Mwanza: Amuua mke wake kwa mapanga, kisa wivu wa mapenzi

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,445
99,033
Mwanza. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mkazi wa Buhongwa, Omary Lucas (48) kwa tuhuma za kumuua mke wake, Elizabeth Lusana (61) kwa kumkata mapanga kutokana na wivu wa mapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano leo Julai 13, 2022 jijini Mwanza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng'anzi amesema tukio hilo la mauaji lilitokea Julai 11, 2022 baada ya kuibuka ugomvi baina ya wanandoa hao.

Amesema marehemu, Elizabeth mkazi wa mtaa wa Kagera kata ya Lwanhima jijini Mwanza aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali maeneo mbalimbali ya mwili wake huku jeshi hilo likimkamata mkazi wa Isabenda kwa kumficha mtuhumiwa huyo.

"Uchunguzi wa awali umebaini wana ndoa hao walikuwa na ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi ambapo mwanaume alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano yasiyofaa nje ya ndoa uliopelekea mauaji hayo," amesema Ng'anzi na kuongeza

"Mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na kwenda kujificha mkoani Tabora kwa Amos Lucas lakini ufuatiliaji wa Polisi uliweza kubaini mahali alipo na kuwakamata yeye na mtu aliyemficha," amesema

======

Omary Lucas (48), Mkazi wa Buhongwa jijini Mwanza anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mke wake, Elizabeth Lusana (61) kwa kumkata mapanga kutokana na wivu wa mapenzi.

Advertisement
Mwanza. Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia mkazi wa Buhongwa, Omary Lucas (48) kwa tuhuma za kumuua mke wake, Elizabeth Lusana (61) kwa kumkata mapanga kutokana na wivu wa mapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano leo Julai 13, 2022 jijini Mwanza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhan Ng'anzi amesema tukio hilo la mauaji lilitokea Julai 11, 2022 baada ya kuibuka ugomvi baina ya wanandoa hao.

Amesema marehemu, Elizabeth mkazi wa mtaa wa Kagera kata ya Lwanhima jijini Mwanza aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali maeneo mbalimbali ya mwili wake huku jeshi hilo likimkamata mkazi wa Isabenda kwa kumficha mtuhumiwa huyo.

"Uchunguzi wa awali umebaini wana ndoa hao walikuwa na ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi ambapo mwanaume alikuwa akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano yasiyofaa nje ya ndoa uliopelekea mauaji hayo," amesema Ng'anzi na kuongeza

"Mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na kwenda kujificha mkoani Tabora kwa Amos Lucas lakini ufuatiliaji wa Polisi uliweza kubaini mahali alipo na kuwakamata yeye na mtu aliyemficha," amesema

Katika tukio lingine, mtoto mwenye umri wa miaka mitano, Ally Sipendeki mkazi wa Nyabulogoya kata ya Nyegezi jijini Mwanza alifariki dunia baada ya kuungua na moto kutokana na ajali ya moto uliounguza nyumba ya Pastory Nestory (70) ambaye ni mwalimu mstaafu wa shule ya msingi Nyabulogoya.

Kwa mujibu wa RPC Ng'anzi tukio hilo lilitokea Julai 12 saa 1:19 usiku ambapo moto huo uliteketeza mali za wapangaji watatu wa nyumba hiyo ambazo thamani yake bado haijafahamika.

"Chanzo cha moto huo kinachunguzwa kwa kushirikiana na idara zinazohusika. Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa Bugando kusubiri uchunguzi wa daktari baada ya uchunguzi kukamilika utakabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi," amesema Ng'anzi.

Chanzo: Mwananchi
 
Mbona hatujapumzika la Said jamani na missed 42 col na hili Tena. Sijui mza sura zetu tunaziweka wapi. Ila Lowe Ni la Taifa zima. Poleni kwa wafiwa.

Halafu Kama umri sijauona vizuri. Aliyekuwa bright ama kipanga wanisadie kusoma hizo namba, yaani kweli kusoma PCM sio kuwa ndio kujua namba
 
Mwanza kuna matatizo gani na wanaume wa huko?

Sisi wa dar huwa mnatusema ila ni wachache ndio wanaweza kuwa na mawazo ya kijinga kama hayo ya kwenu.
 
Ukishaona mwanamke anatoka nje ya ndoa achana nae huyo mapenzi na wewe yamefika mwisho.
Sahii kabisa,

Afu nadhan Kuna kauli flan za kebeh na dharau wanawake huzitoa kwa mumewe akishaanza kutokana nje.

Nadhan hiki ndicho kinachozaa maafa yote haya
 
Ukishaona mwanamke anatoka nje ya ndoa achana nae huyo mapenzi na wewe yamefika mwisho.
Na mwanamme akitoka nje ya ndoa asiachwe.
Auliwe? Siku hizi mkuu naona ngoma droo..kina mama wanakata jongoo kwa meno!

Tujiangalie Sana!
 
Back
Top Bottom