Mwani Pemba wadaiwa kuuzwa kwa kujuana

G-Mdadisi

Senior Member
Feb 15, 2018
157
99
KAMPUNI zinazo nunua zao la mwani kisiwani Pemba zimelalamikiwa na wakulima wa zao hilo wakidai zinanunua mwani kwa ubaguzi hali inayosababisha mwani kurundikana majumbani kwa kukosa soko.


Hayo yamebainishwa na wakulima wa mwani wa wadi ya Tumbe kwanye mkutano wa kusikillza kelo za wananchi ulioitishwa na diwani wa wadi hiyo.


Wamesema pamoja na juhudi wanazo zifanya za kujukwamua na maisha kupitia kilimo cha mwani lakini changamoto kubwa ilio jitokeza ni kwa kampuni hizo kununua zao hilo kwa mtindo wa ubaguzi


Sheha wa shehia ya Tumbe Magharibi Massoud Hamad Khamis amesema muda si mrefu changamoto ya soko la zao la mwani itapatiwa ufumbuzi kwani serikali ipo mbioni kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha mwani katika eneo la Chamanangwe Wilaya ya Wete.


Akijibu malalamiko hayo Diwani wa Wadi ya Tumbe Mhe Ali Juma Shaib amezitaka kampuni zinazonunua mwani kwa wakulima kufuata taratibu zilizopo kwa kujiepusha na ubaguzi katika ununuzi wa zao hilo

#UGATvFurahaYako


 
Back
Top Bottom