Mwanza: Aliyeshusha bei ya mahindi asakamwa

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
14,980
9,873
Sasa hivi ni msimu wa mavuno ya mahindi katika miji ya Guru na Mbarara nchi Uganda. Wafanyabiashara katika miji ya mwanza geita kahama na shinyanga wanafata mahindi nchini uganda na kuwauzia wananchi.

Mfanyabiashara mmoja aliamua kushusha bei ya mahindi ili wananchi wapate unafuu wa maisha cha ajabu viongozi wa jiji la mwanza wamekuwa wakiwasakama wafanyabiashara hao na kuwafungia biashara zao.

Wiki iliyopita katika manispaa ya Ilemela wafanyabiashara wa mahindi walifungiwa biashara zao na kuleta usumbufu kwa wateja.
 
Watu kama hawa wanampa kazi ya ziada bwana polepole,atakuwa kila wakati anawaomba radhi wananchi.
 
Mwanza Ndiko Tamko Lilikotoko Kuwa Wamachinga Ruksa Kuuza Kitu Popote
Naamini Magwangala Ilishindika Lakini Hili La Mahindi Litaondoka Na Mtu
Hivi Mongela Hayupo Hapo Mwanza ?
 
Hee au hao viongoz wana stock zao za nafaka ili walangue jamii kwa bei wanazotaka wao za juu.kanda ya ziwa bwana?
 
Huu sasa ni uenda wazimu mtu anauza mahindi kwa bei nafuu ili wasio na uwezo wapate nafuu halafu jitu kwa utashi tu linazuia yaani huyo kama kweli jpm ni mtumbuamajipu sasa tuone maamuzi magumu
 
serikali haisambazi mahindi iwauzie kwa bei nafuu.
Wanaojitolea kuwaokoa wananchi wanasumbuliwa.
Eee Mungu tusamehe na uturehemu watanzania na viongozi hawa wenye mioyo migumu.
 
!Let's wait and see!
5847fea57afb00623651e949571aef5b.gif
 
Sasa hivi ni msimu wa mavuno ya mahindi katika miji ya Guru na Mbarara nchi Uganda. Wafanyabiashara katika miji ya mwanza geita kahama na shinyanga wanafata mahindi nchini uganda na kuwauzia wananchi.

Mfanyabiashara mmoja aliamua kushusha bei ya mahindi ili wananchi wapate unafuu wa maisha cha ajabu viongozi wa jiji la mwanza wamekuwa wakiwasakama wafanyabiashara hao na kuwafungia biashara zao.

Wiki iliyopita katika manispaa ya Ilemela wafanyabiashara wa mahindi walifungiwa biashara zao na kuleta usumbufu kwa wateja.
Rais fyatua haya majitu,ni kero kwa ustawi wa Watanzania,taifa na chama.
 
Sasa hivi ni msimu wa mavuno ya mahindi katika miji ya Guru na Mbarara nchi Uganda. Wafanyabiashara katika miji ya mwanza geita kahama na shinyanga wanafata mahindi nchini uganda na kuwauzia wananchi.

Mfanyabiashara mmoja aliamua kushusha bei ya mahindi ili wananchi wapate unafuu wa maisha cha ajabu viongozi wa jiji la mwanza wamekuwa wakiwasakama wafanyabiashara hao na kuwafungia biashara zao.

Wiki iliyopita katika manispaa ya Ilemela wafanyabiashara wa mahindi walifungiwa biashara zao na kuleta usumbufu kwa wateja.
Unatumia vibaya sana uhuru uliopewa kuongea uongo.Hivi kweli inawezekana mtu akasakamwa kwa kuuza mahindi wakati bei sokoni inajipandisha na kujishusha yenyewe.Leta ushahidi wa mfanya biashara mmoja tu aliefungiwa
 
Mwaka mzima mnatumbua tu ila tija itokanayo na utumbuaji huo bado haijaonekana!! Wakati watu waliaminishwa kuwa ugumu wa maisha yao chanzo ni hao watumbuliwa!!
Watumbuliwa hawajaisha. Si unasoma hii habari ya viongozi walioota mapembe.
Viongozi wengi wapo kimafia zaidi. Wanalala wakifikiria matumbo yao,siyo habari cjui ya uzalendo, sijui kutumikia wananchi ni hadaa.
 
Kabombe, kulikuwa na roli lenye shehena ya mahindi maeneo ya mwaloni lilikamatwa na kushikiliwa wakitaka nyaraka za kusafirisha na kuuza nafaka huku mmiliki akiwa kaelekea nchini uganda kufata shehena nyingine. Hivyo dalali aliyeachiwa akalazimika kulipia tena upya.

Vipi tuweke kila kitu wazi?
 
Rais alisema wakulima wapandishe bei Mara dufu asiyeweza bei nae akalime. Kwahiyo hao viongozi wanatekeleza Agizo la Rais
 
Username1, uko sahihi ukitizama barabara za kuingia katika masoko ya mwaloni na kilimahewa ni mabovu sana kiasi maroli yenye shehena za mahindi na mchele hayawezi kufika hivyo kulazimika kufaulishwa kwenye mafuso na kuongeza usumbufu
 
Kabombe, kulikuwa na roli lenye shehena ya mahindi maeneo ya mwaloni lilikamatwa na kushikiliwa wakitaka nyaraka za kusafirisha na kuuza nafaka huku mmiliki akiwa kaelekea nchini uganda kufata shehena nyingine. Hivyo dalali aliyeachiwa akalazimika kulipia tena upya.

Vipi tuweke kila kitu wazi?
inamaana Huyo Mfanya Biashara hakujua taratibu na sheria za Nchi? kama kakimbia kwa kuwa anajua hajafata taratibu, hao wasimamizi wangejuaje?
Au ndio zile kasumba za linapo tokea tatizo wengine wakiuke taratibu kwa mgongo wa hilo tatizo? Tufanye kazi tuachane kulalamika hata pale tunapokiuka taratibu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom