliwa kuwa naibu katibu mkuu (Zanzibar) ambaye alikuwa mgombea pekee kwa kupata kura 60 za ndiyo na tano za hapana.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jijini Mwanza leo, Ruth Mollel aliyekuwa msimamizi amemtaja Nuru Ndossi kuwa mshindi wa nafasi ya unaibu katibu mkuu (Bara) kwa kupata kura 33.

Nuru alichuana na Brenda Rupia aliyeondoka na kura 17 na Emma Bhoki aliyepata kura 15.

Nafasi nyingine iliyopata kiongozi ni mratibu uenezi wa Bawacha Taifa ambayo amechaguliwa Aisha Machano Amme aliyepata kura 36 hivyo kumshinda Husna Said aliyepata kura 23.

Uchaguzi huo wa Bawacha umefanyika ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi baada ya baadhi wa waliokuwa viongozi kuvuliwa uanachama kwa tuhuma za kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama.

Licha ya msimamo huo wa chama, Spika wa Bunge, Job Ndugai ameendelea kuwatambua akisema hakuna utaratibu uliokiukwa ndani ya chama hichio kilichokuwa kinaongoza kwa idadi kubwa ya wabunge wa upinzani kwenye Bunge la 11.
 
Back
Top Bottom