Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,023
- 1,609
Mkazi wa Mtaa wa Mlimani 'A' eneo la Kabuoro Kata ya Kirumba wilayani Ilemela mkoani Mwanza, Mohammed Khatibu (29) anadaiwa kuvunjwa miguu na Askari wa Polisi ambaye ni Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Kiseke wilayani humo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Paulo aliyekuwa anamtuhumu kuwa na mahusiano na mke wake.
Licha ya hila za askari polisi kutaka kumfichia siri mkuu wao, jitihada binafsi za Hidaya Somba zilisaidia kutambua alikofichwa mwanaye, Mohamed Khatibu (29) aliyekamatwa akiwa nyumbani kwao kwa tuhuma ambazo hazikubainishwa na alipofuatiliwa ikaelezwa hayupo mikononi mwa polisi.
Taarifa zilizothibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya zinasema Khatibu alikamatwa Januari 3 na Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Kiseke kilichopo wilayani Ilemela, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Paulo ambaye anadaiwa kumvunja miguu na kiuno akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mzazi mwenzake.
Katika ukamataji, askari huyo ambaye ametoroka na sasa anatafutwa, anadaiwa kushirikiana na rafiki yake, wakitumia gari binafsi waliloenda nalo nyumbani kwa Khatibu katika Mtaa wa Mlimani A na kumkamata bila kumweleza kosa lake wakisema wanampeleka Kituo cha Polisi Kirumba ambako ndugu walipofuatilia hawakumkuta, kwani alipelekwa Kiseke.
Kituoni hapo alipigwa akihojiwa kwa nini ana uhusiano na mke wa mkuu huyo wa kituo mpaka akavunjwa vikombe vya magoti na majeraha kwenye uti wa mgongo kama ilivyothibitishwa na vipimo alivyofanyiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando.
Mama Mzazi wa Khatibu amesema baada ya kumkosa mwanaye Kituo cha Kirumba, walipata fununu kuwa yupo Kituo cha Kiseke lakini nako waliambiwa hakuwepo. Hata hivyo kutokana na kuwa na uhakika kuwa mwanae yupo Kituoni hapo alijifanya anaenda chooni, akazunguka nyuma ya mahabusu na kuita jina kwa sauti, ambapo aliitikia akiwa mahabusu,”
Kamanda Msuya alisema japo mtuhumiwa namba moja katika tukio hilo ametoroka, uchunguzi unaendelea na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaothibitika kushiriki uhalifu huo.
“Primary suspect (Paulo) kwenye tukio la mtu kushambuliwa ametoroka na tunaendelea kumtafuta, uchunguzi ukikamilika wahusika watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria sawa na watuhumiwa wengine,” alisema Msuya.
Chanzo: Mwananchi