Mwangwi wa "Travel Ban" na Ubeberu wa Marekani

chagonjam

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
354
418
Nimefuatilia kwa ukaribu mwelekeo wa sera za Marekani hususan kuanza kuweka vikwazo kwa wanasiasa/viongozi wa Tanzania kutemebela nchi yao na kupiga marufuku WATZ kuomba green card kwa njia ya bahati nasibu.

kuna uwezekano mkubwa wa watu wengine kuendelea kuongezwa kwenye Orodha ya kuzuiwa kuingia Marekani. Wachambuzi wa mambo wanaona anayelengwa hapo ni Rais wetu mpendwa JPM.

Tukio la hivi karibuni la Zitto Kabwe kuwakuwadia mabeberu ili Benki ya Dunia isitoe mkopo wa masharti nafuu kwa Tanzania wa USD 500 Milioni na mjadala wa hoja bungeni iliyotolewa na Dr. Mollel. Hoja ni usaliti kwa nchi yetu na ukuwadi kwa mabeberu.

Sasa ona video hii ndiyo ujue kuwa wamarekani hawana wazo lolote la kutetea haki za binadamu isipokuwa maslahi yao tu.
 
Mi niko nyuma kdg, ila ningependa kujua huyo unaemsema kuwadi,
Hasa... Aliwaambia nn mabeberu? chagonjam

Sent using Redmi Y2
 
Issue ni uzalendo kwa nchi yako kwanza. Tupingane kwa hoja humu ndani. Kupeleka taarifa kwa mataifa ya nje ni usaliti
 
Nimefuatilia kwa ukaribu mwelekeo wa sera za Marekani hususan kuanza kuweka vikwazo kwa wanasiasa/viongozi wa Tanzania kutemebela nchi yao na kupiga marufuku WATZ kuomba green card kwa njia ya bahati nasibu.

kuna uwezekano mkubwa wa watu wengine kuendelea kuongezwa kwenye Orodha ya kuzuiwa kuingia Marekani. Wachambuzi wa mambo wanaona anayelengwa hapo ni Rais wetu mpendwa JPM.

Tukio la hivi karibuni la Zitto Kabwe kuwakuwadia mabeberu ili Benki ya Dunia isitoe mkopo wa masharti nafuu kwa Tanzania wa USD 500 Milioni na mjadala wa hoja bungeni iliyotolewa na Dr. Mollel. Hoja ni usaliti kwa nchi yetu na ukuwadi kwa mabeberu.

Sasa ona video hii ndiyo ujue kuwa wamarekani hawana wazo lolote la kutetea haki za binadamu isipokuwa maslahi yao tu.
View attachment 1346380
ila huo ndio ukweli wenyee basi tu
 
Ila watawala kufanya mambo kibabe ndio uzalendo. ? .

Zitto amehoji Sera na mkakati wa serikali juu ya usimamizi na utekelezaji wa huo mradi wa watoto walioacha shule ni upi. ?

Shule hizi za kawaida uendeshaji umekua ni wa hovyohovyo tuuu, leo hiii tuna watoto kadhaa wameshindwa kuanza sekondari kwa kukosa madarasa !!.ikiwa haya tuuu yana washinda huo mradi mwingine watauweza. ? .

Ilisemwa kua hoja ni utawala wa jiwe kutosomesha wazazi japo ilikua kwenye ilani ya ccm . je hata hizo nduruuu za waitwao"mabeberu "nazo zinawama nini zikienda kusomesha hao watoto kwa mfumo huu huu wa sasa. ?

Ujima wa kifkra utaliangamiza hili taifa
Issue ni uzalendo kwa nchi yako kwanza. Tupingane kwa hoja humu ndani. Kupeleka taarifa kwa mataifa ya nje ni usaliti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom