Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
JK mwaka wa 2005 alipata karibu 82% lakini mwaka 2010 alipata karibu 61% likiwa ni anguko la 21%.
JPM mwaka 2015 alipata takribani 56% kwa kuangaliza anguko la JK kwa 21% basi JPM uchaguzi ujao yaani 2020 kuambulia 35%.
Kama upinzani kura zao zote wataziweka kapu moja basi hakuna jinsi mgombea wao wa UKAWA ataibuka kidedea kwa 65%.
Na jinsi uchumi unavyozidi kudorora na wapigakura wengi kuisoma namba vilivyo huku watawala hawana majibu zaidi ya kudai tunaolalama ni wapiga dili wakati kama dili zilikuwepo wachoraji ni wao basi tegemea hata hiyo 35% kushuka chini ya 30%.
Nyerere mwaka 1981 baada ya kuona kila mtu analia na ugumu wa maisha hakutulaumu bali alikuja na kauli za matumaini akiwa Kigoma alisema yafuatayo......" ....tusikubali kugeuka kuwa jiwe....na tufunge mikanda kwa miezi kumi na nane."
Ulikuwa ni utapeli wa kisiasa lakini ulimsaidia kumaliza ngwe yake ya mwisho bila vurugu na akasoma alama za wakati na kubwaga manyanga hapo 1985.
Kuwalaumu wapigakura na kuwaita wapiga dili ni kuwatusi na kukosa majibu ya kero za kiuchumi ni kuwafyagilia wapinzani wako na kujiandaa kisaikolojia kuwakabidhi dola kiulaini kabisa.