Mwantumu Mahiza: Waandishi wa Habari mnaogopesha wawekezaji kuonesha picha za ajali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwantumu Mahiza: Waandishi wa Habari mnaogopesha wawekezaji kuonesha picha za ajali.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mjomba wa taifa, Aug 17, 2012.

 1. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tarehe 15 Agost, 2012 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza ametembelea kituo cha utangazaji cha Radio CLOUDS FM ya Dar es Salaam. Katika mengi aliyoyasema katika tasnia ya habari ni pamoja na kuwaomba waandishi wa habari wasioneshe katika televisheni na wala kuandika katika magazeti habari za ajali za vyombo vya usafiri kwa kuwa habari hizo zinatisha wawekezaji na watalii wasije Tanzania.

  Haya ndio maneno ya Mkuu wa Mkoa wa serikali ya JK, badala ya kuonea huruma maisha ya watanzania kwa kutafuta mbinu za kupunguza ajali yeye anaficha maradhi kwa kuomba wanahabari wasitoe taarifa.

  Kweli!!!!! Zama hizi za kuficha habari??? Aibu.
   
 2. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  tatizo la watu wanaoishi kwa kudra za jk ndo hilo. Hawana kingine cha kufikiria zaidi ya kuficha uovu. Wanashindwa kumwambia bwana wao abanane na mwema ili trafik wafanye kazi yao ya kukagua vyeti vya udereva, kuzuia vipara visitie timu barabarani wao wanataka wananchi tusipate habari. Hayo yaliwezekana enzi za gazeti la habari leo peke yake! Sasa hivi kuna tz daima watu tutalitafuta hadi mapangoni. Kwa akili zao zilivyo matope wanaweza kutunga sheria hiyo.
   
 3. m

  mamajack JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  huyo ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya gani kweli????

  kweli hawa wakuu wa wilaya&mikoa ni mzigo kwa taifa.inabidi waondoshwe mara moja.
   
 4. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Kwa hiyo waripoti nini ufunguzi wa majengo na mbio za mwenge?
   
 5. j

  jiwe gumu Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu kachoka.Vyombo viripoti nini kama siyo pamoja na ajali zinazotumaliza?Umenikumbusha siku mh Lisu alipoomba mwongozo wa naibu spika ili ajali ya meli ijadiliwe,akakataliwa.Kwa CCM ni sawa tu ukiweka picha ya Paris kwamba ndo Dar es Salaam.Kila mwaka wanakuja na takwimu za ukuaji wa uchumi,lakini wananchi tunadidimia kwenye umaskini.Rais ana ndege ya bei mbaya,viongozi wanatumia business class,maisha yao ya kifahari mno.Hee!na ile shule yenye mwalimu mmoja kuanzia chekechea mpaka la saba,mwalimu kawekwa kiti moto.Nafuatilia...
   
 6. Mzalendo2015

  Mzalendo2015 JF-Expert Member

  #6
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 1,954
  Likes Received: 2,313
  Trophy Points: 280
  Huyu RC Mwantumu Mahiza nilimsikia mwenyewe live kwenye Clouds FM akibwabwaja uchuro wake. Nilishangaa sana kwa kauli zake zile. Kweli nilijua Kikwete hana RC mkoa wa Pwani. Pengine ndiyo maana alikosa Ubunge na hatimaye kukosa Uwaziri. Nakumbuka wakti ule huyu mama akiwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, alitoa kauli ambayo Watanzania hasa WAALIMU hawataisahau. Alisema kwamba,kama Waalimu wanataka Mishahara mikubwa WAACHE UALIMU WAKAFANYE KAZI NYINGINE! Huyo alikuwa Waziri Mwantumu Mahiza na sasa RC Mkoa wa Pwani!!

  Ninachotaka kusema kuwa huyu mama ni Mpayukaji na huwa hachagui maneno ya kuongea. Alichoongea kuhusiana na swala la ajali maeneo ya Kibaha-Chalinze juzi kwenye Clouds ni utumbo uleule wa siku zote. Hivi huyu mama anafikiri zikitokea ajali watu wasipige picha za tukio la ajali kweli? Ili iweje? Anataka kuficha nini kwa ajili ya nani hasa? Hata mimi nikiwa kwenye safari nikikuta ajali imetokea sitaacha kuchukua picha! Huyu mama hakuishia hapo alikwenda mbali zaidi na kusema kwamba dereva atakayesababisha ajali kwanza watamtandika makofi halafu ndiyo apelekwe kwenye sheria! Wewe utampigaje mtu makofi wakati sheria zipo? Huyu mama nafikiri anataka kuchochea vurugu kati ya Polisi wa Usalama barabarani na Madereva! Hapa hajatumia busara baali ametumia makalio kufikiri!

  Mawazo ya Mwantumu Mahiza ni mawazo mfu yasiyokubalika!Picha ni muhimu kama kumbukumbu kwa ajili ya ukumbusho wa baadaye.Picha ni sehemu ya kuhabarisha watu. Bila shaka habari bila picha inakuwa haijakamilika.Picha zinatufundisha kuepukana na makosa kama yaliwahi kufanyika au kama ni mema kuyaendeleza.Lakini pia picha zinaweza kuwa ni Ushahidi wa tukio husika kama zinaweza zitahitajika kwenye kesi ya tukio husika.

  Kisingizio cha RC Mwantumu kuwa picha hizi zitaogopesha wawekezaji na Watalii ni upuuzi. Mwantumu Mahiza lazima ajue kuwa kuna ajali kibao zimetokea live mbele ya haohao Watalii au Wawekezaji na hata baadhi yao wamepoteza maisha kwa ajiali hizohizo anazotaka kuwaficha au kuwadanganya Watanzania.

  Watu bado hatujasahau ajali ya juzi tu ya meli ya MV Scagit ambayo imepoteza uhai wa Watanzania wenzetu na watalii kadhaa. Kwa akili ya Mwantumu Mahiza alitaka hiyo ajali isionyeshwe wala kuripotiwa kwenye magazeti kwa njia ya picha. Huu ni ujinga! Hata picha kama hazitapigwa na kupelekwa mitandaoni Watalii na Wawekezaji tayari wanajua ajali za barabarani na majini Tanzania ni sehemu ya maisha!!!!
   
 7. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #7
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Hivi JK alitoa wapi watu dizaini hii?
   
 8. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #8
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,682
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Huyo Mwantumu ni mwongo, siku wakenya walipopata ajali mkoani kwake nilimuona muhimbili anakimbia huko na huku akijipitisha pitisha mbele ya maofisa wa ubalozi wa kenya na kujifanya kutoa maelekezo hata kwa shughuli zilizokuwa hazimhusu. Mnafiki mkubwa huyo dada.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Aug 17, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Good question. Ndiyo dizaini yake mwenyewe JK
   
 10. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #10
  Aug 17, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Duh!Halafu huyo ndo mwenyekiti wa ulinzi na usalama katika mkoa wake,kwake waekezaji na watalii ndo muhimu kazi tunayo.
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Aug 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Unategemea nini toka kwa makada wanaopewa post kulipa fadhila, ushikaji na urafiki. Mimi sishangai hao ndo wasaidizi wa JK.
   
 12. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2012
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Mkuu huyu mama si tatizo; naye ni mhanga wa mfumo anaoutumikia. Ukisema JK kamtoa wapi itakuwa kama vile unamuona JK mtu wa maana sana lakini kakosea kumchagua "mtu mbovu". Mimi binafsi pamoja na kero zote nilizonazo jinsi serikali ya CCM inavyoendesha nchi, huyo mama namuona kama mtu makini zaidi na mwenye dhamira njema katika kazi zake. Anaweza kuwa na upungufu wa uwezo lakini anajituma sana kwenye masuala ya wanyonge na humsikii akitoa kauli mbovu kushambulia wapinzani tofauti na wengine waliokalia ushabiki wa kisisasa tu. Kauli hiyo amekosea lakini si mtu wa kumtosa sana.
   
 13. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #13
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,843
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Nilimsikia Akilaumu watu wanaopiga picha kwenye Matukio ya ajali Kweli nilimshangaa sana!! Alikuwa anasisitiza umuhimu wa Kuokoa! Hili ni sawa ila kwenye Uokozi lazima uwe na Vifaa!! Na pia Habari kwa zama hizi huwa zinasambaa haraka ili kuweza kuwapa ndugu na Jamaa habari za Tukio Baya na Msaada wa Haraka!! "Ogopa mwanamke Anayetumia Masaa mawili (2hrs) Kupaka Wanja na kujichubua in the Age of 50 plus!! Ni Hasara Tupu@"
   
 14. ruhi

  ruhi JF-Expert Member

  #14
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 1,409
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  kazi kwelikweli
   
 15. k

  kisimani JF-Expert Member

  #15
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Huyu mama kweli hamnazo, yani anafikiri ni kumsaidia mtanzania kuficha ajali...ni bora wajue, tukose watalii na wawekezaji ili tuunde namna ya mpya na sahihi ya kuendesha hivi vyombo. Tatizo la kufikiri kwa urefu wa pua ndio hilo, unaona vya karibu tuu.
   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Haya ndiyo mawazo ya watu wanaopewa dhamana, yaani funikafunika. Badala ya kupigia kelele kuongeza umakini wa usimamizi wa sheria wa sheria ili kuepusha ajali yeye anataka ajali zisitangzwe. Haya ni mawazo ya failed leader, yaani hana jipya na hajui nini cha kufanya kuondoa tatizo, njia pekee anayoona ni kulipuuzia tatizo hilo kwa kulifunika na magunia lisionekane kama lipo.

  Statements kama hizi katika nchi za demokrasia zinatosha kumfanya mtu ajiuzulu uongozi kwa kuwa ameshindwa. Hawa watu wanakubali kuwa wameshindwa ila hawataki kuwaacha watanzania wachague watu wengine ambao wanaweza, wanang'ang'ania nyadhifa zilizo juu ya uwezo wao wa kufikiri.
   
 17. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #17
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  HII hainipi shaka kwamba hata mtoto wangu wa miaka 13 ana uwezi kwa kuwa kiongozi ktk serikali hii ya leo! na pia anaweza kuwapita kimawazo viongozi wengi tu kama huyu!
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Aug 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nadhani hapa kuna maelekezo maalum kutoka kwa mamlaka za juu za nchi. Mkuu wa mkoa anataka matukio ya ajali yasionyeshwe ama kutangazwa na vyombo vya habari ili kutowatisha wawekezaji, kwakuwa wao ni muhimu zaidi kuliko uhai wa watanzania.
  Si ajabu SUMATRA nao katika kutekeleza maagizo hayo wamekurupuka kulazimisha watu kuwa na vitambulisho wakati wanaposafiri kati ya Dsm na Zanzibar ili wakifa majini watambulike, badala ya kuhakikisha kwamba vyombo vya majini ambavyo ni vibovu na havina ubora wa kutoa huduma ya usafiri majini vinasimamishwa ama kukfanyiwa matengenezo muhimu ili kukidhi viwango vya ubora unaotakiwa.
   
 19. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #19
  Aug 17, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Mimi nilimwelewa vingine huyu mama(kama alikuwa na maana hiyo). Nilichoelewa mimi ni kuwa wakati ajali inapotokea, baadhi ya wananchi hawajihusishi na kuokoa wahanga bali wanakuwa bize kupiga picha za tukio kwa kutumia simu zao na kuwaacha wahanga wakifa bila msaada wowote (endapo wamebanwa na viti ndani ya gari)! Picha hizo ambao zingine hazifai kuonyeshwa kwa wananchi kutokana na utamaduni wetu, utazikuta kwenye Blog mbalimbali eti ni Breaking news!
   
 20. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #20
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Wanalipana fadhila na wanajua kuwa wa Tanzania ni waoga,mbumbumbu na wasiojua haki zao!!
   
Loading...