Mwanyika siku zake za kazi ofisini zahesabika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanyika siku zake za kazi ofisini zahesabika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Aug 5, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,067
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  Na Leon Bahati

  WAKATI wabunge wakishikilia msimamo wao wa kuitaka serikali iwaadhibishe maafisa wa serikali wanaodaiwa kuhusika katika upitishaji wa zabuni tata ya umeme wa dharura iliyoipitia ushindi Kampuni ya Richmond Develepment (LLC) akiwamo Mwanasheria Mkuu (AG), Johnson Mwanyika, imefahamika kuwa anatarajia (Mwanyika) kustaafu kwa mujibu wa sheria kabla ya mkutano wa Bunge wa 18 utakaofanyika Novemba, mwaka huu kuanza.

  Wiki iliyopita Bunge liliikataa taarifa ya serikali juu ya utekelezaji wa maagizo yake, ambayo iliwasafisha maafisa hao ikisema hawastahili kuchukuliwa hatua.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na tovuti ya Bunge, zimeeleza kwamba Mwanyika anatarajia kustaafu Novemba 6, mwaka huu ikiwa ni siku 21, kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa 18 wa Bunge unaotarajia kuanza Novemba 27.

  Taarifa hizo zimeeleza kwamba ifikapo Novemba 6, mwaka huu, Mwanyika atakuwa amefikisha umri wa miaka 60, umri ambao kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma, anapaswa kustaafu.

  Vilevile, kumbukumbu zilizopatikana kwenye tovuti ya Bunge, zinaonyesha kuwa Mwanyika alizaliwa Septemba 6, 1949, hivyo kumfanya awe amefikisha umri wa miaka 60 ifikapo tarehe sita mwezi ujao.

  Kumbukumbu hizo pia zinaonyesha kwamba, muda wa Mwanyika kuwa kwenye wadhifa huo utaisha Desemba 27, mwakani, siku ambayo inatarajiwa kwamba Uchaguzi Mkuu wa wabunge na rais utakuwa umekamilika.

  Juhudi za Mwananchi za kumpata Mwanyika kuelezea juu ya fununu hizo hazikuzaa matunda baada ya kutopatikana kupitia simu yake ya mkononi.

  Hata hivyo, tulipowasiliana na Ofisa wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Wizara ya Katiba na Sheria, Omega Ngole alisema kuwa hana taarifa zinazohusiana na Mwanyika kustaafu, lakini akabainisha kwamba likitokea hivyo siyo jambo la kushangaza kwa sababu mtumishi yeyote wa umma anapofikisha miaka 60 anaruhusiwa kustaafu kisheria.

  "Mimi niko Dodoma... Sina habari kama hizo. Lakini si ajabu kwa mtumishi yeyote wa umma kufanya hivyo, pindi akifikisha miaka 60," alisema Ngole.

  Ingawa suala hilo linaonekana kuwa la kisheria, lakini vyanzo vyetu vya habari vimesema kustaafu kwake kinaonekana kuelemewa pia na shutuma kutoka kwa wabunge ambao wametishia kuonyesha msimamo wa kutokuwa na imani na serikali.

  Katika mkutano wa Bunge uliomalizika Jumamosi iliyopita, wabunge wengi walionyesha kutoridhishwa na taarifa ya serikali inayoonekana kumsafisha Mwanyika pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah kwa kutowajibika ipasavyo katika mchakato wa zabuni ya Richmond.

  Kutokana na wabunge wengi kushupalia suala hilo, Spika, Samuel Sitta alitangaza msimamo wa Bunge wa kuitaka serikali kutoa maelezo upya juu ya utekelezaji wa maagizo yake kuhusiana na kashfa hiyo ya Richmond.

  Kabla ya wabunge kuichachamalia hoja ya serikali, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shelukindo (Bumbuli-CCM) alisoma taarifa ya kamati yake bungeni akisema kwamba hawakubaliani na ripoti ya serikali.

  Akielezea kuhusu kilichofanyika kwenye kamati hiyo, mmoja wa wajumbe ambao hawakupenda jina lake litajwe gazetini kwa kuwa wao siyo wasemaji aliposema kwa hisia kali:

  "Tunahoji kwamba, hivi kweli mamlaka hizo zimewajibika ipasavyo katika kuchunguza suala hilo; kwani kimazingira tu haiwezekani kuamua kwamba, Dk Hoseah (Edward) ambaye ndiye msimamizi Mkuu wa Takukuru na Mwanyika ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa serikali wawe hawakutenda kosa katika suala hilo."

  Aliongeza: "Sisi tunasema, kama ni kulindana, imetosha, tunahoji na kulazimika kuamini kwamba, ripoti hiyo pengine ina mkono wa viongozi wa juu serikalini".

  Alisema, kama aliyekuwa Waziri Mkuu wakati wa sakata hilo Edward Lowassa na mawaziri Nazir Karamagi (Nishati na Madini) na Ibrahim Msabaha (Afrika Mashariki) walikubali kujiuzulu, lazima kuna watendaji walioboronga katika suala hilo.

  "Kamati sasa tunataka wale waliokuwa wakimsaidia Lowassa wawajibike, iweje Lowassa aone kosa lake na hawa wengine walindwe?” alihoji.

  Ripoti ya serikali ambayo ilipingwa na wabunge, iliishia kwa kumpa onyo Dk Hoseah kwa kutokuwa makini katika utendaji wake wa kazi wakati anachunguza mkataba tata kati ya Kampuni ya Richmond na Tanesco.

  Serikali pia imesema mamlaka yake ya kinidhamu imeona Hoseah hana hatia kijinai kwani sheria ya Takukuru wakati huo, ilikuwa na mapungufu katika kubaini viashiria vya rushwa kwenye mchakato wa zabuni.

  Mbali na Dk Hoseah ripoti ya serikali ilimuelezea Mwanyika kwamba, hakuna ushahidi unaodhihirisha kuwa hakutumia utaalamu na uzoefu wake kuishauri vizuri serikali katika mchakato mzima wa upatikajaji wa zabuni.

  Taarifa hiyo imesema, Mwanyika ambaye mamlaka yake ya nidhamu ni Rais, hakuwa na kosa lolote katika mchakato mzima wa kuipa Kampuni ya Richmond zabuni ya kuzalisha umeme.

  Miongoni mwa wabunge walioishikia bango la kuipinga ripoti hiyo ni Dk Willibrod Slaa (Karatu-Chadema) aliyelalamika kuwa kitendo cha kuwasafisha baadhi ya wahusika sio cha kiungwana, kinarudisha nyuma juhudi za kupambana na mafisadi na kuifanya serikali iwe safi.

  “Hapa tunatakiwa kwenda mbele zaidi hivyo, nasema kuwa ifikapo mwezi Novemba mwaka huu kama serikali haitatoa ufumbuzi wa kina juu ya jambo hili ni lazima ijiuzulu na tuingie kwa wananchi kuomba ridhaa tena katika uchaguzi,” alilalamika Dk Slaa.

  Christopher Ole- Sendeka (Simanjiro-CCM) aliitaka serikali imtaje kigogo anayekwamisha utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu suala hilo la Richmond.

  Ole-Sendeka licha ya kumtetea Rais Jakaya Kikwete kwamba hahusiki na Richmond, aliitaka serikali yake iwe wazi na isimuonee haya mtu.

  Said Nkumba (Sikonge-CCM) alisema kama Rais Kikwete alikubali kujiuzulu kwa Lowasa, alikwisha tambua kuna kosa, hivyo ni lazima na wengine wawajibike.

  Nkumba aliwataka wote wanaotuhumiwa katika sakata hilo wawajibike mara moja kuliko kuendelea kusubiri wawajibishwe na wengine.

  "Ukiona umechafuka kaa utulie, kuliko ukiendelea utachafuka zaidi na ikibidi usitake kuwachafua na wengine, kwani kwa kufanya hivyo unaweza kuchafuka zaidi," alisema Nkumba.

  Nazir Karamagi (Bukoba Vijijini-CCM) alisema kuwa Bunge la Tanzania halijawahi kumuonea mtu katika maamuzi yake na kuitaka serikali isipate kigugumizi katika kutoa maamuzi. "Kama mimi Karamagi nimefanya makosa basi niwajibishwe na ikibidi akaunti zangu zikamatwe kwa uchunguzi ili haki iweze kutendeka na sio kukaa muda mrefu ili kusubiri maamuzi ambayo hayajulikani yatatolewa lini." Alisema
   
 2. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Hata karamagi anashangaa kuona watu waliofaudu kwenye Richmond bado wanadunda wakati wao akina Bangusile wameshatema mzigo. Nakubaliana sana na Karamagi katika hili.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Huko ni kulindana kusiko na msingi
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Rais Kikwete nadhani amekwisha amua kuwa Bunge haliwezi kumchagulia watendaji wake na ndio maana anadharau hayo maazimio ya Bunge; na mimi binafsi ninavyomuelewa Jakaya hatakekeleza hata moja ya maazimio hayo ya Bunge kama alivyopewa altimatum na kikao cha Bunge kilichokwisha. He is bracing himself for a showdown against Sitta na genge lake na hapo ndipo tutakapomuoa ujeuri wa huyu mkwere. Yale matamko ya Luhanjo kuhusu jinsi Jakaya alivyohusika na Richmond ni preamble ya maamuzi yake kuwa hatawafukuza kazi watendaji wa serikali kama Bunge lilivyotaka bali atawaacha wakae mpaka muda wao wa kustaafu utakapofika!! Amefanya hivyo kwa Mgonja na atafanya hivyo hivyo kwa hao wengine.Sasa itakuwa juu ya Bunge kuamua kama wasuke au wanyoe!!!
   
 5. H

  Haruna Malima Member

  #5
  Aug 6, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karamagi anaonyesha ukomavu wake kiutendaji na jinsi alivyo na confidence ya kile alichofanya wakati wa uwaziri wake. nampa shavu! Lakini Kikwete Mmmhhh! Haachi asili.
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hatma ya yote ni Novemba,tutaona meno ya Bunge yaking'ata la sivyo...............
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180

  Kikwete kwa kuwatuma TAKUKURU kwenda kuzichunguza kamati za bunge anajua kule lazima watakuta ubadhilifu na uchafu mwingi wa hali ya juu; nadhani ili kupreempt hatua za kisheria dhidi ya wabunge wahusika atachukua hatua ya kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mkuu prematurely!! The dissolution of parliament will avoid the anticipated clash in November between the Executive and the Legislature; huu ndio utabili wangu.
   
Loading...