Mwanza: Amuua mke wake kwa kumpiga risasi, naye ajiua

Fundisho:
Mkishaoana muache mambo mengine ya ajabu ajabu ambayo huleta uadui. Maana unapokwenda kinyume na mwenzako huwezijua moyoni mwake na akili yake inakuwaziaje!!!!
Hii ndiyo hatma ya kutoelewana katika maisha ya wanandoa.
Sure
 
Mkazi wa Mahina, jijini Mwanza, aliyefahamika kwa jina moja la Max, anadaiwa kumuua mke wake, Teddy Malulu kwa kumpiga risasi usiku wa kuamkia leo.

Baada ya kufanya mauaji hayo, Max naye anadaiwa kujiua kwa kujipiga risasi.

Mpaka sasa chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana. Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa mwanamke anayedaiwa kuuawa na mume wake ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wavuvi Tanzania (Tafu) .

Kamanda Msangi amesema uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea.
Siyo mkazi wa Mahina bali ni mkazi wa Mtaa wa Kanyerere,Kata ya Butimba,Wilaya ya Nyamagana.Hilo ni fundisho kubwa sana kwa wanandoa. Kwa maelezo ya binti wa marehemu ulitokea ugomvi na mama akawa anaongea maneno machafu sana dhidi ya mumewe,inawezekana ikawa ni kiburi cha pesa...!!!
 
Nchi zetu hazina wale watoa ushauri wa kisaikojia ambayo husaidia kuvunja ukimya na kupunguza msongo wa mambo na maamuzi magumu kama haya. Ni muhimu ukiwa na ishu nzito kushea inasaidia kufanya maamuzi sahihi.
Shida ya maisha yetu ya siku hizi,rafiki yako ni yule tu mwenye rika moja na wewe,hatuna marafiki wanaotuzidi umri(wazee) ambao unaweza kuwaomba ushauri wakakusaidia, Mambo kama haya kwa wazee yanasovika
 
Kujitoa uhai na kutoa wa mwingine pia ni kosa la jinai na analakujibu mbele za Mungu, wakati mwingine ni vyema umilikishwaji wa silaha upewe vigezo zaidi kwa majaribio ya mara kwa mara kabla ya kukubaliwa umiliki
Hii haisaidii!Kwanza watu wapole ndio hufanyiwa ujinga ujinga na wanawake na ndio wanaofanyaga mambo ya kushangaza kama mauaji hayo!Utapimaje ili utoe silaha,kwani hasira hupanda ghafla na bila kutarajia
 
Mkuu;
Kama ulimsikiliza kamanda Msangi, lazima utaelewa kuwa Max alikuwa na hiyo bunduki siku nyingi tu. Ila hili la kumuua mtu na yeye kujiua nadhani ni wazo la siku nyingi sana alikuwa nalo kichwani. Hii husababishwa na maneno ya huyo mwanamke. Na maneno hayo siyo mengine, ni dharau za kwenye 6 x 6. Max akaona, waondoke wote asije waachia wengine mzigo wakijipigia watakavyo.
Kama wote wanaofanyiwa usaliti wakiua....tutabaki na yatima wengi sana!
 
Kama wote wanaofanyiwa usaliti wakiua....tutabaki na yatima wengi sana!

RRONDO;
Nashukuru mkuu kwa kunielewa. Sasa tuje na wazo kuwa, enyi mlio olewa au mliooa; punguzeni mambo yenu kwani mnachokifanya ni mateso kwa uzao mlio nao.
Iwepo kanuni kuwa, ukiona ugomvi hauishi ndani ya nyumba, serekali iingilie kati na kuwatenganisha kwa amri kuwa, usimuonee mwenzio wivu aendako. Pia, usipokelewe na mtu mwingine huko, ukapata raha. Huenda yakapungua. Muaji huja kwa sababu; Hakuna mdume awezaye kumwangalia mzazi mwenzie akiwa amekumbatiwa na mwanamume mwingine. Hayupo huyo. Si umesikia huyo aliyekufa kwa sonona?? Acha tu mazee, yasikie kwa mwenzio.
 
Ushahidi wa kusema na yeye kajiua baada ya kuua nani anao. Hapa unaweza kuta mtu kawaua wote kwa pamoja na kusingizia kuwa kaua na kujiua
 
Ushahidi wa kusema na yeye kajiua baada ya kuua nani anao. Hapa unaweza kuta mtu kawaua wote kwa pamoja na kusingizia kuwa kaua na kujiua

Watoto wao walivyohojiwa ndio wamesema ... so hao watoto ndio wanaweza kua wamesema uwongo au ukweli
 
Kujitoa uhai na kutoa wa mwingine pia ni kosa la jinai na analakujibu mbele za Mungu, wakati mwingine ni vyema umilikishwaji wa silaha upewe vigezo zaidi kwa majaribio ya mara kwa mara kabla ya kukubaliwa umiliki
Silaha nini tafsiri yako?

Vitoa roho ni vingi. Usipomilikisha bunduku watauwana kwa njia nyingine mbadala.
 
Ushahidi wa kusema na yeye kajiua baada ya kuua nani anao. Hapa unaweza kuta mtu kawaua wote kwa pamoja na kusingizia kuwa kaua na kujiua
Mkuu,

Huyo kajiua kweli baada ya kumuua mkewe. Niliangalia habari Jana. Alijiua kwa kujipiga risasi 2.

Yani alijipiga risasi ya kifuani, akaona haitoshi akajipiga mkononi tena! Sijajua alitumia bastola ya aina gani na size ya risasi.
 
Sina maana hio,ila nadhani ts time wanaume waelewe wanawake miaka hii si kama miaka ya zamani, makuzi ya binti miaka hii na miaka ya 70's ama 80's ni tofautiii sanaaa...
Nani anamfundisha huyu mwanamke kushuka wakati miaka yote anakuzwa aambiwa u can do what a man can do??
Mme unaoa uaexpect binti awe kimyaa na wa kulia Lia tu wakati hajakuzwa hivyo..ama u expect awe mpole wakati by nature upole si tabia yake..kuwa mwanamke nayo ts an art, ts a lifetime process and endless learning...
Mtu miaka hii point of reference yake ni instagram, Facebook, snapchat nk unategemea nini kwake
Tumeyaona ya ufoo saro,waliochomwa moto Arusha,haya ya mwanza,scenario zote unaona mwanaume ameshindwa kubeba lile jambo akaamua kama mbwai iwe mbwaii...
Wanaume ts time to adjust kuwa mabinti wanalelewa tofauti sn sikuiz,and ts not their fault, NI MFUMO...nani sikuhizi haendi shule, nan skuiz hafanyi kazi ama biashara, wanawake wamepanda chati kufanya yale aliokua akifanya mwanaume tu zamani, sasa ts only few women ambao ataweza mheshimu mume inavyostahiki..depending na kama amefunzwa,ana hofu ya Mungu nk otherwise mda mwingine wanawake wanakosea coz hawajui namna gani ya kupatia ama hata kama akipatia mume anaona ts not enough...
Ni mengi ila wanaume kuna ujumbe hapa,MTAUA HADI LINII?..ts high time mjue women are different
Na hiz kelele za 50/50 sijui mtatoka vipi...
Nimekuelewa na upo sahihi! Usisahau mama alikuwa makamu Mwenyekiti wa chama cha wavuvi. Nahisi hata kipato Kilikuwa kikubwa. Age difference ni miaka miwili. Si ajabu hata hiyo Nyumba ni yake! Binti alisema mama alikuwa anamsemea mbofu mbofu baba. Hivi unaweza kujiua kwa kujipiga risasi tatu? Kusema za ukweli mwanamke humuheshimu anayemtoa uhanga na akishatolewa uhanga nje akija ndani utaipata wewe mwanaume.
 
Nilikuwa naplan kununua silaha mwaka huu mwishoni, Daah sister nitaenda jela mie kwa vituko vya hawa viumbe???? Huwa siwezi kujibishana Mara mbili Mara tatu, busara yangu huwa nikuondoka. Eeh mungu nilinde ila silaha lazima niwe nayo for my own security.
 
Back
Top Bottom