Mwanga, Kilimanjaro: Jinsi vibaka wenye silaha za jadi walivyochota Milion 16 dukani kwa mfanyabiashara

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Usiku wa Jumapili ya January 19 ,2020 majira ya saa 4 usiku , vibaka wapatao wanne wenye visu , mapanga walipora dukani kwa mfanyabiashara Milioni 16 na kutokomea kusikojulikana.

Ilivyokuwa:

Wezi waliingia nyumbani kwa mfanyabiashara huyo baada ya kugundua ameenda msikitini kuswali.

Walikaa sebuleni na kumsubiri.

Alivyoingia tu wakavimba nae. Kukuru kakara wakamkata sikio lake na hapo ndipo alipolazimika kuonyesha mzigo huo wa pesa.

Ifahamike kwamba duka na nyumba vimeungana.

Baada ya kupiga mayowe ndipo raia wema waliposogea na kuanza kumshambulia mwizi mmoja ambaye baadae alipoteza maisha.

Mwenye duka hana mlinzi, hana mke, hana mbwa na anachelewaga sana kufunga usiku.

January ni ngumu kinoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wezi sometimes wanalazimishwa kuiba kulingana na mazingira. Hata panya ukiweka kitu anachotumia exposed atapga tu kisha uanze kumlaumu
 
Wezi sometimes wanalazimishwa kuiba kulingana na mazingira. Hata panya ukiweka kitu anachotumia exposed atapga tu kisha uanze kumlaumu
Acha Ufala we mbwiga,Mwizi hata kama kakuta mlongo uko wazi bado hana right ya kuiba.
 
Wanalazimishwa na nani?Kwa nini waibe?Kwani hakuna shughuli nyingine za kufanya?Au wewe ulikuwa na maana gani kusema wanalazimishwa kuiba?

Kama alivyo panya hana haki ya kula kilichopo ndani, ukikuta anafanya hivyo piga ukiweza ua. Lakin risk kma hiz tunazipunguza kwa namna kadri iwezakavyo. Kukaa na hela nyingi ndani inafahamika siyo salama. Kama hela zina mzunguko wa kilasiku mfano huduma za miamala ya uwaka wa simu au bank inahitaji security kwa hela nyingi kama hiyo.
 
Sasa Mfanyabiashara mfano ulitaka aweke nini ndani kama siyo Pesa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom