Mwanri [naibu TAMISEMI] ampiga stop Masaburi kuvunja bodi ya DDC

Papa D

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
753
182
Ofisi ya Waziri mkuu imezuia agizo/Tangazo la meya wa Dar kuvunja bodi ya Wakurugenzi wa DDC kwa madai kuwa hana mamlaka hayo kisheria. Awali Masaburi aliivunja ili kupisha uchunguzi wa ufujaji wa mali za DDC.

Source TBC1

Je, Masaburi hakujua mipaka yake kuhusu hilo?
Je, zuio la Ofisi ya waziri mkuu lina huo ulazima katika kufanikisha uchunguzi?

Kwa misingi wa utawala bora, nilitegemea Dr Masaburi awekwe pembeni ili kupisha uchunguzi 'huru'.

Masaburi sasa hivi yupo na watendaji wote na madiwani wa dsm court yard hotel upanga anawapa dinner buffer baada ya kikao kirefu. Hii movie tamu na masteling wote ni wa ukweli

kuna mengi sana yamejificha katika sakata hili. Hata huyu nae aliyesema Masabuli hana mamlaka nae kuna watu wake anataka kuwalinda was4aibike

Ukweli ni kwamba, there is a lot at stake here. Kuna credibility za Wabunge na madiwani wa CCM, kina Idd Simba, Kisena ,Riz1, Kapuya etc. No wonder kuna sarakasi za hapa na pale. Kama wananchi hawatakuwa imara kudai ukweli, hili jambo litapita bure.

Kama ni movie basi hii ni treller. Hata mtoto wa mkulima hana mamlaka kisheria kupinga maamuzi ya meya. Hahahaaaah!

Ofisi ya Waziri mkuu imezuia agizo/Tangazo la meya wa Dar kuvunja bodi ya Wakurugenzi wa DDC kwa madai kuwa hana mamlaka hayo kisheria. Awali Masaburi aliivunja ili kupisha uchunguzi wa ufujaji wa mali za DDC.

Source TBC1

Je, Masaburi hakujua mipaka yake kuhusu hilo?

Je, zuio la Ofisi ya waziri mkuu lina huo ulazima katika kufanikisha uchunguzi?

Kama lingekuwa ni tukio la kwanza kwa masaburi kuvunja baraza lililo chini yake, ningemuelewa kidooogo mwanri, mpaka sasa mwanri amebeba bango lililo andikwa maneno ya masaburi (wabunge wa d.... wanafikiri kwa kutumia m.a..kal.i..o!) ameshindwa kuonyesha kwa vitendo kuwa anatumia ubongo kufikiri.

hao wanacheleweshwa sana, walipaswa wawe wameshaanza kuwajibishwa, lakini tumezoea kila kitu kiundiwe tume, na tume kuundiwa tume, lakini majibu yasiatikane. tujiulize kwanini alivunja bodi hiyo muda muu? je aliona tatizo hilo kabla halijafika Bungeni?

Kila siku linaibuka jipya Tuliyotegemea yashakuwa atatokea wa kumpinga Meya kwa maamuzi ya kuvunja bodi ya ddc, soon utasikia atakuja wa kumpinga kauli ya office ya waziri mkuu.. mwisho yatajichuja yote tutajua mwenye nchi ni yule mwenye mdomo mrefu na pumba ni nani serilaki hii hakuna mkubwa wa mwenzie.

hao wanacheleweshwa sana, walipaswa wawe wameshaanza kuwajibishwa, lakini tumezoea kila kitu kiundiwe tume, na tume kuundiwa tume, lakini majibu yasiatikane. tujiulize kwanini alivunja bodi hiyo muda muu? je aliona tatizo hilo kabla halijafika Bungeni?
Mkuu kwa mwaka unachangia post ngapi duh! Join 2008 Post 7? Yahoo watakuwa washakudelete!

Mambo haya ni kale kamchezo ukimwaga Mboga na mimi namwaga Ugali Tulia tu Sie Tunatizama Movie la Faida na Ndio kwanza limeanza

Bora Rostam ameacha siasa Uchwala... Pangu pakavu

Masaburi nae anatumia makalio kutoa maamuzibya kuvuta bodi? Ina maana alikua hajui kua hana mamlaka kisheria

Hayo ndo matokeo yakuwa na Serikali legelege sasa hawa watendaji wa serikali wanapopingana wao kwa wao Wananchi tuwaelewe vipi!!Huyu Meya anakashifa tayari kwanini asisimamishwe uchunguzi ufanyike?

On my side namuona kama mpambanaji japo hili la UDA linamtia doa kidogo jinsi alivyolipeleka faster,lakini haiwezi kujustify kuwa UDA was clean before Masaburi.

Tumuunge mkono Masaburi ana dhamira ya kweli,na kelele nyingi anazopigiwa ni za kumtaka asiwafikie huko kwenye maslahi yao na madudu waliyofanya.

Hayo ndo matokeo yakuwa na Serikali legelege sasa hawa watendaji wa serikali wanapopingana wao kwa wao Wananchi tuwaelewe vipi!!Huyu Meya anakashifa tayari kwanini asisimamishwe uchunguzi ufanyik
e?

Kashfa ya Meya ni ipi? Mbali na so called kukiuka taratibu za kisheria kuna kipi kingine?Tuache tabia za kudandia mambo, hiyo UDA imeanza kufa leo?je tunaweza kulinganisha hujuma kubwa zilizofanywa kwa mali za jiji la Dar es salaam na haya anayofanya Masaburi.

Kosa la kisheria kila mtu anaweza kulifanya na sishangai haya kutokea Jiji la Dar es Salaam kwani hata waliokuwepo aidha bodi zao ama viongozi nao wapo kinyume cha sheria.Kumbuka kamati ya Mheshimiwa Zitto ilivyotimua Bodi isiyo ya kisheria ya soko la Kariakoo.

Turuhusu vichwa vyetu vifanye kazi badala ya kuzibwa na mawazo potofu,kisa sauti kubwa ya kuuzwa kwa UDA ndiyo imeingia katika vichwa vyetu na kufuta mabaya yote iliyotendewa UDA kabla ya kuuzwa.

Back
Top Bottom