Mwanguko wa kura za Kikwete (2005 to 2010) ni ashirio mbaya kwa Magufuli!

Laiti ungelijua form four kiswahili nilipata nini ungebana na masikio yako!

You see yale yale...lait ungelijua nilipata ngapi kiswahili form four, ungeziba mdomo wako.

Neno "ungebana" halitumiki hivyo. Pia ungebana masikio yako na sio ungebana na masikio yako.
 
Sentensi yako inashangaza. "na" is as "and", sasa unaposema "ungebana na" its like saying shut your "ears and" what by the way? Ningebana masikio yangu na macho or mdomo? I post and you shouldn't under no circumstance ask me to "ningebana masikio"

Your choice of words is terribly weird. Ningebana masikio! Funga or ziba.
 
JK mwaka wa 2005 alipata karibu 82% lakini mwaka 2010 alipata karibu 61% likiwa ni anguko la 21%.

JPM mwaka 2015 alipata takribani 56% kwa kuangaliza anguko la JK kwa 21% basi JPM uchaguzi ujao yaani 2020 kuambulia 35%.

Kama upinzani kura zao zote wataziweka kapu moja basi hakuna jinsi mgombea wao wa UKAWA ataibuka kidedea kwa 65%.

Na jinsi uchumi unavyozidi kudorora na wapigakura wengi kuisoma namba vilivyo huku watawala hawana majibu zaidi ya kudai tunaolalama ni wapiga dili wakati kama dili zilikuwepo wachoraji ni wao basi tegemea hata hiyo 35% kushuka chini ya 30%.

Nyerere mwaka 1981 baada ya kuona kila mtu analia na ugumu wa maisha hakutulaumu bali alikuja na kauli za matumaini akiwa Kigoma alisema yafuatayo......" ....tusikubali kugeuka kuwa jiwe....na tufunge mikanda kwa miezi kumi na nane."

Ulikuwa ni utapeli wa kisiasa lakini ulimsaidia kumaliza ngwe yake ya mwisho bila vurugu na akasoma alama za wakati na kubwaga manyanga hapo 1985.

Kuwalaumu wapigakura na kuwaita wapiga dili ni kuwatusi na kukosa majibu ya kero za kiuchumi ni kuwafyagilia wapinzani wako na kujiandaa kisaikolojia kuwakabidhi dola kiulaini kabisa.

Ruta uko sahihi. Hata hivyo lazima tukubaliane kuwa upinzani wana kazi kubwa ya kuiondoa CCM madarakani. Kumbuka CCM ina wabunge zaidi ya 250 katka bunge la JMT. Na hhii ndio nguvu kubwa ya CCM.

Ni dhahiri CCM wameshidwa kuingoza nchi kuelekea kwenye maendeleo endelevu; na hawataweza kamwe kwa sababu kuibakisha nchi kwenye umaskini ni sehemu ya utamaduni wao. Pia tukumbuke kuwa umaskini na ujinga wa Watanzania walio wengi ndivyo mtaji mkubwa wa CCM wa kisiasa. Hivyo chini ya utawala wa CCM Watanzania wasahau kupiga hatua yoyote mbele kimaendeleo. Haishangazi kuwa sasa ni karibu miaka 60 tangu Tanzania ipate uhuru lakini zaidi ya 75% ya wananchi wanaishi kwa kipato cha dola moja kwa siku!

Sera za CCM zimeshindwa katika elimu, afya, kilimo, ajira, mipango miji, ukusanyaji kodi, maendeleo ya miundombinu, kuleta usawa wa kiuchumi na kijamii na katika usimamizi wa uchumi kwa ujumla. Kwa lugha nyingine, sera za CCM zimefanikiwa tu katika kuwaongezea Watanzania umaskini na ujinga.

Lakini kuchemsha kwa CCM pekee hakuwapi wapinzani unafuu wa kisiasa (political leverage) au hata uhalali wa kuchukua nchi. Ni lazima waje na ajenda, dira, maono na sera mbadala na wavitangaze (articulate and propagate) nchi nzima na ujumbe wao uwafikie Watanzania wote. (Hapa wasije na visingizio vya kukatazwa mikutano ya hadhara). Wakifanya hivyo watashinda uchaguzi wowote kirahisi chini ya tume hii hii ya uchaguzi na kwa katiba hii hii iliyopo.

Madhalan, Chadema wana nini mbadala cha kutueleza kuhusu elimu, sekta muhimu sana ambayo imetelekezwa na CCM, kwa upande mmoja, na mfuno mbovu wa kodi nchini, kwa upande mwingine? Kwa mfano, wakati nchi karibu zote za Ulaya (na za Asia zinazoinukia kiuchumi) zinatumia 4% ya pato la taifa (CDP) katka elimu, Tanzania inatumia chini ya 0.2% ya GDP katika elimu. Lakini pia Tanzania inakusanya 11% tu ya GDP kama mapato ya kodi kiasi ambacho ni kidogo kuliko cha nchi zote duniani zinazotegemea kujiendesha kwa mapato ya kodi! Ikumbukwe hapa kuwa bajeti na mipango yoyote ya serikali ya maendeleo vitakuwa ni ulaghai mtupu kama ukusanyaji wa kodi ni chini ya 25% ya GDP. Serikali ya CCM imeshindwa kurasimisha sehemu kubwa ya shughuli za kiuchumi nchini ambazo zingekuwa ni vyanzo vya mapato ya serikali. Ubunifu wa serikali ya awamu ya tano katika kupanua wigo wa mapato ya kodi umeishia katika kuwatuma askari polisi barabarani 'kukusanya mapato!! Je Chadema wana nini mbadala cha kutueleza kuhusu haya? Mbona hawasemi?

Kwa upande mwingine, ni lazima wanasiasa wapinzani wajitofautishe kitabia na kimwelekeo na wale wa CCM ili wananchi wawe na imani nao. (Ni bahati mbaya sana siasa hapa nchini imefanywa biashara na njia ya kupatia fursa za kiuchumi. Na hii ni kwa wanasiasa wote, upinzani na CCM, kitu ambacho kinawafanya wasionekane tofauti). Pia ni lazima kuwe na demokrasia ya kweli katika vyama vya upinzani ili tuone tofauti na madudu yanayofanywa na CCM. Na mwishowe ni lazima vyama vya upinzani viendeshwe kwa sera zenye misingi ya itikadi zao na sio kujikita katika matukio.
 
Ingelikuwa hivyo leo wasingekataza maandamano au mikutano ya siasa ni kwa sababu ghala liko tupu
Unafanya kosa kubwa kabisa wanalofanya wapinzani wa CCM! Kutojua kuwa ghala haliishiwi hata kidogo wakati wa uchaguzi. Tuombe Mungu uzima ufike wakati wa uchaguzi uone jinsi watanzania walivyo na memory fupi.
 
kwani mitandao yaa kijamii ndio inayoamua ?unadhani ccm ni rigid?ccm inaevoleve ....inabadilika kulingana na mazin****...unategemea hoja za kkitoto kama za kwako zitaiangisha ccm eti kwa sababu zinatolewa kupitia mitandao ya kijamii?kumbuka kuwa humu humu kwenye mitandaao ya kijamii zipo hoja mujarabu za wanaccm na zitakazo toa muelekeo wa nchi,
Ingelikuwa inabadilika hali ya uchumi ingelikuwa shwari kabisa
 
You see yale yale...lait ungelijua nilipata ngapi kiswahili form four, ungeziba mdomo wako.

Neno "ungebana" halitumiki hivyo. Pia ungebana masikio yako na sio ungebana na masikio yako.
Lini utaanza kupangua hoja au ni.mlima Kilimanjaro hazipanguliki?
 
Sentensi yako inashangaza. "na" is as "and", sasa unaposema "ungebana na" its like saying shut your "ears and" what by the way? Ningebana masikio yangu na macho or mdomo? I post and you shouldn't under no circumstance ask me to "ningebana masikio"

Your choice of words is terribly weird. Ningebana masikio! Funga or ziba.
Huu mchepuko unathibitisha nimekutoa Mike Tyson knock out. Hili sumbwi limekulaza chali hujitambui na umehesabiwa kumi bado unagalagala
 
Ruta uko sahihi. Hata hivyo lazima tukubaliane kuwa upinzani wana kazi kubwa ya kuiondoa CCM madarakani. Kumbuka CCM ina wabunge zaidi ya 250 katka bunge la JMT. Na hhii ndio nguvu kubwa ya CCM.

Ni dhahiri CCM wameshidwa kuingoza nchi kuelekea kwenye maendeleo endelevu; na hawataweza kamwe kwa sababu kuibakisha nchi kwenye umaskini ni sehemu ya utamaduni wao. Pia tukumbuke kuwa umaskini na ujinga wa Watanzania walio wengi ndivyo mtaji mkubwa wa CCM wa kisiasa. Hivyo chini ya utawala wa CCM Watanzania wasahau kupiga hatua yoyote mbele kimaendeleo. Haishangazi kuwa sasa ni karibu miaka 60 tangu Tanzania ipate uhuru lakini zaidi ya 75% ya wananchi wanaishi kwa kipato cha dola moja kwa siku!

Sera za CCM zimeshindwa katika elimu, afya, kilimo, ajira, mipango miji, ukusanyaji kodi, maendeleo ya miundombinu, kuleta usawa wa kiuchumi na kijamii na katika usimamizi wa uchumi kwa ujumla. Kwa lugha nyingine, sera za CCM zimefanikiwa tu katika kuwaongezea Watanzania umaskini na ujinga.

Lakini kuchemsha kwa CCM pekee hakuwapi wapinzani unafuu wa kisiasa (political leverage) au hata uhalali wa kuchukua nchi. Ni lazima waje na ajenda, dira, maono na sera mbadala na wavitangaze (articulate and propagate) nchi nzima na ujumbe wao uwafikie Watanzania wote. (Hapa wasije na visingizio vya kukatazwa mikutano ya hadhara). Wakifanya hivyo watashinda uchaguzi wowote kirahisi chini ya tume hii hii ya uchaguzi na kwa katiba hii hii iliyopo.

Madhalan, Chadema wana nini mbadala cha kutueleza kuhusu elimu, sekta muhimu sana ambayo imetelekezwa na CCM, kwa upande mmoja, na mfuno mbovu wa kodi nchini, kwa upande mwingine? Kwa mfano, wakati nchi karibu zote za Ulaya (na za Asia zinazoinukia kiuchumi) zinatumia 4% ya pato la taifa (CDP) katka elimu, Tanzania inatumia chini ya 0.2% ya GDP katika elimu. Lakini pia Tanzania inakusanya 11% tu ya GDP kama mapato ya kodi kiasi ambacho ni kidogo kuliko cha nchi zote duniani zinazotegemea kujiendesha kwa mapato ya kodi! Ikumbukwe hapa kuwa bajeti na mipango yoyote ya serikali ya maendeleo vitakuwa ni ulaghai mtupu kama ukusanyaji wa kodi ni chini ya 25% ya GDP. Serikali ya CCM imeshindwa kurasimisha sehemu kubwa ya shughuli za kiuchumi nchini ambazo zingekuwa ni vyanzo vya mapato ya serikali. Ubunifu wa serikali ya awamu ya tano katika kupanua wigo wa mapato ya kodi umeishia katika kuwatuma askari polisi barabarani 'kukusanya mapato!! Je Chadema wana nini mbadala cha kutueleza kuhusu haya? Mbona hawasemi?

Kwa upande mwingine, ni lazima wanasiasa wapinzani wajitofautishe kitabia na kimwelekeo na wale wa CCM ili wananchi wawe na imani nao. (Ni bahati mbaya sana siasa hapa nchini imefanywa biashara na njia ya kupatia fursa za kiuchumi. Na hii ni kwa wanasiasa wote, upinzani na CCM, kitu ambacho kinawafanya wasionekane tofauti). Pia ni lazima kuwe na demokrasia ya kweli katika vyama vya upinzani ili tuone tofauti na madudu yanayofanywa na CCM. Na mwishowe ni lazima vyama vya upinzani viendeshwe kwa sera zenye misingi ya itikadi zao na sio kujikita katika matukio.
Ubunge CCM wataendelea kutesa kwa sababu ya nguvu ya pesa ingawaje idadi yao itaendelea kuporomoka.

Urais watautema tu ufahamu wa wapigakura ni mkubwa
 
Wako na uhakika wa ushindi hawajali nini wanafanya na hawako pale kumfurahisha mtu,

Wananchi msikae mkawaza kwamba mtaigaiwa serikali kwa makaratasi ya kura

Hayo mawazo msiyapatanishe na akili kabisa yani hao waanze kuisoma namba kidandara dandara tu kwa wewe mwananchi kupiga kura?

Kura zote mpeni ukawa lakini rais wenu yuko ccm

Wananchi tufike mahali tukubali kufa watu elfu tano ili milioni 50 waishi maisha ya wanayoyataka iyo tu ndio inaweza kuwa njia sahihi ila sio kuiwaza kura
Tuko utumwani bado na zaidi ni utumwa wa fikra kwa mwendo huu labda vizazi vyetu ndio huenda vikashuhudia mabadiliko yani ccm kutoka kwenye kiti
 
Rutashubanyuma said:
Lini utaanza kupangua hoja au ni.mlima Kilimanjaro hazipanguliki?

Tujadili nini na kwa lugha ipi? Kiswahili chako kibovu mno uko bize kukopi words kwenye kamusi most of which are out of use.

English ni vilevile, you are not that good grammatically kama walivyo Wakenya wengi. Copying words from dictionaries wakati hujui hayo maneno are no longer in use ni umbulula na ujinga wa Kikenyakenya. Screw you!
 
Ubunge CCM wataendelea kutesa kwa sababu ya nguvu ya pesa ingawaje idadi yao itaendelea kuporomoka.

Urais watautema tu ufahamu wa wapigakura ni mkubwa

Hata siasa ujui.

Wapi umeona 97% idadi ya wabunge toka chama kimoja na 3% idadi ya wabunge toka vyama upinzani wakatoa Rais? Hataikitokea hivyo ataachia madaraka soon.

Idadi kubwa ya wabunge ndio watakaotoa Spika wa bunge na kwa idadi hiyo hiyo wanaweza kuvote kutokua na imani na Rais na kumtoa.

Huna hoja, pia si muelewa wa mambo ni mpayukaji usiye na uelewa wa Siasa. SIASA miaka yetu ilikua ni somo la lazima mpaka lilipobadilishwa na kua URAIA.

Nenda kwa Wakenya wenzako mjadili extrajudicial killings zinazoendelea huko kabla ya uchaguzi.
 
Ubunge CCM wataendelea kutesa kwa sababu ya nguvu ya pesa ingawaje idadi yao itaendelea kuporomoka.

Urais watautema tu ufahamu wa wapigakura ni mkubwa

Ni kweli upinzani unaweza kabisa kushinda urais kwenye sanduku la kura. Lakini swali ni je, kuna uwazi kiasi gani lkatika hatua ya kujumlisha kura za urais ili kuhakikisha anayeshinda kwenye sanduku la kura ndiye anayetangazwa mshindi? Jibu ni: hakuna uwazi; na kutokuwepo uwazi si kwa bahati mbaya. Lengo la kukosekana kwa uwazi ni kuficha udangayifu wakati wa kuhesabu kura.

Mwaka juzi Ukawa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) walianzisha vituo vyao vya kujumlisha kura za urais lakini vikasambaratishwa na polisi na maofisa wao kukamatwa. Kimantiki, Ukawa na LHRC walilazimika kuanzisha vituo hivyo kwa sababu wasingeshirikishwa kikamilifu katika mfumo wa kuhesabu kura wa Tume ya Uchaguzi (NEC).

Moja kati ya njia zinazotumika sana siku hizi kuiba kura ni kuchezea (crack) software inayotumika kujumlisha kura ili itoe mshindi anayetakiwa na watawala. Mtu yeyote mwenye ujuzi wa hacking au reverse engineering anaweza kufanikisha 'goli la mkono' kwa njia hii. Na hii inaweza kufanyika bila hata "Mzee Lubuva" kuwa na habari. Mwisho wa siku wapinzani watalalamika tu kuwa wameporwa ushindi lakini hawatakuwa na ushahidi kwa sababu wataalam wao wa IT hawakupata fursa ya kukagua mfumo wa kujumlisha kura na pia hawakushirikishwa katika mchakato wenyewe wa kujumlisha kura.

Wapinzani wanatakiwa kujipanga kweli kweli katika idara zote na kuwa na timu ya strategists mahiri. Kuiondoa CCM madarakani "siyo lelemama".
 
Back
Top Bottom