Mwantumu Mahiza uliwaletea nyodo waalimu na wewe sasa nje! Subiri 2015


kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
22
Points
135
Age
42

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 22 135
MATOKEO ya Uchaguzi Mkuu ulioanza katika ngazi ya vyama kwa kura za maoni katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), yamewaondoa mawaziri 10 katika nafasi za ubunge ambazo ndio kigezo cha kuteuliwa katika wadhifa wanaomaliza kuutumikia.

Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Philip Marmo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Batilda Burian ambao wamepoteza nafasi hizo baada ya kushindwa na wagombea wa vyama vya upinzani.

Wengine ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala na Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mangunga ambao wamepoteza nafasi hizo wakati wa mchakato wa kura za maoni za kuwapata wagombea ubunge wa CCM.

Mbali na mawaziri hao kamili, wapo manaibu waziri watano, akiwemo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk James Wanyancha na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda ambao wote walipoteza nafasi hiyo katika kura za maoni.

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omar Yussuf Mzee yeye amepoteza nafasi hiyo baada ya kufanya uamuzi wa kutogombea nafasi yoyote ya kisiasa.

Baraza la mawaziri linalomaliza muda wake linakuwa na mawaziri 48 na kati ya hao mawaziri kamili ni 27 na manaibu wao 21.

Wakati huohuo, matokeo ya uchaguzi katika majimbo ya Segerea, Ukonga na Ilala yalitangazwa juzi usiku, CCM ilishinda katika majimbo yote.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Makongoro Mahanga kutangazwa Mbunge mteule wa Jimbo la Segerea.

Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi katika majimbo hayo, Gabriel Fuime alianza kutangaza Jimbo la Ilala saa tano usiku wa kuamkia jana, ambapo Musa Zungu alishinda kwa kura 25,940 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema, Naomi Kaihula aliyepata kura 5,053.

Katika jimbo hilo wagombea wengine ni Asia Hussein wa NLD (157), Juventina Ching’ande wa NRA (34), Ngowi Alfayo wa SAU (29), Asifiwe Mwakalinga wa UDPD (50), Juma Khamis wa UMD (51) na wengine.

Katika Jimbo la Ukonga lililotangazwa saa 7:25 usiku, mgombea wa CCM Eugen Mwaiposa alishinda kwa kura 28,000 na kumshinda mgombea wa Chadema, Binagi Chacha (17,059), Heko Pori 5,220 na wengineo.

Matokeo ya Segerea, yalitangazwa saa 8:45 usiku ambapo Mahanga wa CCM alishinda kwa kupata kura 43,554 na kufuatiwa na mgombea wa Chadema, Fred Mpendazoe kwa kura 39,150.

Wengine ni Kimangale Musa wa CUF (18,737), Martha Ndaki wa APPT Maendeleo (419), Yusuf Salum wa SAU (288), Asia Chale wa Jahazi (220) na wengineo.
 

Forum statistics

Threads 1,204,071
Members 457,119
Posts 28,140,165